Katika somo hili utajifunza kuhusu syntax za PHP
Katika somo hili utajifunza TAG za PHP na jinsi zinavyofanya kazi
Tulishaona katika somo lililopita namna ya kuandaa kompyuta yako na simu yako kwa ajili ya kufunguwa php. Kwa maelezo yaliotangulia katika somo la kwanza uliweza kuandaa simu ama kompyuta yako kuwa server. Katika somo hili tutakwenda kujifunza tag za php na jinsi zinavyofanya kazi.
Php ni tofauti sana na html huwenda ni kwa sababu ni lugha mbili tofauti. Hata hivyo html ina mamia ya tag kama tulivyojifunza katika mafunzo ya html level ya kwanza na pili. Php ina tag chache. Katika mafunzo ya HTML pia tulijifunza kuwa kuna tag za kufungulia na kufungia.
TAG ZA PHP
Php hufunguliwa na tag <?php na hufungwa na ?>. huwenda hizi ndio tag pekee za php zinazotumika katika kucode php. Tag hizi pia unaweza kuzifupisha kwa <? na ?> mfano
<?php
?>
Au
<?
?>
ECHO na PRINT
Ili kuweza kuandika kitu na kionekane kama tulivyotumia kwenye html, basi php inatumia echo na print. Hizi ni statement mbili za php ambazo hutumika ili kuweza kuleta matokeo kwenye browser. Yaani unapoandika code za php zinachakatwa kwenye server, kisha matokeo yake hutolewa kwenye browser kama plain teext (maandishi ya kawaida) kisha html hufanya kazi yake ya kupangilia. Sasa ili kupata haya matokeo ya code za php ambapo mtumiaji wa mtandao ataona ndipo tunatumia hizi echo na print.
Mfano katika html unapotaka kuandika neno “hallo” ili lionekane na mtumiaji wa ukurasa huo utatumia tag mfano <h1>hallo</h1>. sasa katika php utaanza tag za php ya kufunga na kufunguwa ambazo ni <?php kisha unaweka echo ama print utaweka alama ya funga semi na funguwa semi kisha ndani ndipo utaandika huo ujumbe mfano
<?php
echo “hello”;
?>
Kwa kutumia print
<?php
print “hello”;
?>
Echo na print sio tag, katika php hizi zinaitwa statement. Tutajifunza zaidi kuhusu statement katika masomo mengine. Kwa ufupi ni kuwa echo na print zinafanya kazi sawa ijapokuwa utofauti wao ni mdogo. Kwa mfano echo ipo fasta katika kuleta matokeo kuliko print. Echo pia inatumika ka">...
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utajifunza kuhusu cronjob na matumizi yake kwenye PHP
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza Jinsi ya utengeneza json data kwa utumia php
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunz akuchakata data zaidi kw akutumia ORM kama ku join table
Soma Zaidi...Katika somo hili uatakwenda kujifunza jinsi ya kutumia htaccess ili kubadili muonekano wa link ya website ama blog ili kuifanya iwe rafiki zaidi.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia PDO kutengeneza database, kuteneneza table na kuingiza data moja na zaidi ya moja.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifnza jinsi ya ku upload file kwenye database. Kisha utajifunza jinsi ya kulisoma faili hilo kwa kutumia php
Soma Zaidi...Hili ni somo la mwisho katika mfululizo huu wa ORM, kupata ujuzi zaidi endelea kusoma ORM nyinginezo ambazo nimetangulia kuzitaja awali ya masomo haya.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza jinsi ya kutengeneza table ambayo tutaitumia kwenye blog yetu
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jisniya kutuma email kwa kutumia PHPMailer kwenye project ya PHP. Katika somo hili tutakwend akutuma email kwa kutumia localhost.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza concept mpya ya abstract class na abstract method kwenye OOP.
Soma Zaidi...