Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu class inheritance kwenye object oriented programming.
Inheritance ni nini?
Hiki ni kitendo kuwa class moja inarithi property na method kutoka class nyingine. Hii inayorithi itaitwa child class yaani class toto. Katika kurithi huku tutazingatia access modifier, hivyo basi tutarithi method na property ambazo ni public au protected. Class ambayo inayorithi (inherited) huongezewa keyword extends wakati wa kuitengeneza.
Mfano:
<?php
class Gari {
}
class prado extends Gari {
}
?>
Hapo class Gari huitwa parent class na hiyo class prado huitwa child class. Sasa ngoja tuone namna ambavyo tunaweza kurithi method na property ambazo ni public ama protected.
<?php
class Gari
{
public $jina;
protected $speed;
public function __construct($jina, $speed)
{
$this->jina = $jina;
$this->speed = $speed;
}
protected function tangazo()
{
echo "Tunauza {$this->jina} yenye speed ya {$this->speed}.";
}
}
class Prado extends Gari
{
public function tangazo_jipya()
{
//method tangazo ni protected
$this->tangazo();
}
}
$Toyota = new Prado("Toyota", "180 km/h");
$Toyota->tangazo_jipya();
?>
Hapo utaona method tangazo() ni protected lakini tumeweza kuitumia kwenye child class prado(). Hii ni kwa sababu class Prado() imerithi property na method kutoka kwenye parent class Gari().
Kwa kutumia mfabo huo hata property ikiwa ni protected unaweza kuitumia ndani ya child class bila ya wasi wasi wowote.
Hapo kuna kitu kipya umekiona {$this->jina} umeona hapo tumetumia mabano {} haya hapo yametumika ili tuweze kutumia hizo property kwenye string. Hii kitaalamu inaitwa string interpolation. Angalia mfano mmoja hapo chini
<?php
$x = 4;
$b = 6;
$z = $x +$b;
echo "jumala ya {$x} na {$b} ni {$z}";
jumala ya ">...
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kusoma data kwenye database kwa kutumia PDO.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kuhusu cronjob na matumizi yake kwenye PHP
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu content-type header.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend kujifunza kuhusu static property na jnsi inavyotumika
Soma Zaidi...Katika soko hili takwenda kujufunza jinsi ya kutuma sms kwa kutumia PHP. Hii itasaidia kama unataka kutuma OTP yaqni Onetime password
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia database ya sqlite kwa kutumia PHP.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ambavyo unaweza kutengeneza blog ambayo utaweza ku upload faili na kuandika makala kwa kutumia PHP
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuandika while loop kwenye PHP
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza ni kwa namna gani utaweza kuzitumiadata za jsonkwenye program yako
Soma Zaidi...Faili la env ni moja kati ya mafaili ambayo ni muhimu kwa usalama wa project. Fili hili hutumika kuhifadhi data za siri
Soma Zaidi...