picha

PHP - somo la 1: Maana ya PHP na jinsi inavyofanya kazi

Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya PHP na jinsi inavyofanya kazi

MAFUNZO YA PHP SOMO LA KWANZA

Mahitaji ya course:
1.Uwe na kompyuta ama smartphone
2.Uwe na uelewa wa html
3.Uwe mjanga, wa kuweza kutumia simu ama kompyuta yako vyema
4.Ujuwe kusoma na kuandika
5.Kuwa na hamu ya kutaka kujuwa.


Utangulizi:
PHP ni katika lugha za kikompyuta inayotumika kwenye server. Php hutumika katika kutengeneza kurasa za wavuti kama ilivyo html. Php pia inaweza kutumika katika kutengeneza software. Php ni moja katika lugha zinazotumika sana katika blog kama wordpress na katika social media kama facebook. Php ni free kibiashara na hata binafsi.

Php ilianzishwa mwaka 1994 na mmarekani aliyejulikana kwa jina la Rasmus Lerdorf, ikiwa kama home project. Nika katika luga za kikompuata zilizo rahisi kujifunza, hata hivyo syntax yake inaweza kuwa ngumu kuliko javascript na lugha nyingine.

PHP ni nini?
Php ni kifupisho cha maneno Hypertext Preprocessor. Php hutengeneza kurasa za wavuti kama html, pia huweza kutumiwa ndani ya html ama html ikatumiwa ndani ya php. Kwa pamoja tukaweza kuhama kutokakurasa kwenda kurasa ndio maana php ikawa nayo ipo katika hypertext kama ilivyo html. Tofauti ni kuwa php kwanza code hufanyiwa processing kwenye server, kisha ndipo server hutuma matokeo kwenye browser kama html code ama plain text kwa maana hii ndipo tunapata preprocessor kwa maana kwana code zinachakatwa kwenye server kisha matokeo ndipo hutolewa kama html ama plain text kwenye browser.

 

NINI PHP HUFANYA:
1.Hutengeneza dynamic web page
2.Hutengeneza static webpage
3.Huwengeneza web App

 

Kwa ufupi php ina uweza kufanya mambo haya:-
1.Inaweza kuedit data kwenye database
2.Kuongeza na kupunguza data kwenye database
3.Kujaza fomu za madodoso
4.Kupokea taarifa kutoka katika madodoso (form)
5.Kufunga na kufunguwa database
6.Kufunguwa na kufunga mafaili
7.Kutengeneza dynamic na static web page
8.Kutengeneza system za web App

 

PHP inafanyaje kazi?
Kwanza browser inapokutana na code za php, code hizi hutumwa kwenda kwenye server. Server inachakata code za php na kurudisha matokeo kwenye browser kama plain text, na hapo html huchukuwa nafasi yake, hatimaye maudhui yanaonekana kwenye browser kama html.

Server ni nini?
Server ni kompyuta inayohudumia kompyuta nyingine. Zipo kompyuta maalumu zinafanya kazi ya kuhudumia kompyuta nyingine, lakini kompyuta yako mwenyewe pia unaweza kuifanya iwe server na kuhudumia kompyuta nyingine. Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia sikuhisi hata simu inaweza kuwa server na kuhudumia kompyuta.

Browseer yako kama chrome, firefox na opera zinaelewa html, javascript, xml, css lakini haziwezi kuelewa php. Hivyo ili code za php uweze kuzirun kwenye browser ni lazima uwe na server ambayo inachakata php na kurudisha majibu kama plain text.

 

KUIANDAA SIMU NA KOMPYUTA YAKO KUTUMIA PHP
Kama nilivyokueleza kuwa php inahitaji server. Hivyo unatakiwa uwe na App ambazo zitaweza kufanya simu yako iwe localhost server. Fuata hatuwa zifuatazo:-

1. Kwa watumiaji wa Simu

Kama wewe unatumia simu basi fuata maelekezo haya ili kuweza kuandaa simu yako kwa ajili ya mafunzo. Hapa nitakuletea list za App ambazo inatakiwa uwe nazo. List hii nimeiweka katiuka vifungu viwili ambavyo ni:-

A. Text editor: Hakikisha una moja kati ya App hizi, kama si u yako itagoma utacheki nyingine.

1. Acode - code editor | FOSS (nakushauri uchukuwe hii)

2. DroidEdit (free code editor)

3. Code Editor- Program on Mobile

 

B. Local host server Hakikisha una moja kati ya server zifuatazo:- Ila ninakushauri uwe na hiyi ya kwanza hapo.

1. AWebServer ( Http Web Server  (nakushauri uchukuwe hii)

2. KSWEB: web developer kit

3. Web Server PHP/MyAdmin/MySQL

 

JINSI YA KUANZA KUTUMIA:

1. Kwenye simu yako tengeneza fol...

Ingia sasa ili uweze kusoma makala hii yote.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: PHP Main: Masomo File: Download PDF Views 2174

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 ai web app     👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉4 web hosting     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 Dua za Mitume na Manabii    

Post zinazofanana:

PHP - somo la 48: Jinsi ya kuzuia hacking kwenye sytem ya kujisajili na ku login

Katika somo hili utajifunza jinsi ambavyo utaweza kutengeneza mfumo wa kuisajiki na ku login, kisha kuangalia usalama wa mfumo kwa kuzuia sql injection.

Soma Zaidi...
PHP somo la 80: Authentication header

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Authentication header, najinsi ya kutuma taarifa hizo na kuzisoma

Soma Zaidi...
PHP somo la 54: class constant kwenye php

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia constatnt kwenye class.

Soma Zaidi...
PHP somo la 100: Jinsi ya kutumia sql moja kwa moja kwenye ORM ya RedBeanPHP

Katika somo hili utakwend akujifunz ajinsi ya kuandika query ndani ya ORM. Hii inakupa uhuru wa kufanya kileunachotaka bila ya kuathiri usalama wa project

Soma Zaidi...
PHP BLOG - somo la 12: Jinsi ya kutumia prepared statement kwenye kusoma post za blog

Katika somo hili tutakwenda kutumia prepared ststement kwenye ku fetch data kutoka kwenye database.

Soma Zaidi...
PHP BLOG - somo la 2: Jinsi ya kutengeneza database na kuiunganisha kwenye blog

Katika somo hili unakwenda kujifunza jinsi y kutengeneza database na kuungansha kwenye blog yetu.

Soma Zaidi...