Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuandika while loop kwenye PHP
LOOP: FOR, WHILE, DO, FOREACH
Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu logical condition. Hapa tutajifunza kuweka masharti maalumu wakati wa kupata matokeo ya code.
Mfano unataka web yako iwe inasalimia kila mtu anapofunguwa. Sasa shakani zipo tatu ya asubuhi, ya mchana na ya usiku. Hivyo utaweka masharti endapo itakuwa ni asubuhi iwe inasalaminia kwa kusema habari ya asubuhi, na ikiwa ni mchana iseme habari ya mchana na ikiwa jioni iseme habari ya jioni.
Katika level 1 tulijifunza kuhusu if….. else na else if…… else. Katika level hii tutakwenda kujifunza condition zilizobakia ambazo ni: -
Ni nini maana ya loop?
Loop ni hali ya kuendelea kwa kujirudia rudia. Chukulia mfano una audio list sasa unataka ubplay moja iwe inajirudia rudia hapo utakuwa unafanya loop.
Sasa kwenye code loop ni pale code zinapojirudia rudia kufanya kazi (excute) kutokana na mashart yaliyowekwa (conditions).
Wacha tuone kwa mifano moja baada ya nyingine.
Hii ni loop ambayo code zitakuwa zinajirudia rudia kufanya kazi maadamu mashart yaliyowekwa yanaruhusu.
Mfano 1:
Tunataka kuandika kuorodhesha namba kutoka moja hadi 10. Hapo ni kuwa tutaanza kuandika kuanzia moja mpaka ifike kumi.
Inamaana kuwa namba zitaendelea kuandikwa maadamu kumi haijafikiwa. Itakapofikiwa tu basi hapo code zitawacha kufanya kazi.
Kanuni za kuandika while loop
while(shart) {
Code zinakaa hapa
}
Jinsi ya ku print tebo ya kwanza:
Kwanza tutaanza kuandaa variable. Tutaiita x kisha tuione thamani ya 0.
$x = 0;
Kisha sasa tutaweka while ndani yake shart letu ni kuwa $x iwe ni sawa ama ndogo kuliko 12. Hiyo 12 ndio mwisho wa tebo yetu. Hivyo itakuwa kama hivi while($x <=12).
Baada ya hapo tutaweka code ambazo zitakwenda kuandika tebo yetu kulingana na sharti hilo la kuwa ndogo ama sawasawa na 12. Hivyo itaonekana kama hivi {echo $x++}
Code nzima itakuwa hvi
<?php
$x = 0;
while($x <= 12){
echo $x++, "<br>";
}
?>
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowKatika somo hili utajifnza jinsi ya kufanya prepared statement kama njia ya kuzuia sql ingection kwenye PHP blog
Soma Zaidi...Hapa utajifunza jinsi ya kutengeneza table ambayo tutaitumia kwenye blog yetu
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwendakujifunza concept ya namespaces na jinsi inavyosaidi kwenye OOP
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kuhusu cronjob na matumizi yake kwenye PHP
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia PHP kutengeneza tabale kwenye database ya mysql .
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kusoma data kwenye database kwa kutumia PDO.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya PHP na jinsi inavyofanya kazi
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu static method na inavtotumika kwenye OOP
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu http header, maana yake na jinsi ya kusoma taarifa zilizopo kwenye http header.
Soma Zaidi...hapa utawenda utuma database wa ajl ya utengeneza maudhu ya PDF.
Soma Zaidi...