image

PHP - somo la 3: Maana ya variable na inavyoandika kwenye PHP

Katika somo hili utakwenda kujifunza kujusu PHP variable, maana yake na sheria za uandishi wa variable

NAMNA YA KUWEKA VARIABLE
Variable ni nini?
Ni ngumu kutoa maana ya hili neno likafahamika bila maswali, ila niseme tu kwa ufupi variable unaweza kuwema ni chombo cha kuhifadhia data kwenye program. Unaweza kuzikusanya data nyingi zinazofanana kwa kutumia variable moja.

Kwa mfano unaweza kusema neno gari likawa na mgawanyiko kama toyota, benzi, basi na pikap. Sasa badala ya kuyaida majina yao unaweza tu kuweka variable ya gari hala fu compyuta ikadisplay magariyote. Badala ya kuanza tena kutaja, majina ya magari unaweka variable gari yanakuja yote.

Cheki mfano huu:
$gari = array("basi", "benzi", "toyota","tractor", "isuzu");
echo "tunauza magari aina ya ". $gari[2].",". $gari[1].".";?>
Kwa kutumia variable gari naweza kutaja vina la gari lolote kati ya hayo bila ya kuandika jina lake halisi. Hii inasaidia kusave time.

Kanuni za kuweka variable
1.Kwanz aunatakiwa uanze na alama ya dola ambayo ni $
2.Kisha utaandika jina la variable usianze na namba
3.Kisha ruka nafasi kisha weka alama ya =
4.Kisha weka alama za kunukuu “ ”
5.Ndani ya alama za kunukuu andiak thamani ya variable yako, yaani unataka variable hiyo iwakilishe nini?
6.Weka alama ya semi colon ambayo ni ;
7.Baada ya hapo ni kuitumia variable yako.

Mafano 1
$chakula = "ugali wa sembe iliyonyeupe na samaki wa bwawani pamoja na kachumbari yenye ndimu nyingi";
echo " napenda kula $chakula";
?>

Kw akutumia mfano huu, baada ya kuyaudia maneno yaliyopo kwenye variable ambayo ni “ugali wa sembe iliyonyeupe na samaki wa bwawani pamoja na kachumbari yenye ndimu nyingi” sasa badala ya kuyaridia rudia nitatumia neno chakula kisha maneno hayo yatatolea. Haijalshi nimeyarudia mara ngapi.

Mfano 2