Njia za kuzuia Ugonjwa wa tauni.
Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuepuka Ugonjwa wa raundi.
Njia za kuepuka Ugonjwa wa tauni.
1.Kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa ugonjwa huu utokana na kuwepo kwa panya ambao ubeba wadudu na viroboto ndio wanaofanya kazi ya kusambaza hawa wadudu kwa hiyo jamii inapaswa kujulisha kuwepo kwa Ugonjwa huu maana Ugonjwa huu utokea kwa msimu na kupotea kwa hiyo kuwepo kwa Ugonjwa huu na kujua Dalili zake itakuwa rahisi kuweza kuudhibiti na kuondoa hali ya kunyanyapaa wagonjwa na watu wakishajua hilo wataweza kuwa na tahadhari.
2. Pia jamii inapaswa kuepukana na tabia ya kukubali kuwepo kwa aina yoyote ya panya kwenye mazingira yao na vilevile kama kuna mgonjwa yeyote ametokea ni lazima kutoa taarifa na kuepuka kugusa maji maji yanayotoka kwa mgonjwa ili kuepuka kuambukiza na pia kuwa mbali na mgonjwa pale ambapo mgonjwa amefikia kwenye hatua ya tatu kwa sababu ni ya hatari sana na watu uweza kuambukizwa zaidi hasa kwenye familia na wote wanaowazunguka .
3. Elimu ni lazima kutolewa kwa jamii kuhusu jinsi Ugonjwa unavyoambukiza, dalili za ugonjwa , chanzo cha ugonjwa na hatua anazopitia Mgonjwa, kwa kufanya hivyo watu watakuwa makini ili kuweza kuepuka kusambaa kwa ugonjwa wa tauni pia jamii inapaswa kuhakikishiwa juwa huu ni ugonjwa ambao unatibiwa kabisa na watu wanapona na pia wajue hatua za ugonjwa na dalili zake ili waweze kupata matibabu mapema iwezekanavyo.
4. Vile vile watu wanapaswa kuacha tabia ya kulala chini kwa sababu chini ndipo kuna viroboto wengi kwa hiyo wanashauriwa kulala kwenye vitanda na pia usafi ni wa lazima hasa katika kipindi cha mavuno kuhakikisha kuwa mazao yamewekwa sehemu nzuri ambapo panya hawawezi kufika na kushambulia mazao na kuleta madhara, au kwa upande mwingine tunapaswa kutumia dawa ili kuua panya na viroboto kwa kufanya hivyo tutaweza kuepuka Ugonjwa huu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉3 Simulizi za Hadithi Audio 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 ai web app
Post zinazofanana:
Utando wa uzazi kupanda nje (Endometriosis): Dalili na matibabu.
Endometriosis ni hali ya kiafya inayotokea pale tishu zinazofanana na utando wa ndani wa mji wa uzazi (endometrium) zinapokua nje ya mji wa uzazi, kama vile kwenye ovari, mirija ya uzazi, au viungo vingine vya nyonga. Hali hii inaweza kuwa chungu sana na kuathiri kwa kiasi kikubwa ubora wa maisha ya mwanamke. Makala hii inaangazia dalili zake, changamoto za uzazi, na njia za kisasa za matibabu.
Soma Zaidi...Maumivu ya tumbo kitovuni
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu maumivu ya tumbo kitovuni
Soma Zaidi...Homa ya matumbo (Typhoid): Jinsi ya kuepuka kurudia kwa ugonjwa.
​Homa ya matumbo (Typhoid fever) ni ugonjwa unaoambukizwa kupitia chakula na maji yaliyochafuka, ukiwa unasababishwa na bakteria aina ya Salmonella Typhi. Licha ya kupata matibabu ya dawa, wagonjwa wengi hukabiliwa na hatari ya ugonjwa huu kujirudia. Makala haya yanatoa mwongozo wa kina kuhusu namna ya kuzuia maambukizi mapya na kuelewa umuhimu wa usafi wa mazingira na chanjo katika kuimarisha afya yako.
Soma Zaidi...Kivimba kwa utando wa pua
post hii inazungumzia kuhusiana na kuvimba kwa utando wa pua unaoonyeshwa na mchanganyiko wa dalili zifuatazo: Kupiga chafya Msongamano wa pua Muwasho wa kiwambo cha sikio Kuwasha kwa pua na koromeo Uvimbe huu hutokea ikiwa mashambulizi ya kupiga chafya,
Soma Zaidi...Madhara ya kutotibu Maambukizi kwenye mifupa.
Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu Maambukizi kwenye mifupa,ni madhara ambayo utokea endapo Maambukizi kwenye mifupa yasipotibiwa kwa mda wake.
Soma Zaidi...Dalilili za pepopunda
postii hii inshusiana na dalili na matatizo ya pepopunda. Pepopunda ni ugonjwa hatari wa kutishia maisha unaosababishwa na sumu ya tetanospasmin inayozalishwa katika majeraha yaliyoambukizwa na kizuizi cha bacillus clostridia. Bakteria ya pepopunda hu
Soma Zaidi...