Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa Dengue, ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ila unasambazwa na mbu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine mbu anayasambaza Ugonjwa huu kwa kitaalamu huitwa Aedes mosquito .
1. Kama tulivyoona hapo awali kwamba hawa virusi wanasambazwa na mbu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na pia wameweza kuleta madhara makubwa katika ulimwengu kwa sababu kadri ya wataalamu mbalimbali wamefanya uchunguzi na kuona kubwa ni Ugonjwa ambao imeshambulia maeneo mbalimbali kwenye Dunia kama vile kasikazini na kusini mwa Amerika , Afrika, kasikazini na kusini mwa Asia.
2. Ugonjwa huu ushambulia kwa vipindi mbalimbali hasa hasa kwa wakati wa mvua ambapo mazalia ya mbu yanakuwa ni mengi na pengine nyasi zinakuwepo za kutosha kwenye mazingira kwa sababu ya kuwepo kwa mvua kwa hiyo mbu wanazaliana kwa urahisi, na kwenye nchi yetu ya Tanzania Ugonjwa huu umetokea tokea sana kwenye sehemu tofauti za nchi kama vile Dar es salaam na kusababisha madhara mbalimbali hata na vifo vilitokea na baadae hali ilitulia.
3. Pia ugonjwa huu unaweza kupimwa na kugundulika kulingana na uchumi wa nchi na vifaa vilivyomo, kwa hiyo tunaweza kutumia kipimo cha kuangalia mwili mzima ambapo kwa kitaalamu huitwa full blood picture na pia tunaweza kutumia kipimo ambacho kwa kitaalamu huitwa ELISA for dengue kwa kuangalia protini ya mdudu kama ikikutwa ni Dalili nzuri ya kuonesha kama kuna Dengue, au kuchukua sampuli na kuipeleka kwa mkemia mkuu wa nchi.
4. Kwa hiyo baada ya kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa huu wa Dengue ni lazima kuieleza jamii mara moja ili kuweza kujua kuwa kuna Ugonjwa fulani na kuwajulisha watu ili waweze kujua Dalili zake na namna ya kujikinga kwa sababu Ugonjwa huu hauna dawa kwa sababu unasababishwa na virusi, baada ya jamii kujulishwa tahadhari itaweza kuchukuliwa kwa urahisi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Maambukizi ya sikio mara nyingi ni maambukizi ya bakteria au virusi ambayo huathiri sikio la kati, nafasi iliyojaa hewa nyuma ya ngoma ya sikio ambayo ina mifupa midogo ya sikio inayotetemeka. Maambukizi ya si
Soma Zaidi...Katika post hii utajifunz akuhusu vidonda vya tumbo na jinsi vinavyotokea. Utajifunza pia tahadhari anazopasa mtu achukuwe na vyakula salama anavyopaswa kula.
Soma Zaidi...Makala hii itaeleza dalili za ukimwi, dalili za VVU, magonjwa nyemelezi na matumizi ya ARV
Soma Zaidi...Fangasi wanaojulikana kama Blastomyces, hawa ni fangasi wanaosababisha maradhi yajulikanayo kama blastomycosis.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dalili za maambukizi kwenye uume, ni dalili ambazo ujitokeza pale maambukizi yanapotokea kwenye uume.
Soma Zaidi...Katika post hii nitakwenda kukujuza kuhusu ugonjwa wa bawasiri
Soma Zaidi...Maumivu ya matiti yanaweza kuanzia kidogo hadi makali. Inaweza kukuathiri siku chache tu kwa mwezi, kwa mfano kabla tu ya kipindi chako, au inaweza kudumu kwa siku saba au zaidi kila mwezi. Maumivu ya matiti yanaweza kukuathiri kabla tu ya kipindi chako
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya viungo vinavyoathiriwa na ugonjwa wa malaria
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi upungufu wa damu unaosababishwa na minyoo dalili zake na namna ya kumsaidia mgonjwa mwenye tatizo hilo.
Soma Zaidi...Jipu la jino ni mfuko wa usaha unaosababishwa na maambukizi ya bakteria. Jipu linaweza kutokea katika maeneo tofauti ya jino kwa sababu tofauti.
Soma Zaidi...