Somo hili linakwenda kukuletea dalili za UTI
Dalili za UTI
1.Kukojoa mara kwa mara
2.Kuhisi kuunguwa ama umoto wakati wa kukojoa
3.Kutoa mikojo kwa uchache
4.Mkojo kuwa mchafu, kama mawingu ama mwekundu uliopauka
5.Harufu kali ya mkojo
6.Maumivu ya kwenye njonga kwa wanawake
7.Maumivu ya mkundu na puru kwa wanaume.
Dalili za UTI zinaweza pia kuwa tofauti na hizo hapo juu. Dalili hizi hutofautiana kwa kulingana na aina ya UTI. Kama unataka kuzijuwa dalili zaidi za UTI endelea kusoma makala hii mpaka mwisho.
Aina za UTI na dalili zake.
Ugonjwa wa UTI umegawanyika katika makundi mbalimbali. Makundi hayo ni kama:-
1.UTI ya kwenye figo (acute pyelonephritis). UTI hii huathiri figo, na kusababisha dalili kama:-
1.Maumivu ya mgongo kwa juu
2.Homa kali
3.Kuhisi baridi na kutetemeka
4.Kichefuchefu
5.Kutapika.
2.UTI ya kwenye kibofu (cystitis). hii ni aina ya UTI ambayo huathiri kibofu cha mkojo. Dalili zake ni:-
1.Maumivu ya nyonga
2.Maumivu ya tumbo kwa chini ya kitovu ama mvurugiko wa tumbo kwa chini
3.Kukojoa mara kwa mara huku ukiwa na maumivu.
4.Kukojoa damu, ama mkojo wenye rangi nyekundu ya kupauka.
3.UTI ya kwenye mrija wa mkojo (urethritis). mrija wa mkojo kitaalamu unaitwa urethra. Huu ndio mrija unaotoa mkojo kutoka kwenye kibofu na kuuleta nje. Dalili za UTI hii ni kuhisi kuunguwa wakati wa kukojoa.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Postii hii inshusiana na dalili na ishara za kujikinga au kuzuia malaria kwa Njia mbalimbali.
Soma Zaidi...Fangasi hawa ni maarufu sana kwa mapunye ya kichwani ama kwenye ngozi mikononi ama miguuni.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kuzuia upele, ni njia ambazo utumiwa Ili kupunguza tatizo la upele kwenye jamii, kwa hiyo jamii inapaswa kutumia njia hizi Ili kuweza kupambana na ugonjwa huu ambao unatibika.
Soma Zaidi...Malaria ni katika maradhi ambayo husambazwa na na mbu jike aina ya anopheles.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia dalili na namna ya kujikinga tusipate mafua .mafua kwa jina lingine hujulikana Kama baridi ya kawaida (common cold).baridi ya kawaida husababishwa na virusi kwenye pua na hutoa makamasi.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyanzo m ali mbali vinavyohisiwa kuwa chanzo cha UKIMWI
Soma Zaidi...Dr huwa nasikia maumivu makali sana juu ya tumbo yn kama kuna moto hivi na mgongon kama unadungwa sindano hivi je hizo ni dalili za vidonda vya tumbo?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za saratani ya ini, ni baadhi ya Dalili ambazo zinaweza kujitokeza na kuona kwamba mtu fulani ana saratani ya ini.
Soma Zaidi...Malaria husababishwa na vijidudu vidogo parasite wanaojulikana kama plasmodium. Vijidudu hivi hubebwa na mbu aina ya anophelesi. Kuna ina nyingi za plasmodium lakini aina 5 tu ndizo husababisha malaria
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kupatikana ikiwa mwili unaweza kujaa sumu, kwa sababu mwili unapaswa kuwa huru Ili kuweza kufanya vizuri kazi yake ila ikiwa utajaa Sumu Kuna hatari mbalimbali zinaweza kutokea kama vile.
Soma Zaidi...