Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kuzuia upele, ni njia ambazo utumiwa Ili kupunguza tatizo la upele kwenye jamii, kwa hiyo jamii inapaswa kutumia njia hizi Ili kuweza kupambana na ugonjwa huu ambao unatibika.
1. Kwanza kabisa tunapaswa kuoga mara kwa mara walau mara mbili kwa siku kwa wale ambao hawajapata ila kwa waliopata wanapaswa kuoga zaidi ya mara mbili au wakioga hata mara tatu sio mbaya na pia kila wanapooga wanapaswa kubadilisha nguo chafu na kuvaa nguo safi Ili kuweza kuepuka kuendelea kuwepo kwa maambukizi.
2. Pia tunapaswa kuwatafuta watu ambao Wana dalili za ugonjwa huu na kuwapatia matibabu muhimu Ili waweze kuwa vizuri Pia kuzunguka kwenye vijiji mbalimbali Ili kuwatafuta wagonjwa wote hasa hasa wale wasiopenda kwenda hospital wapewe elimu Ili waone umuhimu wa kwenda hospital.
3. Watu wanapaswa kupewa elimu kuhusu namna ya kufanya usafi kwa sababu kwa wale wanaozingatia usafi ni vigumu sana kupata ugonjwa huu kwa hiyo ni vizuri kuwajulisha njia na namna ugonjwa huu unavyosambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na jinsi ya kutibu ugonjwa huu.
4. Vile vile na mifumo ya maji inapaswa kuboreshwa Ili watu waweze kupata maji ya kutosha kwenye familia na nyumba baada ya nyumba kwa kufanya hivyo watu wataweza kufua na kuoga na maambukizi yataisha au kupunguza kwa kiasi.
5. Pia wahudumu wa afya na viongozi wanapaswa kwenda mashuleni kutoa elimu kwa watoto kuhusu namna ya kujikuna kwa sababu watoto wengi wanapata kwa kuambukizana kutoka kwa mtoto mmoja kwenda kwa mwingine na tatizo kama lipo watibiwe kwa wale walioambukizwa Ili kuepuka maambukizi kuendelea.
6. Vile vile wahudumu wa afya wanapaswa kuzunguka kutoka kwenye nyumba Moja na nyingine Ili kutibu wale wenye ugonjwa tayari.kwa hiyo jamii inapaswa kuelekezwa kuwa chanzo kikubwa cha ugonjwa huu ni uchafu na dawa kuu ni usafi kwa kujua hivyo hali itaweza kutulia na watu watapona.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Kaswende ni maambukizo ya bakteria ambayo kawaida huenezwa kwa kujamiiana. Ugonjwa huu huanza kama kidonda kisicho na maumivu kawaida kwenye sehemu zako za siri, puru au mdomo. Kaswende huenea kutoka kwa mtu hadi mtu kupitia ngozi. Kaswende ya Mapema
Soma Zaidi...post hii inazungumzia kuhusiana na kuvimba kwa utando wa pua unaoonyeshwa na mchanganyiko wa dalili zifuatazo: Kupiga chafya Msongamano wa pua Muwasho wa kiwambo cha sikio Kuwasha kwa pua na koromeo Uvimbe huu hutokea ikiwa mashambulizi ya kupiga chafya,
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Njia za kufanya Ili kupunguza maumivu ya tatizo la uti wa mgongo, ni njia unazopaswa kufanya pale unapokuwa na tatizo la uti wa Mgongo.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo kitovuni na dalili zake
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi mambo yanayochangia katika makuzi ya mtoto, mtoto katika makuzi yake anahitaji kutunzwa vizuri Ili akue kwa afya nzuri bila magonjwa
Soma Zaidi...posti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa wa Maambukizi kwenye mfupa ambao kitaalamu hujulikana Kama
Soma Zaidi...Post hii inahusu Zaidi dalili za kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu, ni dalili ambazo zinaweza kujitokeza Kwa mgonjwa,Kwa hiyo baada ya kuona dalili hizi mgonjwa anapaswa kuwahi hospital mara moja Kwa ajili ya matibabu.
Soma Zaidi...Post ya leo inaenda kufundisha dalili na hatari za presha ya kupanda. Presha ni ugonjwa unaosababishwa na baadhi ya vitu mbalimbali.pressure hujulikana kwa jina lingine ambolo ni hypertension (pressure ya kupanda). presha hugundulika pale ambapo presha ya
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia ambazo utumiwa Ili kuweza kuzuia kuwepo ugonjwa wa kisonono, kwa kufuata njia hizi ugonjwa huu wa kisonono unaweza kupungua kwa kiasi au kuisha kabisa.
Soma Zaidi...Post hii inazungumzia kuhusiana na Sababu zinazopelekea kuvimba kwa kope, kawaida huhusisha sehemu ya kope ambapo kope hukua na kuathiri kope zote mbili. Pia hutokea wakati tezi ndogo za mafuta ziko karibu na msingi wa kope huziba. Hii inasababisha kuw
Soma Zaidi...