Post hii inahusu mwendelezo wa hadithi ya Nimlaumu nani ambapo juma anapanga na madaktari wanaopima DNA ili kuweza kutambua kwamba mtu mimba ni ya kwake na sio ya Frank kwa hiyo tuendelee kusikiliza mpaka tutakapoona mimba itakuwa ya Frank au juma.
1. Kama tulivyoona kwamba juma anaenda hospitalini na kuwapatia hela nyingi wale wanaopima DNA ili kuweza kutangaza kwamba mimba sio ya Frank ni ya juma, kwa sababu juma alikuwa anazomewa na marafiki zake pamoja na ndugu kwa kufikia umri alio nao bila kuwa na mtoto hali hiyo umepata kwa sababu ya kutembea na wanawake wengi na pia mara nyingi huwa anadhulumia watoto na waume wengine, kwa hiyo alipobahatisha kwa Amisa na akakuta Frank hana hili wala lile akaamua kutaka kuchukua watoto wasio wa kwake.kwa hiyo siku zikaenda na frank akawa anajiandwa na watu wengi ndipo Amisa akaamua kumpeleka Frank chuo ili kukamilisha masomo yake aliyoachia njiani kwa sababu ya kukosa mtu wa kumlipia karo.
2. Basi Frank akaamua kwenda kusoma nchi za nje kwa kuwa alikuwa amefaulu vizuri masomo ya sayansi akaamua kuchukua udaktari wa kupima genetic kwa sababu ya tatizo aliloliacha nyumbani, kwa hiyo akaanza kusoma ila mawazo yake ni juu ya mimba yake aliyoacha inagombaniwa , Frank alipoondoka nyumbani Amisa mimba yake ilikuwa na miezi sita tu, kwa hiyo alipofika chuoni akatengeneza urafiki na balozi wa nchi yake aliyekuwa kule nje alikoenda kusomea na akamwambia inshu yote na jinsi hongo ilivyotumika ili kuweza kuwachukua watoto wake, kwa hiyo huyo balozi akawa bega kwa bega na Frank.
3. Basi siku za kujifungua zinafika na Amisa alikuwa na rafiki yake aliyekuwa anaitwa Rhoda akimsindikiza mpaka hospitali na hatimaye akajifungua mapacha wawili watoto wa kike, baada tu ya Mama kujifungua tayari madaktari wa kupima DNA wakajitokeza tayari na Amisa akawa na wasiwasi sana na akaamua kumpigia Frank simu , Frank akasema kadri ya sheria watoto upimwa DNA wakiwa na miaka mitano ila madaktari baada ya kuambiwa na Amisa hawakukubali wakajifanya ujuaji na Amisa akampigia simu Frank na baadae Frank akawasiliana na balozi na balozi akawasiliana na wizara ya afya nchini na mda mfupi polisi wakawa weka chini ya ulinzi madaktari pamoja na Juma na hatimaye wakawa weka sero na madaktari wakanyanganywa leseni kila mtu akaanza kusema NIMLAUMU NANI? Basi wakatumikia kifungo kwa mda na baadae mda ulipofika wakatolewa kifungoni na maadui wa Frank wakaongezeka mara James, Amina, Baba Amina na Juma.
4. Basi Frank akamaliza masomo na wakati ule baba Amina alifungua hospitali kubwa ya kupima genetic na hakuwa na daktari wa kusimamia hospital yake alipoangalia mtandaoni akaona kuna daktari mmoja ndiye aliye na ujuzi wa kufanya kazi ya genetic kwa hiyo akatafuta number zake akampigia simu akisema Mheshimiwa dactor Frank naomba unipe mda nije kuongea nawe basi akamwambia aje, alipofika ofisini kwa Frank alipiga magoti na kumsalimia Frank na Frank hakumtambua mara moja kama alikuwa baba Amina na baba Amina hakumtambua frank.
5. Basi wakaelewana na Frank akakubali kuwepo pale kama mkuu wa hospitali kwa hiyo baba Amina akasema inabidi wafanye mkataba wakapanga siku ya mkataba na siku hiyo baba Amina alimletea Amina Ili aweze kushuhudia basi Frank anajitambulisha na history yake kwa ufupi na katika kujitambulisha na kusema magumu aliyoyapitia akiwasihi vijana waliokuwapo pale kupambana na kutokata tamaa na kuendelea kupambana Amina alikuwa na uchungu mkubwa kwa sababu aligundua kwamba ni Frank na ukizingatia alikuwa ameolewa na James na maisha yakawa magumu na akarudi nyumbani kwao kwa hiyo kabla ya Frank kumaliza kuongea Amina aliangua kilio kikubwa na watu wakakimbia kumsaidia ili watake kujua chanzo ni nini hapo Amina akaanza kuita akisema Frank nisamehe.
itaendelea.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme, baada ya kijana wa kiume wa binti mfalme kuoa yule ndugu yake baba anafanya sherehe kubwa na wake wenza wamepata habari kwamba kijana wa kiume wa mfalme ameoa ndugu yake wakaamuru kunyamaza il
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya nne ni pale bibi anawachanganya kwa maneno yake yaani mke wa kwanza anaambiwa aandae malkia na mke mdogo atafute njia za kufanya kijana wake kuwa mfalme.
Soma Zaidi...Post hii ni mwendelezo wa hadithi ambayo Kwa jina inaitwa wakati wa Kufumbuka, ni mwendelezo wa pale maria anawekwa mbele ya wazee Ili akili kwamba John sio mtoto wa Mzee maganga ila maria akikumbuka wazi kwamba John ni mtoto wa Mzee maganga anakataa kuki
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mafundisho ambayo tunayapata kutoka kwa binti mfalme, tunapotoa hadithi sio kusoma na kufurahia tu ila kuna mafundisho muhimu katika maisha yetu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi hadithi ya Binti mfalme ni hadithi ya kusisimua, kuhusu hadithi hii ni kwamba mfalme alihitaji mtoto wa kiume ila wanawake wote hawakumpata ila alitokea mke mdogo mmoja wa mfalme akajifungua watoto wawili mapacha mmoja wa kiume na
Soma Zaidi...Hii ni siri kubwa kuhusu wanawake. Hapa utajifunza jinsi ya kumfanya mwanamke asikuache.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya sehemu ya sita.sehemu hii inaonyesha jinsi bibi alivyo ndumila kuwili na hapendi kuonekana mbaya.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi hadithi ya vijana wawili ambao walipoteana katika hali za kukimbizwa na wazazi Ili waweze kutimiza ndoto zao na siku wakakutana wakiwa watu wazima.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi vijana wawili ambao ni msichana na mvulana walioingia kwenye mahusiano wakiwa sekondari na wakahaidiana kuoana ila kwa sababu mbalimbali walizokutana nazo kwenye safari yao ya mahusiano mmoja akamsaliti mwingine na kusababisha kupo
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya mahusiano ya vijana wawili baada ya kuhamia shule mpya.
Soma Zaidi...