NIMLAUMU NANI (SEHEMU YA SITA)


image


Post inahusu zaidi hadithi ya NIMLAUMU NANI ambayo ni sehemu ya sita, katika kipengele hiki tunaenda kumwona msichana Amina anapambana na hatimaye anafunga ndoa ya kiserikali na Frank


NIMLAUMU NANI (sehemu ya sita)

1. Baada ya Frank kupewa hospitali ya genetic ili awe daktari mkuu watu wengi waliumia hasa akina juma , Amina na James, juma aliumia kwa sababu alijua kwamba Frank ni kijana ambaye hana kazi, Amina aliumia kwa sababu aliachana na Frank kwa sababu ya umaskini wa Frank na pia James aliumia kwa sababu alikuwa akimdharau Frank kama mtu maskini na ukizingatia alimyanganya msichana wake na kumbandikiza Frank kesi ya kusababisha ajali ya Amina, kwa sababu baba Amina alimpenda sana Frank na akataka amwoe binti yake Amina ila hakusema moja kwa moja ila alitamani sana.

 

2. Kwa sababu Amina alikuwa msichana mmoja mpambanaji na alikuwa hapendi kushindwa kwa hiyo akaamua kwenda shule , kwa sababu alikuwa amemaliza kidato cha nne na matokeo yake yalikuwa mazuri ila tatizo lake  alikuwa hajatulia akaenda kusoma kwa miaka miwili na akaweza kuwa msaidizi wa dakitari wa genetic ambaye ndiye Frank, kwa hiyo Amina akaanza kufanya kazi kwenye hospitali ya baba yake na kila siku Frank anapokuwa lazima afuaatane naye tu hali ambayo ilimfanya hata na Amisa kujua tatizo hilo ila  Frank hakuwa na mda naye, kwa hiyo baba Amina alipoona kwamba Amina bado anampenda sana Frank alifurahi sana, siku moja Baba Amina akaamuru kumwita Amina Ili waweze kuongea kwa karibu.

 

3.ilikuwa ni asubuhi nzuri yenye hali ya hewa inayovutia baba Amina akiwa na kikombe cha kahawa kwa sababu alizipenda mno , akamwita mwanae mpendwa Amina na kumwambia kwamba yeye umri umekwenda kwa hiyo Amina anapaswa kusimamia miradi ya baba yake na pia akamwambia angependa kuona Amina ana mwanaume ambaye ana ujuzi wa genetic wakaweza kufanya kazi pamoja,kwa hiyo baba Amina akasema nimekupa mwezi mmoja utaniletea jibu na sharti la kwanza unapaswa kuwa na mme anayejua mambo ya genetic ili kuweza kuridhi miradi ya Baba yake, kwa sababu Amina alikuwa anapenda sana hela akaanza kumshawishi Frank ili waoane na waweze kurithi ile hospitali kwa sababu na Frank alikuwa anapenda sana hela ila alimkumbuka mke wake Amisa na kuanza kulia.

 

4. Basi na siku nyingine baba Amina alimwita Frank na kumwambia kwamba angependa kumkabidhi mali yake na sharti kuu ni lazima kufunga  ndoa na Amisa , Frank aliumia sana na kumkumbuka mke wake mpenzi Amisa ,basi kwa kuwa Frank alikuwa mwungwana aliamua kumwambia mke wake kila kitu kinachoendelea kazini, Amisa alimshukuru sana mme wake kwa kumwambia na kumshirikisha mambo makubwa kama hayo, Amisa alimwambia mme wake  aende kazini mimi nitapata cha kufanya, kwa hiyo mda huo Amisa alienda kwa rafiki yake Rhoda na kumwambia kila kitu, ila Rhoda akamwambia Amisa wamwite Frank na waanze kumpa maoni na wakawa na hamu ya kumiliki ile hospitali na miladi mingine.

 

 5. Basi Frank akashauliwa kwamba anapaswa kujifanya kwamba ana uhusiano na Amina akiwa na lengo la kumwoa ila wakimaliza kusaini mikataba Frank anaweza kuendelea na kazi na hatimaye kumiliki ile hospitali na miladi mingine, basi siku iliyofuata Frank alimtumia Frank sms iliyokuwa ikisema njoo tuongee mpenzi wangu, Amina alifurahi sana kwa kuona sms ya mtu anayempenda, basi Frank akamwambia twende kwa mzee nitangaze uchumba Amisa akauliza kuhusu mmke wake Amisa huyo akamwambia usijali kwa sababu sijafunga naye ndoa na yeye ndiye aliyenilazimisha  nioe kwa hiyo Amina aliamua kukimbia kwenda kwa baba kumpasha habari njema.

Itaendelea

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    2 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    3 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    4 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    5 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    6 Magonjwa na afya    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Hadithi ya kisiwa cha mawe yanayolia
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

image Kuelekea bonde la uokozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

image Hadithi ya chongo wa kwanza mtoto wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Muendelezo wa hadithi ya mshona nguo
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Hadithi iliyosimuliwq na mlevi mbele ya sultani
Posti hii inakwenda kukusimulia hadithi iliyosimuliwa na mlevi mbele ya sultan Soma Zaidi...

image Mahusiano ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mahusiano yaliyotokea kati ya vijana wawili ila yanafika baadae mmoja akamsaliti mwenzake. Soma Zaidi...

image Mshenga wa aladini mbele ya mfalme kwa mara ya pili
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili, hapa tunaona Jackie anajibu barua ya Julius kwa kusema yafuatayo. Soma Zaidi...

image Hadithi ya chongo wa pili mtoto wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Hadithi iliyosimuliwa na tabibu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...