Home Afya Shule ICT Burudani Dini Maktaba Maswali Madrasa Apps Blog Legacy Login

MWENDELEZO WA HADITHI YA BINTI MFALME


image


Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme, tunajua kuwa mama yake na binti alimtorisha yule binti mbali kabisa ila kijana naye aliamua kutoroka na kumfuata binti mfalme na hatimaye akampata alipo.


Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme.

1. Kama tulivyoishia kwenye sehemu ya kutoroshwa kwa bibi na binti, hali hii ilimuumiza sana mtoto wa kiume wa mfalme, lakini alipoulizwa hakuweza kusema chochote , ila siku Moja mama yake aliandaa chakula kizuri alichokuwa anakipenda yule mtoto wa kiume wa mfalme akawaita na marafiki zake akampatia zawadi nzuri,akawakusanya mabinti wazuri wakawa kwenye Ile tafrija lengo la Mama ni kutaka kumfanya yule kijana asahau yule Binti Ila hayo yote yalikuwa bure, katika sherehe hiyo watu vijana wote waliamka kucheza na wale mabinti wazuri ila mtoto wa kiume wa mfalme hakucheza na Binti yoyote yule.

 

2.ilifika wakati mpaka mabinti wanamsogelea yule kijana aliwaangalia kwa dharau tu, ndipo ilipofika jioni mtoto wa kiume wa mfalme akaandaliwa chumba kizuri kama heshima ya watoto wa mfalme ndani ya chumba aliwekwa msichana mlembo yule kijana alipoingia na kumkuta alitoka chumbani akamfungia yule msichana ndani yeye akatoka nje na kwenda kulala kwa walinzi wa mfalme, mama yake alipoamka asubuhi na mapema kuangalia kwenye chumba kilichoandaliwa alishangaa kuona msichana Yuko mwenyewe kitandani amelala fofofo, mama aliumia sana na akamfungulia msichana akamruhusa aende kwa wenzake..

 

3. Baada ya mtoto wa mfalme kuwa kwenye mawazo mazito aliamuru kumshirikisha rafiki Yake maangaiko aliyo nayo moyoni ila hakumwambia kwamba yule Binti anayemtesa ni ndugu yake Bali alimwambia kuwa amehama na ajui kaenda wapi, basi yule kijana akamwambia wewe ni mtoto pekee wa kiume wa mfalme kwa nini usimwambie mfalme tatizo lako akakupatia watu wakakusaidia kumtafuta huyo Binti? Yule kijana akakubali shingo upanda alipenda Siri hii isijulikane kwa mfalme na aliogopa sana kumwumiza mama yake kwa hiyo hali ikaendelea kuwa mbaya zaidi na maisha yakaendelea kuwa magumu kwa yule kijana kwa sababu hakutaka kumwaibisha mama yake na hakupenda kuoa msichana mwingine tofauti na yule Binti.

 

4. Kadri siku zilivyoenda ndipo na Mama akaingia katika wasi wasi mkubwa na akaamuru kumwita kijana wake na kuongea naye kuhusu Sheria za ufalme ni kwamba mtoto wa kiume wa mfalme anapaswa kuoa Binti ambaye Hana undugu naye na wewe ukipenda kuoa huyu ndugu yako hautaweza kupata ufalme kwa sababu ya kufanya kitendo cha namna hiyo kwa sababu mimi nilikutambulisha kwa mfalme bila kumtambulisha dada Yako lengo ni kwamba wewe urithi ufalme wa baba Yako ila wewe bado unagangania kuoa ndugu yako, yule kijana wa kiume wa mfalme akasema Mama kama yule angekuwa ni ndugu yangu angekuwa anatambulika a kwenye familia na ukoo pia ila kwa kuwa hawamtambui mimi siwezi kukusikiliza kwa hilo kwa hiyo mama tangia mda huu mimi naenda kumtafuta yule binti popote alipo na nitamuoa na sitasikiliza chochote kutoka kwako.

 

5. Baada ya mama kuona msimamo wa kijana ni mkali mno aliwaandaa watu ili kwenda kumuua yule binti na bibi, lakini kijana akapata taarifa ndipo akaenda kwa baba yake akamuomba jeshi akiwa na lengo la kwenda kumwokoa yule binti, alimwambia baba naomba niende kusherehekea na marafiki zangu ila naomba kwenda na jeshi kusudi wanilinde, kwa kuwa baba alikuwa anampenda sana kijana wake akamuandalia chakula, nyama na vitu vyote vinavyofaa kwa sherehe akampatia na jeshi pia akiamuru jeshi limlinde na kumsikiliza kwa kila kitu atakachowaambia baada ya kufika mbele kidogo akawaambia juwa wafuatane na hao wauaji waliotumwa na Mama yake kwa sababu wanajua binti alipo.

 

6. Yule kijana akamwambia mkuu wa jeshi kwamba kabla hatujaenda kwenye sherehe tunapaswa kumwokoa mchumba wangu kutokana na wauaji na tupambane nao mpaka tumwokoe , basi mkuu wa majeshi anawapanga watu wake na wakaanza mashambulizi mpaka wakamwokoa yule binti na bibi, baada ya hapo bibi alipopata taarifa za kutaka kuuawa kwa sababu ya yule binti alisikitika sana na akaamuru kuvujisha siri hiyo kwa wake wengine wa mfalme, basi mtoto wa kiume wa mfalme akamchukua yule binti akaenda kusherehekea naye na baadae akaja naye kwa mfalme akamtambulisha kama mke wake mfalme akafurahi kwa kuona kijana wake kapata mke ila mama alikoswa amani.

 

7. Basi ikafika siku ya maandalizi ya kumsimika kijana kurithi ufalme wa baba yake kwa sababu alikuwa ni mzee, kufuatia na sheria ya kwamba mtu anayerithi ufalme ni lazima mke wake wasiwe na undugu hata kidogo na kumbuka habari imo mikononi mwa wake wenza, je unafikili watanyamaza? 

 

itaendelea



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    2 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    3 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    4 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    5 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    6 Jifunze fiqh    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS

Imeandikwa na Salvertory Tags Burudani , simulizi , ALL , Tarehe 2022/07/11/Monday - 10:41:44 pm     Share On facebook or WhatsApp Topic school Zaidi Dini AFYA ICT Burudani Tags Uzazi maswali Afya mengineyo dini HIV Sira vyakula Matunda HTML php Alif Lela 1 Alif Lela 2 FANGASI Dawa SQL Tips Quran Sunnah fiqh DARSA Magonjwa Tajwid tawhid simulizi Dua Academy Wahenga chemshabongo WAJUWA Michezo ICT Imesomwa mara 700



Post Nyingine


image Hadithi ya samaki wa Rangi nne
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image The fastest (anakwenda mbio zaidi)
Posti hii inakwenda kukuletea sifa za mnyama anayekwenda mbio zaidi Soma Zaidi...

image Historia ya pango, aladini na kitabu
Soma Zaidi...

image Jaribio la tatu la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image Kukatwa mkono na kuurithi utajiri
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Hadithi iliyosimuliwa na mshona nguo
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image UFUPISHO WA ALIFU LELA ULELA KITABU CHA KWANZA
Posti hii inakwenda kukisimulia kuhusu hadithi za alifu lela ulela KITABU CHA KWANZA Soma Zaidi...

image Ndoa ya Siri yafanyika
Posti hii inakwenda kukuendelezea hadithi kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultan Soma Zaidi...

image Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya tano
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya tano, baada ya bibi kuachana na mke mdogo wa mfalme alienda kwa kijana wa kiume wa mfalme na kuona udhaifu wake kwamba anapenda sana mali. Soma Zaidi...

image Hati.a ya kijana mchonganishi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...