Msisitizo juu ya kutoa zaka na sadaka

Msisitizo juu ya kutoa zaka na sadaka

Msisitizo wa Utoaji wa Zakat na Swadaqat katika Uislamu



1.Kutoa Zakat ni faradhi na nguzo ya tatu ya Uislamu. Amri ya kutoa Zakat ya vile Allah (s.w) alivyoturuzuku iko wazi katika Qur’an. Hebu turejee aya chache zifuatazo:


Waambieni waja wangu walioamini, wasimamishe Swala na watoe katika vile tulivyowaruzuku, kwa siri na kwa dhahiri, kabla haijafika siku isiyokuwa na (msaada unaopatikana kwa) kujikomboa wala urafiki (14:31).


Enyi mlioam ini! Toeni katika vile tulivyokupeni kabla haijafika siku am bayo hapatakuwa kujikom boa wala urafiki (wa kusaidiana) wala uombezi. Na w aliokufuru ndio w aliojidhulumu (kw eli kw eli). (2:254).



2.Utoaji wa Zakat na Sadaqat ndio kitambulisho cha Uislamu na Ucha-Mungu wa mtu kama tunavyojifunza katika Qur-an:
Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake, ni uwongozi
kwa wamchao Mwenyezi Mungu. Ambao huyaamini yasiyoonekana (maadam yamesemwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake) na husimamisha Sala na hutoa katika yale tuliyowapa. (2:2-3).



Sio wema (tu huo peke yake) kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa Mashariki na Magharibi (katika kusali,. Yako na mema mengine). Bali wema (hasa) ni (wa wale) wanaomwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na wanawapa mali juu ya kuwa wanayapenda - jamaa na mayatima na maskini na wasafiri (walioharibikiwa) na waombao na katika (kuwakomboa) watumwa, na wakawa wanasimamisha sala na kutoa zaka, na watekelezao ahadi zao wanapoahidi, na wavumiliao katika shida na dhara na (katika) wakati wa vita; hao ndio waliosadikisha (Uislamu wao); na hao ndio wamchao Mungu. (2:177)
Tunajifunza kutokana na aya hizi kuwa utoaji mali kwa ajili ya Allah ni miongoni mwa matendo yanayompelekea mtu kuwa Mcha-Mungu. Kwa ujumla Qur-an inapotaja sifa za waumini huwa ni pamoja na watoao Zakat. Kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:



Na wanaoamini wanaume na wanaoamini wanawake, ni marafiki wao kwa wao. Huyaamrisha yaliyo mema na huyakataza yaliyo mabaya, na husimamisha sala na hutoa Zakat na humtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao ndio ambao Mw enyezi Mungu ataw arehem u. Hakika Mw enyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mw enye Hikima. (9:71).



3. Utoaji mali kwa ajili ya Allah (s.w) ni miongoni mwa mambo makubwa ya kumpelekea mja kufuzu hapa duniani na huko akhera kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:


Hakika wamefuzu Waislamu. Ambao katika sala zao huwa ni wanyenyekevu. Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi. Na ambao (nguzo ya) Zakat w anaitekeleza. (23:1-4).


“..Na wabashirie wanyenyekevu ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hutetemeka na wanavumilia juu ya yale yanayowasibu na wanasimamisha swala na katika vile tulivyowapa wanatoa ” (22:34-35).


”Wale watoao mali zao usiku na mchana kwa siri na dhahiri, wana ujira wao kwa Mola wao, wala haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika”. (2:274).


4. Kutotoa mali kwa ajili ya Allah ikiwa ni pamoja na Zakat na Sadaqat ni jambo mojawapo kubwa litakalomfanya mja afeli katika maisha yake ya hapa duniani na ya huko akhera hata kama atajiita Muislamu na kutekeleza baadhi ya matendo mengine ya Kiislamu. Adhabu watakayoipata wale wenye kufanya ubakhili na kujizuilia wasitoe katika njia ya Allah (s.w) na huku wana uwezo, imewekwa bayana katika Qur’an na Hadithi. Hebu tuzingatie aya chache zifuatazo:


“Na wale wakusanyao dhahabu na fedha wala hawazitoi katika njia ya Allah, wape habari ya adhabu iumizayo. Siku (mali yao) yatakapotiwa moto w a Jahannam na kw a hayo vikachomw a vipaji vya nyuso zao na mbavu na migongo yao(na huku wanaambiwa):”Haya ndiyo (yale mali) mliojilimbikizia nafsi zenu, basi onjeni yale mliyokuw a mkiyakusanya ”. (9:34-35).


Na afanyae ubakhili, asiwe na haja ya viumbe wenzake. Na akakadhibisha mambo mema (asiyafanye) tutamsahilishia njia ya kwendea Motoni (92:8-10).
Hebu pia tuzingatie Hadithi inayotufahamisha juu ya adhabu itakayowafikia wale wanaoyafanyia ubakhili yale aliyowaruzuku Allah (s.w).



Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Yule am baye Allah (s.w) am empa m ali lakini haitolei Zakat, m ali yake itageuzw a kuwa nyoka mkubwa (mwenye sumu kali). Ataviringwa shin goni mwake katika siku ya Hisabu na kuanza kumuuma. Baadaye nyoka huyo atasema: “Mimi ni mali yako, mimi ni hazina yako iliyohifadhiwa ”. Kisha Mtume alisoma (aya ifuatayo): “Wala usiwaone wale ambao wamefanyaubakhili katika yale aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zake kuwa ni bora kwao. La, ni vibaya kwao. Watafungwa kongwa (madude ya kunasa shingoni) za yale waliyoyafanyia ubakhili- siku ya Kiyama. Na urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu. na Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyafanya ” (3:180). (Bukhari).




                   


Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1274

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 kitabu cha Simulizi    👉6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

Funga za Sunnah na umuhimu wake

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Wanaowajibika kuhijji

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Aina za twahara na aina za najisi

Katika post hii utakwenda kuzijuwa aina za twahara katika uislamu. Utaviona vigawanyo vya twahara kulingana na maulamaa wa Fiqh

Soma Zaidi...
Msimamo wa uislamu juu ya utumwa

Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Maana ya talaka na kuacha ama kuachwa

Maana ya TalakaTalaka ni utaratibu wa kuvunja mkataba wa ndoa waliofunga mume na mke wakati wa kufunga ndoa mbele ya mashahidi wawili.

Soma Zaidi...
Jinsi ya kumuandaa maiti baada ya kufa

Haya ni maandalizi ya kumuandaa maiti baada ya kufariki.

Soma Zaidi...