Umuhimu wa uchumi katika uislamu

2.

Umuhimu wa uchumi katika uislamu

2. Umuhimu wa uchumi katika Uislamu
Mwanaadamu ameumbwa na mahitajio mengi ambayo hana budi kuyapata ili aweze kuishi kwa furaha na amani hapa ulimwenguni. Kwa kuwa mwanaadamu ni mchanganyiko wa mwili na roho, pia mahitajio yake yamegawanyika, ana mahitajio ya kiroho na kimwili. Mahitajio ya kiroho ambayo humuwezesha mwanaadamu kuishi maisha ya utulivu yenye furaha na amani, hupatikana kwa kufuata kwa utii na unyenyekevu mwongozo wa Allah (s.w).



Mahitajio ya kimwili kama vile chakula, mavazi, vipando na njia ya uchumi hupatikana kwa kuchapakazi chini ya mazingira yatokanayo na itikadi sahihi yenye kusimamiwa na viongozi wanaozingatia haki itokayo kwa Muumba. Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa Allah (s.w) amejaalia mali anayoichuma mwanaadamu iwe ndiyo inayoboresha maisha yake: “Wala msiw ape w apumbavu mali zenu ambazo Mw enyezi Mungu amezijaalia kwa ajili ya maisha yenu …” (4:5)


Kutokana na aya hii, kuchuma mali si jambo la hiari kwa mwanaadamu kwani kwa namna Allah (s.w) alivyokadiria, maisha ya mwanaadamu kwa hapa ulimwenguni hayawezekani pasi na kuchuma. Ni kweli kwamba vitu vyote vilivyomzunguka mwanaadamu katika ulimwengu huu vimeumbwa kwa ajili yake kwa ushahidi wa Qur-an: “Yeye ndiye aliyekuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi…” (2:29).



Lakini mara nyingi vitu hivi haviko katika hali ya kutumiwa na mwanaadamu moja kwa moja. Bali mwanaadamu analazimika kutumia elimu yake, Maarifa yake, juhudi zake na vipawa vyake vingine ili ayabadilishe mazingira yake yaweze kumtumikia na kukidhi haja zake.
Kwa mtazamo huu Uislamu unatuamrisha kuchuma kama unavyotuamrisha kusimamisha Swala, kutoa Zakat na kutekeleza Ibada nyingine maalumu kama hizi:


Na itakapokwisha swala, tawanyikeni katika ardhi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi, ili mpate kufaulu. (62:10)
Tunajifunza kutokana na aya hii kuwa, kuchuma ni wajibu unaompasa Muislamu mara tu baada ya kutekeleza Ibada maalum. Hili linabainishwa katika Hadithi ifuatayo:
“Abdullah bin Mus ’ud ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Kutafuta chumo la halali ni faradhi baada ya kutekeleza faradhi nyingine.” (Baihaqi).
Pia Mtume (s.a.w) amebainisha wazi ubora wa kujizatiti katika kutafuta chumo la halali kwenye Hadith ifuatayo:



“Miqdam bin Ma ’ad Yakrab ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Hapana mmoja wenu aliyekula chakula kizuri kuliko kile alichokula kutokana na kazi ya mkono wake mwenyewe. Na Daud, Mtume wa Allah, alikuwa anakula kutokana na kazi ya mikono yake.” (Bukhari)



Kwa upande mwingine Uislamu unalaani uvivu na kuwategemea wengine pasi na sababu au dharura maalum kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:
“Jubair bin Awam ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Mmoja wenu kuchukua kamba na kisha akaja na mzigo wa kuni akiwa amebeba mgongoni mwake na akauuza, na kwakufanya hivyo Allah akailinda hadhi yake, ni bora kwake kuliko kuomba omba watu, wakimpa chochote au wasimpe (Bukhari.)



Mpaka hapo tumejifunza kuwa kwa mtazamo wa Uislamu, uchumi ndio msingi wa maisha ya mwanadamu hapa ulimwenguni na Uislamu umewajibisha kuchuma kwa kila mwenye uwezo. Ni makosa katika Uislamu mtu mwenye uwezo na afya kubweteka na kuwategemea wengine katika kukidhi mahitaji yake.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1486

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 Kitabu cha Afya    👉5 kitabu cha Simulizi    👉6 Dua za Mitume na Manabii   

Post zinazofanana:

Ni kwa nini riba imeharamishwa kwenye Uislamu

Hapa utajifinza uharamu wa riba na sababu za kuharamishwa kwake.

Soma Zaidi...
Sunnah za udhu

Posti hii inakwenda kukufundisha kuhusu sunah za udhu

Soma Zaidi...
Funga za Sunnah na namna ya kuzitekeleza

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Swala ya jamaa.

Kipengele hiki tutajifunza kusimamisha swala ya jamaa,swala za ijumaa.

Soma Zaidi...
Umuhimu wa swala yaani kuswali kwa mwanadamu

Kwa nini ni muhimu kuswali? Post hii itakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kusimamisha swala.

Soma Zaidi...
Fadhila za usiku waalylat al qadir

Zijuwe fadhila za usiku wenye cheo kuliko nyusiku ya miezi 1000.

Soma Zaidi...
taratibu na namna ya kutaliki, na mambo ya kuzingatia

Taratibu za Kutaliki KiislamuKama palivyo na taratibu za kuoa Kiislamu ndivyo hivyo pia ilivyo katika kuvunja ndoa.

Soma Zaidi...
Aina za swala..

Nguzo za uislamu,aina za swala (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Jinsi ya kuzika maiti wa kiislamu hatuwa kwa hatuwa

Post hii itakufundisha taratibu za kuzika maiti wa kiislamu hatuwa kwa hatuwa.

Soma Zaidi...