image

Namna ya kuswali swala ya maiti: nguzo zake, sunnah zake na maandalizi juu ya maiti

3.

Namna ya kuswali swala ya maiti: nguzo zake, sunnah zake na maandalizi juu ya maiti

Namna ya kuiswali sala ya maiti

3. Kumswalia Maiti.

Masharti ya Swala ya Maiti.
- Kwa wenye kumswalia maiti, watekeleze masharti ya kawaida ya swala.
- Masharti ya maiti anayeswaliwa:
1. Maiti awe muislamu
2. Maiti iwe imeoshwa na kukafiniwa
3. Maiti iwekwe mbele ya wanaoisalia.


- Inajuzu kusalia maiti iliyo masafa ya mbali (swala ya ghaibu).
- Maiti zikiwa nyingi zipangwe mbele, za kiume zikiwa karibu na imamu kisha kusaliwa zote kwa pamoja.
oMaiti isiwe ya shihidi.
- Kwa mujibu ya Hadith ya Mtume (s.a.w), mashahidi hawaoshwi wala kusaliwa.



Nguzo za Swala ya maiti.
- Swala ya maiti inaswaliwa wima; haina rukuu, sijda wala kikao.
- Nguzo za swala ya maiti ni;
i.Nia
ii.Takbira ya kuhirimia
iii.Kusoma Suratul-Faatiha.
iv.Takbira ya Pili.
v.Kumswalia Mtume (s.a.w) kama tufanyavyo kwenye Tahiyyatu.
vi.Takbira ya Tatu.
vii.Kumuombea dua maiti.
viii.Takbira ya Nne.
ix.Kuombea dua waislamu wote, kisha kutoa Salaam.



Namna ya kutekeleza swala ya Maiti hatua kwa hatua.
Utaratibu wa kusimamisha swala ya maiti ni kama ifuatavyo;
a)Maiti iwekwe mbele.
b)Imamu asimame katikati ya mwili wa maiti ikiwa maiti ni ya kike, na usawa wa mabega kama maiti ni ya kiume.
c)Maamuma watasimama kwenye mistari (safu) kwa idadi ya witiri; 1, 3, 5, n.k.
d)Baada ya hapo swala itaanza na kuendelea kama ifuatavyo:
i.Nia - ambayo ni kukusudia moyoni.
ii.Kuleta takbira ya kwanza; kwa kusema, “Allaah Akbar”
iii.Imamu na maamuma watasoma suratul-Faatiha – kimya kimya.
iv.Imamu ataleta Takbira ya Pili kisha maamuma – kimya kimya kwa maamuma na si lazima kuinua mikono wao.
v.Kumswalia Mtume (s.a.w) kama ilivyo katika Tahiyyatu, wote – kimya kimya.
vi.Imamu ataleta takbira ya Tatu kisha maamuma- kama walivyofanya awali.
vii.Wote kumuombea maiti dua kimya kimya, ikiwemo:


“Allaahumma ghfir lihayyinaa wamaayyitinaa washaahidinaa waghaaibinaa waswaaghirinaa wakaabirinaa wadhakirnaa waunthaanaa. Allaahumma man ahyaytahuu minnaa faahyi ‘alal Islaam. Waman tawaffaytahuu minnaa tawaffahuu ‘alal Imaani. Allaahumma laa tahirimnaa ajirahuu walaa taftinaa ba’adahuu”


Tafsiri:
“Ewe Allah tusamehe sisi, na maiti wetu, na mashahidi, na wasiokuwepo miongoni wetu, vijana wadogo miongoni mwetu na wakubwa miongoni mwetu, wanamume wetu, na wanawake wetu. Ewe Allah, yeyote yule miongoni mwetu utakayemewezesha kuishi, mjaalie aishi katika Kiislamu na yeyote miongoni mwetu utakayemfisha, mfishe katika Imani (ya Kiislamu). Ewe Allah, usitukatishe ujira kutoka kwake na wala usitufitinishe baada yake.”



- Au kwa kifupi tuweza kumuombea maiti kama ifuatavyo;
“Allaahumma ghfir lahuu warhamhuu wa-afihii wa-afu-anhu”
Tafsiri:
“Ewe Allah, Mghufirilie na Umrehemu”.



viii.Imamu ataleta Takbira ya nne na maamuma kufuatihia kama awali.
ix.Wote watawaombea waislamu dua – (pia si lazima kuleta dua hii).
Rejea Qur’an (59:10).



x.Imamu kutoa salaam na maamuma kufuatishia bila kutoa sauti kama ilivyo kwenye swala ya kawaida kwa kusema;
“Assalaamu ‘alaykum Warahmatullaah (Wabarakaatuh)”
Tafsiri:
“Amani iwe juu yenu na Rehema za Allah na Baraka zake”.



                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2956


Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Aina za talaka, sharti zake na taratibu za kutaliki katika uislamu
Maana: ni utaratibu wa kuvunja mkataba wa ndoa baina ya mume na mke mbele ya mashahidi wawili kwa kuzingatia sheria ya Kiislamu. Soma Zaidi...

Dhana ya kumiliki raslimali katika uislamu
Ni ipi raslimali ya halali kuimiliki katika uislamu. Soma Zaidi...

Kwanini wengi wanaohijji hawafikii lengo la hijjah zao
Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Namna ya kutayamamu hatuwa kwa hatuwa
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi yavkutayamamu. Soma Zaidi...

MTAZAMO NA HUKUMU YA KUPANGA UZAZI WA MPANGO KWENYE UISLAMU
Atika uislamu swala la kupanga uzazi linaruhusiwa endapo kutakuwa na sababu maalumu za kisheria. Soma Zaidi...

Yaliyo haramu kwa mwenye hadathi kubwa.
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu mambo ya haramu kwa mwenye hadathi kubwa Soma Zaidi...

Dhamana ya Kuchunga Ahadi Katika Uislamu
Kuchunga au kutekeleza ahadi ni miongoni mwa vipengele muhimu vya tabia ya muumini wa kweli. Soma Zaidi...

Eda ya kufiwa na hukumu zake
Soma Zaidi...

Jinsi ya kutoa zakat al fitiri na umuhimu wa zakat al fitri kwa waislamu
Hapa utajifunza kuhusu zakat al fitiri, kiwango chake, watu wanaostahili kupewa na kutoa, pia umuhimu wake katika jamii. Soma Zaidi...

Namna ya kujitwaharisha Najisi ndogo
Soma Zaidi...

Mambo yanayotenguwa udhu
Post hiibinakwenda kukufundisha mambo ambayo yanaharibu udhu. Soma Zaidi...

Kwa nini lengo la Hija halifikiwi?
Soma Zaidi...