nyakati za swala

3.

3. Kuchunga wakati



“... Kwa hakika swala kwa waumini ni faradhi iliyowekewa nyakati makhususi” (4:103).
Swala tano zilizofaradhishwa kwa Umma huu wa Mtume Muhammad (s.a.w) ni:- Adhuhuri, Alasiri. Magharibi, Ishai na Alfajiri. Wakati wa kuswali kila swala unabainishwa katika hadith ifuatayo:



“Abdullah Ibn ‘Amir amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema, Wakati w a sw ala ya adhuhuri ni kuanzia jua linapopinduka hadi kivuli cha mtu kin apokuwa sawa na kimo (urefu) chake. Na unamalizika kwa kuingia


Alasiri. Na muda wa swala ya Alasiri (ni kuanzia inapomalizika Adhuhuri) hadi jua linapopiga umanjano. Muda wa swala Magharibi (ni mara baada ya kuzama jua na) utabakia mpaka wingu jekundu litow eke. Muda wa swala ya Isha (ni baada ya kutoka Mgharibi) na kubakia hadi katikati ya usiku. Na wakati wa swala ya Alfajiri unaanza kwa kudhihirika kwa ukanda mweupe mpaka kabla ya kuchomoza jua. Jua linapochomoza jizuilie kusw ali kw ani huchomoza kati ya pembe za shetani. (Muslim)
Kutokana na hadithi hii, nyakati za swala tano ni:



Adhuhuri: Inayopasa kuswaliwa mara tu jua linapogeuka kuelekea Magharibi mpaka kuingia swala ya al’asiri.



Al’asiri: Huanza pale urefu wa kivuli unapokuwa sawa na kitu chenyewe mpaka kivuli kinapokuwa mara dufu ya urefu wa kitu ch en yewe.



Magharibi: Huanza mara tu jua linapozama na kuingia pale mawingu mekundu yanapobadilika kuwa ya kimanjano wakati inapoingia swala ya Isha.



Isha: Kuanzia mara tu yanapobadilika mawingu kuwa ya kimanjano mpaka usiku wa manane.



Alfajir: Huingia kwa kutokea alama ya mstari mweupe unaotokea Mashariki ambao ni alama ya kwisha kwa usiku na kuanza kwa mchana. Kuingia kwa Alfajiri kwa alama hii ya uzi mweupe ndio mwisho wa kula daku kwa mwenye kufunga kama isemavyo Qur-an:


“... Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa Alfajiri katika weusi wa usiku ...” (2:187)
Hizi ndizo swala tano na nyakati zake kama alivyotufundisha Mtume (s.a.w) ambazo hutegemea uchunguzi wa mwendo wa jua katika saa ishirini na nne za siku. Utaalamu wa karne hii umerahisisha kuzijua nyakati za mwanzo na mwisho wa kila, swala kwa kutengeneza ratiba ya nyakati za swala kwa kutumia takwimu za mwendo wa jua


katika nyakati zilizonukuliwa kwa muda mrefu na wachunguzi wa hali ya hewa.
Kuswali swala katika wakati wa mwanzo ni bora zaidi kama tunavyojifunza katika hadith ifuatayo:-
“Ummi Farawata(r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) aliulizwa, ni kitendo gani kilicho bora kuliko vyote? Akajibu: “Swala wakati wake wa mwanzo”.(Ahmad, tirm idh, Abu Daud).



Swala hukubaliwa kwa Kuwahi rakaa moja ndani ya wakati



Iwapo Muislamu kwa dharura atachelewa kuiswali swala ya faradh kiasi cha kupata rakaa moja tu ndani ya wakati,swala yake itakubaliwa kwa mujibu wa Hadith ifuatayo:
Abu Hurairah(r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: “Mwenye kupata rakaa moja ya swala ameipata swala ”.(Maimamu sahihi sita tu).
Si vizuri kabisa kwa Muislamu, kwa makusudi kuchelewesha swala kiasi hicho.



Nyakati zilizoharamishwa kuswali



Kwa mujibu wa Hadith mbali mbali kuna nyakati tano zilizoharamishwa kuswali na Mtume (s.a.w):-
1. Kuswali sunnah baada ya swala ya Alfajiri mpaka jua litakapochom oza.
2. Wakati wa kuchomoza jua mpaka litakapopanda juu kabisa kiasi cha urefu wa mkuki.
3. Jua linapokuwa katikati wakati wa mchana mpaka litakaposogea kidogo upande wa Magharibi.
4. Kuswali sunnah baada ya swala ya alasiri mpaka jua litakapozama kabisa.
5. Wakati wa kuzama jua.




                   


Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 520

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

Zijuwe funga za sunnah na jinsi ya kuzifunga

Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu funga za sunnah na jinsi ya kuzigunga.

Soma Zaidi...
udhaifu wa hoja za kuunga mkono kuzibiti uzazi na uzazi wa mpango

Udhaifu wa Hoja za Kudhibiti Uzazi:Hoja nyingi zinazotolewa kuunga mkono udhibiti wa uzazi zimejengwa juu ya hali na mazingira ya maisha yaliyoletwa na utamaduni na maendeleo ya nchi za Ulaya na Marekani.

Soma Zaidi...
Mali zinazojuzu kutolewa zaka, nisaab yake na viwango vyake

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Kutoa kati kwa kati

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Kugungisha ndoa ya kiislamu hatuwa kwa hatuwa

Hapa utajifunza jinsi ya kuozesha hatuwa kwa hatuwa. Pia utajifunza masharti ya kuoa na masharti ya kuolewa.

Soma Zaidi...
Kwa nini imefaradhishwa kufunga mwezi wa Ramadhani

Unaweza kijiuliza ni kwa nini hasa kimepelekea kufaradhishwa kufunga mwezi wa Ramadhani.

Soma Zaidi...