Maana ya Mirathi
- Ni kanuni na taratibu za kugawa mali aliyoiacha mtu aliyekufa kwa ndugu na jamaa wa karibu kinasaba waliohai kwa mujibu wa sheria za Allah (s.w).
Mambo ya Kuzingatia kabla ya Kugawa Mali ya Urithi
a) Haki zilizofungamana na Mali ya Urithi ambazo ni;
i. Madeni
ii. Zakat kama haijatolewa.
iii. Gharama za makazi ya mkewe katika kipindi cha eda au mwaka mzima kama ataamua kubakia.
iv. Usia usiozidi 1/3 ya mali iliyoachwa.
b) Sharti za Kurithi
i. Kufa mwenye kurithiwa.
ii. Kuwepo hai mwenye kurithi wakati anakufa anayerithiwa. iii. Kukosekana mambo yenye kumzuilia mtu kurithi.
c) Mambo yanayomzuilia mtu kurithi
i. Kumuua anayemrithi hata bila ya kukusudia (japo kwa bahati mbaya). ii. Kutofautiana (kuhitilifiana) katika dini kati ya mrithi na mrithiwa.
iii. Mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa hatamrithi baba aliyemzaa wala baba hatamrithi huyo mtoto.
d) Sababu za Kurithi
i. Kuwa na nasaba na marehemu anayemrithi.
ii. Kuwa katika ndoa ya halali na marehemu anayemrithi.
iii. Kuacha huru, yaani mwenye kumuacha huru mtumwa wake, ana nafasi ya kumrithi huru wake.
Mgawanyo wa Mirathi kwa Mujibu wa Qurβan (4:11-12), (4:176) ni:
a) Wanaume Wenye kurithi wako 15 kama ifuatayo;
i. Mtoto mwanamume.
ii. Mtoto mwanamume wa mtoto mwanaume (mjukuu). iii. Baba
iv. Babu wa kwa baba.
v. Ndugu mwanaume wa kwa baba na mama. vi. Ndugu mwanaume wa kwa baba tu.
vii. Ndugu mwanaume wa kwa mama tu.
viii. Mtoto mwanaume wa kwa ndugu mwanamume wa kwa baba na mama. ix. Mtoto mwanaume wa ndugu mwanaume wa kwa baba tu.
x. Ami (baba mdogo) wa kwa baba na mama (ndugu yake baba). xi. Ami wa kwa baba tu.
xii. Mtoto mwanaume wa Ami wa kwa baba na mama. xiii. Kijana mwanaume wa Ami wa kwa baba.
xiv. Mume.
xv. Bwana mwenye kumuacha huru mtumwa wake.
b) Wanawake Wenye kurithi wako 10 kama ifuatavyo;
i. Binti (mtoto mwanamke).
ii. Binti wa mtoto mwanaume (mjukuu). iii. Mama.
iv. Dada wa kwa baba na mama. v. Dada wa kwa baba.
vi. Dada wa kwa mama. vii. Bibi mzaa baba.
viii. Bibi mzaa mama. ix. Mke.
x. Bibi mwenye kumuacha huru mtumwa wake.
c) Kuzuiliana
Jumla ya wanaorithi ni 25 (wanaume 15 na wanawake 10), wanakutana wote pamoja, hawawezi kurithi wote ila baadhi yao huwazuilia wengine wasipate fungu au wapate fungu dogo. Hii ni kama ifuatavyo;
i. Mtoto mwanamume hazuiliwi na mtu
ii. Mjukuu huzuiliwa na mtoto mwanaume, na kila mtoto wa kiume aliyekaribu na marehemu humzuilia aliye mbali.
iii. Baba hazuiliwi na mtu
iv. Babu wa upande wowote huzuiliwa na baba au babu wa karibu zaidi.
v. Ndugu wa kwa baba na mama huzuiliwa na mtoto mwanamume au mjukuu au baba.
vi. Ndugu wa kwa baba huzuiliwa na ndugu wa kwa baba na mama; na kila amzuiliye ndugu wa mama, vile vile kila amzuiliaye ndugu wa kwa baba na mama akiwa pamoja na binti au binti wa mtoto wa kiume (mjukuu) au wote wawili.
vii. Ndugu wa kwa mama huzuiliwa na mtoto au mtoto wa mtoto mwanamume au baba au babu.
viii. Mume hazuiliwi na mtu ix. Mke hazuiliwi na mtu
x. Binti hazuiliwi xi. Mama hazuiliwi
xii. Bibi huzuiliwa na mama
d) Mafungu ya Urithi yako 6 ambayo ni;
i. Nusu (1/2). ii. Robo (1/4).
iii. Thuluthi (1/3).
iv. Thuluthi mbili (2/3). v. Sudusi (1/6).
vi. Thumuni (1/8)
e) Wenye Mafungu Maalumu wako 12, kama ifuatavyo;
i. Baba ii. Babu iii. Binti
iv. Binti wa mtoto mwanamume (mjukuu)
v. Ndugu wa kwa mama
vi. Dada wa kwa baba na mama vii. Dada wa kwa baba
viii. Dada wa kwa mama ix. Mama
x. Bibi
xi. Mume xii. Mke
Asaba
- Ni warithi wasiokuwa na mafungu maalum.
- Warithi hawa wanaweza kupata mali yote kama hakuna wa kurithi au kupata kilichobaki baada ya wenye mafungu kupata haki zao.
- Nao wako aina tatu;
a) Asaba kwa nafsi yake
Ni wale wanaume tu ambao uhusiano wao na marehemu haukuingiliwa na mwanamke. Nao ni;
i. Mtoto mwanamume ii. Baba
iii. Babu (baba yake baba)
iv. Ndugu wa kwa baba na mama v. Ndugu wa kwa baba
vi. Mtoto mwanaume wa ndugu wa kwa baba na mama vii. Mtoto mwanaume wa ndugu wa kwa baba
viii. Ami (baba mdogo) wa kwa baba na mama ix. Ami wa kwa baba
x. Mtoto mwanaume wa Ami wa kwa baba na mama xi. Mtoto mwanaume wa Ami wa kwa baba
xii. Bwana na bibi mwenye kumuacha mtumwa wake huru xiii. Asaba wa mwenye kumuacha mtumwa huru.
b) Asaba wa pamoja na mtu mwingine. Nao ni;
i. Binti akiwa pamoja na kijana mwanamume
ii. Binti wa mtoto wa kiume (mjukuu) akiwa pamoja na mtoto mwanaume wa mtoto mwanaume (mjukuu wa kiume).
iii. Dada wa kwa baba na mama akiwa pamoja na ndugu wa kwa baba na mama.
iv. Dada wa kwa baba akiwa pamoja na ndugu wa kwa baba.
v. Dada wa kwa baba na mama au wa kwa baba akiwa pamoja na babu.
c) Asaba kwa sababu ya mtu mwingine nao ni;
i. Dada wa kwa baba na mama au wa kwa baba tu akiwa pamoja na binti au binti wa mtoto wa kiume au wote wawili.
? Musharakah β kushirikiana fungu katika kurithi
- Ni pale ambapo asaba wana daraja sawa na wenye fungu, hivyo asaba na wenye fungu watashirikiana kugawana fungu hilo.
Kuongeza Mafungu ya kurithi (Awl)
- Iwapo idadi ya mafungu yatakayogawiwa warithi wenye mafungu maalum ni kubwa kuliko mafungu yaliyopatikana kwa njia ya K.D.S, idadi ya mafungu iongezeke ili kila mmoja apate haki yake.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Postvhiibinakwenda kukufundisha kuhusu swala ya msafiri na jinsi ya kuiswali.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza aina za biashara ambazo ni haramu.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukugundisha kuhusu swala ya ijumaa taratibu zake na jinsi ya kuiiswali.
Soma Zaidi...Quran imegawanya mirathi katika haki. Mgawanyo huu ndio unaotakiwa utumike na si vinhinevyo.
Soma Zaidi...Tumesha mzika maiti sasa imebakia mali yae nyumbani, watoto, wake na menginyeo.
Soma Zaidi...Haya ni mamno muhimu yanayozingatiwa kabla ya kuanza zoezi la kugawa mirathi ya marehemu.
Soma Zaidi...Post hii itakwenda kukufundisha kuhusi swala ya tarawehe, faida zake na jinsi ya kuiswali.
Soma Zaidi...Kabla ya kuhubiriwa uislamu watu wa Maka walikuwa na tarayibu zenye dhuluma ndani yake katika ugawaji wa mirathi.
Soma Zaidi...