Kulipia Ramadhani
Mtu anapodaiwa siku alizo kula katika mchana wa mwezi wa Ramadhani,au siku ambazo swaumu yake ilibatilika, si lazima azilipe mara tu baada ya Ramadhani, japo ni bora mtu kumaliza deni lake haraka. Tunafahamishwa katika Hadith kuwa Bibi βAysha (r.a) alikuwa akilipia Ramadhani katika mwezi wa Shaaban:
Aysha (r.a) ameeleza: βNilikuwa na madeni ya swaumu ya Ramadhani. Sikuweza kulipa kadha ila katika mwezi wa Shaaban. (Bukhari na Muslim).
Hali kadhalika si lazima mtu kulipa mfululizo siku zote anazodaiwa, bali anaweza kuzilipa kidogo kidogo kutokana na Hadith ifuatayo:
Ibn Umar (r.a) ameeleza kwamba Mtume (s.a.w) amesema juu ya kulipa Ramadhani: (Mtu) akitaka na afarikishe; na akitaka na afululize. (Daru Qu tni).
Kama mtu amechelewa kulipa siku anazodaiwa mpaka Ramadhani nyingine ikaingia, basi kwanza ataifunga hiyo Ramadhani iliyomuingilia. Baadaye ndipo alipe hiyo deni yake wala halipi fidia; iwe kuchelewa huko ni kwa udhuru ama si kwa udhuru. Lakini ni vizuri zaidi kulipa siku anazodaiwa kabla ya kuingia Ramadhani nyingine.
Umeionaje Makala hii.. ?
Kipengele hichi tutajifunza tofauti kati ua fiqh na sheria.
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha kuhusu swala ya sinnah ya tawba.
Soma Zaidi...Jifunze namna ya kuswali, zijuwe aina za swala na ujifunze masharti ya swala, kwa nini swala hazijibiwi? nini kifanyike?
Soma Zaidi...Utangulizi:Uislamu unamuelekeza mwanaadamu namna nzuri ya kuendesha maisha yake katika kila kipengele cha maisha akiwa binafsi, katika familia na katika jamii.
Soma Zaidi...Sharti za SwalaSharti za Swala Sharti za swala ni yale mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu ayachunge na kuyatekeleza kabla hajaanza kuswali.
Soma Zaidi...