image

Sharti za kutoa zaka

Masharti ya Utoaji wa Zakat na Swadaqat Utoaji katika njia ya Allah (s.

Sharti za kutoa zaka

Masharti ya Utoaji wa Zakat na Swadaqat
Utoaji katika njia ya Allah (s.w) ni ibada ambayo hukamilika kwa kuzingatia masharti yafuatayo:
(1)Kutoa vilivyo halali
(2)Kutoa vilivyo vizuri
(3)Kutoa kwa kati na kati
(4)Kujiepusha na ria na kufuatilia kwa masimbulizi
(5)Kuwapa wanaostahiki.
1. Kutoa vilivyo halali
Sharti ya kwanza ya kutoa katika njia ya Allah (s.w) ni kutoa kilichochumwa au kilichopatikana kwa njia ya halali. Mali ya haramu ni najisi na ni sumu kwa nafsi zetu. Kumlisha mtu chakula cha haramu ni kama kumlisha sumu. Ukimlisha mtu mali ya haramu utakuwa umefanya makosa mawili mbele ya Allah (s.w), kwanza, umedhulumu mali uliyoipata kwa njia ya haramu na pili umemdhulumu mtu kwa kumlisha haramu. Kula chumo la haramu kumefananishwa na kula moto:“Hakika wale wanaokula mali ya yatima kwa dhuluma, bila shaka wanakula moto matumboni mwao, na wataungua katika huo moto uwakao”. (4:10).Aidha, Allah (s.w) hapokei mali itokanayo na uchumi haramu wala hapokei ibada ya mtu ambaye anaishi kutokana na chumo haramu kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:
Abu Hurairah amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Enyi watu Allah ni mzuri na kwa hiyo hakubali ila vilivyo vizuri tu.
Na Allah ameamrisha waumini kama alivyowaamrisha Mitume wake kwa kuwaambia:
Enyi Mitume! Kuleni vyakula vizuri na fanyeni mema, hakika mimi ni Mjuzi wa (yote) mnayoyatenda” (23:51).Na Allah amesema: Enyi mlioamini! Kuleni vizuri tulivyokuruzukuni...” (2:1 72)
Kisha Mtume akaeleza juu ya mtu aliyesafiri safari ndefu mpaka nywele zake zikanyonyoka (kwa taabu na dhiki ya safari) na kufunikwa na vumbi. (Katika hali hii ya dhiki) akainua mikono yake mbinguni (na kuomba) Ee Allah! Ee Allah! ambapo chakula chake ni haramu, na kinywaji chake ni haramu na mavazi yake ni haramu, na siha yake ni haramu (imejengeka kwa chumo haramu), itawezekanaje sasa dua yake ikubaliwe? (Muslim).
Ibn Umar(r.a) ameeleza kuwa amesikia Mtume (s.a.w) akisema: Atakayenunua nguo kwa dirham kumi, ambapo dirhamu moja ni haram (imepatikana kwa njia ya haramu) Allah hatazikubali swala zake pindi atakapokuwa anasali na nguo hiyo” (Ahmad, Baihaq).
3. Kutoa vilivyo vizuri
Tunapotoa kwa ajili ya Allah (s.w) hatuna budi kutoa vilivyo vizuri kama inavyosisitizwa katika aya zifuatazo:Enyi mlioamini! toeni katika vile vizuri mlivyovichuma, na katika vile tulivyokutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msingevipokea isipokuwa kwa kutoviangalia (Basi Mw enyezi Mungu atapokea kibaya)? Basi jueni kw am ba Mw enyezi Mungu ni Mkwasi Asifiwaye. (2:267).Hamtaweza kuufikia wema (khasa) mpaka mtoe katika vile m navy ovipenda na chochote mnachokitoa, basi hakika Mw enyezi Mungu anakijua (3:92).
4.Kutoa kwa kati na kati
Muislamu anatakiwa atoe kiasi ambacho hakitamuathiri yeye pamoja na familia yake. Anatakiwa atoe kwa kipimo, atoe kila kilicho ziada ya matumizi muhimu ya maisha.Utoaji wa sadaqa hauna kiwango maalum wala nisaab, hivyo umeachwa huru ili tutoe kulingana na haja iliyopo huku tukizingatia maelekezo ya Allah (s.w) katika aya zifuatazo:
“... Na wanakuuliza watoe nini sema: ‘Vilivyokuzidien i’. Namna hivi Mwenyezi Mungu an a k u b a in is h ie n i aya (Zake) mpate kufikiri”. (2:219).Wala usifanye mkono wako kama u l i ofu n g w a shingoni mwako, wala usiukunjue ovyo ovyo, utakuwa ni mwenye kulaumiwa na kufilisika (ukiukunjua ovyo ovyo)” (17:29).
5.Kujiepusha na ria na kufuatilia kwa masimbulizi
Kutoa kwa ria ni kutoa ili kujionyesha kwa watu na ili usifiwe. Pia tunakatazwa kufuatilia kile tulichokitoa kwa masimbulizi. Kusimbulia ni kwa mfano, kuwaambia watu wasiohusika kabisa, kuwa kila kitu alichonacho fulani ni mimi niliyempa.Allah (s.w) hapokei mali iliyotolewa kwa ria au iliyofuatiliwa kwa masimbulizi kama inavyobainika katika aya ifuatayo:“Enyi m lioam ini! Msiharibu sadaka zenu kw a m asim bulizi na udhia; kam a yule anayetoa mali yake kwa kuwaonyesha watu, wala hamwamini Mwenyezi Mungu wala siku ya mwisho. Basi hali yake ni kama hali ya jabali ambalo juu yake pana udongo kisha ikalifikia (jabali hili) mvua kubwa (ikasukuma udongo wote huo) na ikaliacha tupu. Basi hawatakuwa na uweza (wa kupata) chochote katika walivyovichuma; na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu makafiri”. (2:264).
Ili kujiepusha na ria katika utoaji mali kwa ajili ya Allah (s.w) tunashauriwa katika Qur’an na Hadith kuwa ni vyema tutoe kwa siri kila iwezekanavyo hasa kwa Swadaqat na kuna malipo makubwa zaidi kwa wale wanaotoa kwa siri. Hebu turejee aya zifuatazo:Kama mkitoa Sadaqa kwa dhahiri ni vizuri; na mkitoa kwa siri na kuwapa mafakiri, basi ni ubora zaidi kwenu; na atakuondoleeni maovu yenu (mkifanya hivyo): na Mwenyezi Mungu anazo habari za (yote) mnayoyatenda. (2:2 71).Wale watowao mali zao usiku na mchana, kwa siri na dhahiri, wana ujira wao kwa Mola wao; wala haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika. (2:274).
Pia Hadith ifuatayo inaonyesha ubora wa kutoa swadaqa kwa siri: Abdullah bin Mas ’ud (r.a) aliyesimulia Hadith hii ameeleza kuwa: “Kuna watu watatu ambao Allah anawapenda mtu anayeamka usiku kusoma Kitabu cha Allah, mtu anayetoa sw adaqa kwa mkono wake w a kulia na kuuficha mkono wa kushoto (usiwe na habari); na mtu ambaye yuko katika kikosi vitani, akawa anawaendea maadui, japo wenzake wote wamekimbia” (Tirmidh).Kutokana na Hadith hii, tunaona umuhimu wa kutoa kwa siri. Kutoa kwa mkono wa kulia na mkono wa kushoto usiwe na habari ni kutoa kwa siri kwa kiasi ambacho, ikiwezekana, hata wale walio karibu sana nawe wasifahamu kuwa umetoa sadaqat kumpa fulani. Kutoa kwa siri humfanya mwenye kutoa aepukane na ria na humfanya mwenye kupokea ajisikie huru. Mtoaji Sadaqat akijificha asifahamike kabisa kwa mpokeaji ni vizuri zaidi.
6. Kuwapa wanaostahiki
Mtoaji wa Zakat na Sadaqat ni lazima awafahamu vyema wale wanaostahiki kupewa Zakat na Sadaqat. Tunahafamu kuwa Zakat na Sadaqat ni haki ya watu kupitia kwa matajiri. Hivyo, ni dhahiri kuwa kuchukua Zakat au Sadaqat na kumpa asiyestahiki ni kudhulumu haki za wale wanaostahiki. Kwa hiyo, Muislamu anaweza akatoa Zakat na Sadaqat na bado akastahiki ghadhabu za Allah (s.w.) badala ya kupata Radhi zake na malipo mema kutoka kwake, kwa kutoa mali yake na kuwapa wasiostahiki na kuwanyima haki zao wale wanaostahiki. Hii ni dhuluma iliyo wazi. Ili kuepukana na hatari hii hatuna budi kuwafahamu vyema wanaostahiki na wasiostahiki kupewa Zakat na Sadaqat.
“Sadaqat hupewa (watu hawa): Mafakiri, Maskini, wanaozitumikia (wanaozikusanya na kuzigaw anya) na wanaotiwa nguvu nyoyo zao (juu ya Uislamu),na katika kuwakom boa watumwa,na katika kuwasaidia wenye madeni, na katika njia ya Allah (s.w) na katika kuwapa wasafiri (walioharibikiwa). Ni faradhi inayotoka kwa Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hekima” (9:60).

                   

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 540


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Kumkafini (kumvisha sanda maiti)
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Usitamani kifo hata ukiwa mchamungu mno ama muovu mno
Katika uislamu imekatazwa kutamani kufa hata kama utakuwa ni mtu muovu sana ama mchamungu sana. Soma Zaidi...

Jinsi ambavyo mgonjwa anatakiwa aswali
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ambavyo mgonjwa anatakiwa aswali kulingana na ugonjwa wake. Soma Zaidi...

Aina za Najisi na twahara katika uislamu
Post hii inakwenda kukufundisha aina za najis. Pia utajifunza aina za twahara katika uislamu Soma Zaidi...

Funga za suna na funga za kafara na nadhiri: Masharti yake, nguzo zake na wakati wa kutekeleza
Funga za Sunnah. Soma Zaidi...

.Mazingatio muhimu katika uchumi wa Kiislamu
3. Soma Zaidi...

Umuhimu wa uchumi katika uislamu
Post hii itakufundisha faida na umuhimu wa kijenga uchumi katika jamii ya kiislamu. Soma Zaidi...

Jinsi ya kujitwaharisha Najisi hafifu na najisi ndogo
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kujitwaharisha kutokana na najisi hafifu na najisi ndogo. Soma Zaidi...

Zifahamu njia za kutwaharisha, aina za maji, udongo na Namna ya kujitwaharisha
Soma Zaidi...

Nguzo za kufunga ramadhani
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

nyakati za swala
3. Soma Zaidi...

Njia haramu za uchumi.
Njia hizi ni haramu katika kukuza uchumi wako. Soma Zaidi...