Ni zipi Nguzo za Udhu au Kutawadha
Nguzo za Udhu
Allah (s.w) anatufunza kutia udhu katika aya ifuatayo:
Enyi mlioamini! Mnaposimama ili mkaswali, basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na (osheni) miguu yenu mpaka vifundoni...” (5:6)
Kutokana na aya hii na kutokana na mafundisho ya Mtume (s.a.w) nguzo au faradhi za udhu ni hizi zifuatazo
1. Kutia nia moyoni kuwa unatawadha.
2. Kuosha uso kwa ukamilifu kwa kufikisha maji mpaka kwenye mipaka yote ya uso.
3. Kuosha mikono miwili mpaka vifundoni.
4. Kupaka maji kichwani.
5. Kuosha miguu, mpaka vifundoni.
6. Kufuata utaratibu huu kwa kuanza (1) hadi (5) katika mfuatano huu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 ai web app 👉3 Dua za Mitume na Manabii 👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉5 Kitau cha Fiqh 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Aina 12 za swala za sunnah na idadi ya rakaa zake wakati wa usiku na mchana
Aina za Swala za Sunnah.
Soma Zaidi...