Lengo la Kusimamisha Swala
Bila shaka swala imepewa umuhimu mkubwa kiasi cha kufanywa nguzo kubwa ya Uislamu kutokana na lengo lake. Lengo la swala limebainishwa katika Qur-an kama ifuatavyo
“Soma uliyoletewa wahyi katika kitabu (Qur-an) na usimamishe swala. Bila shaka swala (ikiswaliwa vilivyo) humzuilia (mwenye kuswali na) mambo machafu na maovu, na kw a yakini kumbuko la Mw enyezi Mungu (lililomo ndani ya swala ni jambo) kubwa kabisa (la kumzuilia mtu na mabaya). Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyatenda.” (29:45).
Kutokana na aya hii tunajifunza kuwa lengo la kusimamisha swala ni kumtakasa mja na mambo machafu na maovu. Kwa maana nyingine, tunajifunza kuwa swala ikisimamishwa vilivyo, humfanya msimamishaji awe mtu mwema mwenye kutakasika na mambo machafu na maovu na mwenye kuendea kila kipengele chake cha maisha kwa kumtii Allah (s.w). Labda tujiulize swali: “Ni nguvu gani au ni msukumo gani uliomo katika swala unaomfanya mwenye kuswali atakasike na maovu na awe na tabia njema anayoridhia Allah (s.w)” Linaloleta mabadiliko haya makubwa katika tabia na utendaji wa Muumini, ni lile kumbuko la Allah (s.w) lililomo ndani ya swala. Kwa hiyo lengo hili la swala litapatikana tu pale mwenye kuswali atakapokuwa na mazingatio na kumkumbuka Allah (s.w) katika kila hatua ya swala.
Umeionaje Makala hii.. ?
Hapa utajifunza taratibu za kutaja mahari katika uislamu.
Soma Zaidi...Zaka, kilugha ni kukua; kubariki na kuzidi kheri.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi yavkutayamamu.
Soma Zaidi...Maana ya elimuElimu ni ujuzi ulioambatanishwa na utendaji.
Soma Zaidi...- Watumwa walikuwa wakikamatwa na kutezwa nguvu bila kujali utu na ubinaadamu wao.
Soma Zaidi...Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...