KUSOMA TAHIYATU NA KUMSWALIA MTUME KWENYE SWALA

11.

kUSOMA TAHIYATU NA KUMSWALIA MTUME KWENYE SWALA

11. Kusoma Tahiyyatu
Kusoma tahiyyatu ni nguzo ya swala. “Tahiyyatu” ina maana ya “Maamkizi”, ukiwa umekaa kikao cha tahiyyatu unaleta maamkizi kama ifuatavyo: “Attahiyyaatu lillaah, wasw-swalawaatu, watwa-yyibaatu, assalaamu ‘alaika ayyuhannabiyyu, warahmatullaahi wabarakaatuhu, assalaamu ‘alay-naa wa-’alaa ‘ibaadillaahi swswaalihiina. Ash-hadu an-llaailaaha illallaahu wa-ash-hadu anna Muhammadan ‘abduhuu warasuuluhu”. “Maamkizi yote ni ya Allah, na swala zote na yote mazuri, Amani iwe juu yako, ewe Mtume na Rehma na Baraka za Allah. Na amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Allah. Ninashuhudia kuwa hapana Mola ila Allah. Na ninashuhudia kuwa Muhammad ni Mja na, ni Mtume wake”. (Muslim).

12. Kumswalia Mtume (s.a.w).
Kumswalia Mtume (s.a.w) ni nguzo ya swala inayofuatia baada ya kusoma Tahiyyatu. Kumswalia Mtume si faradhi katika swala tu bali pia ni faradhi kumswalia kila anapotajwa kwa jina lake. Msisitizo wa amri ya kumswalia Mtume unaonekana katika aya ifuatayo:

“Hakika Mwenyezi Mungu anamteremshia Rehema Mtume; na Malaika wake (wanamuombea dua). Basi; enyi Mlioamini msalieni (Mtume, muombeeni Rehema) na amani”. (33:56)

Pia hadithi zifuatazo zinasisitiza umuhimu wa kumswalia Mtume (s.a.w) kila atajwapo na kila mtu apatapo wasaa. Ali (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Bakhili ni yule anayesikia nikitajwa, lakini haniswalii. (hanitakii rehma). (Tirmidh).

Abu Hurairah amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Anayenitakia Rehma (anayeniswalia) mara moja, Allah humrehemu mara kumi”. (Muslim).

“Ibn Mas’ud amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Atakayekuwa kipenzi changu katika watu, katika siku ya Kiama atakuwa ni yule aliye mbele kuliko wote katika kunitakia Rehma (kuniswalia). (Tirmidh).

Namna ya kumswalia Mtume (s.a.w) imeelezwa katika Hadithi nyingi lakini iliyomashuhuri katika hizo ni ile iliyosimuliwa na Abdur- Rahman bin Ubaidillah(r.a) na kupokelewa na Maimamu wote wa Hadithi kuwa Mtume (s,.a.w) ametufundisha tumswalie (tumtakie Rehma) kama ifuatavyo;

“Allahumma swalli ‘alaa muhammad wa’alaa aliy Muhammad kamaa swallaita ‘alaa ibraahima wa’alaa ali ibraahim innaka hamiidum-majid. Wabaaik ‘alaa muhammad wa’alaa ali muhammad kamaa barakta ‘alaa ibraahima wa’alaa ali ibraahima innaka hamiidum-majid”

Ewe Mola mrehemu Muhammad na wafuasi wake kama ulivyomrehemu Ibrahim na wafuasi wake hakika wewe ni mtukufu na msifiwa wa haki. Ewe Mola mbariki Muhammad na wafuasi wake kama ulivyombariki Ibraahim na wafuasi wake hakika wewe ni wewe ni mtukufu na msifiwa wa haki.


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Jiunge nasi WhatsApp
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 12502

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Dua za Mitume na Manabii    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

Ni ipi hukumu ya kutoa talaka hali ya kuwa umelazimishwa au ukiwa umerukwa na akili

Endapo mtu atamuacha mke pasi na ridhaa yake yaani amelazimishwa ama amemuwacha wakati amerukwa na akili. Je ni ipo hukumu yake.

Soma Zaidi...
Usawa na uhuru wa kuchuma mali katika uislamu

Uchumi wa uislamu umeweka taratibu mbalimbali katika kuchuma mali.

Soma Zaidi...
MAMBO YANAYOBATILISHA (HARIBU) SWALA YAKO

Lugha ya Swala Lugha ya swala,kuanzia kwenye Takbira ya kuhirimia Swala mpaka kumalizia swala kwa Salaam, ni Kiarabu.

Soma Zaidi...
Jinsi ya kutwaharisha Aina mbalimbali za Najisi katika uislamu

Katika somo hili utakwedna kujifunza jinsi ya kutwaharisha aina mbalimbali za najisi kwa mujibu wa mafundiso ya Mtume Muhammad (s.a.w)

Soma Zaidi...
Nini maana ya funga na ni lipi lengo lake

Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu lengo la funga na maana yake katika uislamu.

Soma Zaidi...
Maswali juu ya Mambo anayopaswa kufanyiwa maiti ya muislamu

Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...