image

Njia za kudhibiti riba

Ufumbuzi wa tatizo la ribaRiba imeenea na kuzoeleka duniani kwa kiasi ambacho watu wengi wanadhani kuwa bila riba hakuna shughuli yoyote ya uchumi inayowezekana.

Njia za kudhibiti riba

Ufumbuzi wa tatizo la riba
Riba imeenea na kuzoeleka duniani kwa kiasi ambacho watu wengi wanadhani kuwa bila riba hakuna shughuli yoyote ya uchumi inayowezekana. Riba imechukuliwa kuwa kama motisha (faida) kwa mwenye kuruhusu fedha zake zitumiwe na mtu mwingine. Hivyo mikopo kutoka kwa watu, makampuni, mabenki, mashirika ya bima n.k. haipatikani bila riba. Hivi sasa mikopo karibu yote duniani haitolewi bila riba. Mikopo hii kwa kawaida imegawanywa katika makundi mawili:
(a)Mikopo ya muda mfupi
(b)Mikopo ya muda mrefu



Tatizo hasa la riba linaonekana katika aina ya pili ya mikopo (yaani mikopo ya muda mrefu) Hii ni kwa sababu kiasi cha riba huongezeka mwaka hadi mwaka pengine kuzidi hata fedha zilizokopeshwa mwanzoni. Aidha katika mikopo hii, baya zaidi ni kuingizwa kwa rahani na hatari iliyopo ya mkopeshwaji kunyang’anywa mali aliyoweka rahani pindi atakaposhindwa kulipa deni kwa muda uliopangwa. Uislamu ukifuatwa vilivyo, tatizo hili haliwezi kujitokeza kwani mwenye fedha analazimishwa kufanya moja kati ya yafuatayo kwa mwenye kuhitaji fedha hizo:



(a)Kumkopesha bila riba kwa muda watakaokubaliana. (Ama kwa kuweka au kutoweka rahani mali yake).
(b)Kushirikiana katika mtaji na kugawana gharama za uendeshaji, faida na hasara.



(a) Kukopesha bila riba
Uislamu ni mfumo kamili wa maisha alioufuma Allah (s.w.) na ni muhali kwa Allah (s.w.) kuwalazimisha wanaadamu kufanya jambo wasiloliweza. Amekataza riba na kuruhusu biashara kwa sababu anafahamu kuwa riba inaweza kuepukika na biashara kufuatwa. Aidha uislamu unawaruhusu watu kukopeshana. Mtu anaweza kumkopesha mwingine fedha ama kwa kutumia (matumizi ya kawaida katika maisha), au kwa kumsaidia mtaji kufanyia biashara. Kwa hali yoyote itakavyokuwa mwenye kukopesha (mtoa fedha) analazimika kudai kiasi kile kile alichotoa kwa muda waliokubaliana bila ya kudai nyongeza yoyote. Sheria iliyopo katika Uislamu katika kukopeshana ni deni hilo kuandikwa (hata kama ni dogo) mbele ya mashahidi waadilifu. Allah (s.w.) hata hivyo ametoa ruhusa ya kukopeshana bila mwandishi kwa njia ya kuweka vitu rahani. Anayathibitisha haya Mwenyezi Mungu pale anaposema:



“Na kama hamkupata mwandishi basi (mdai) apew e (astakabadhishwe) (kitu kiwe) rahani mikononi mwake. Na kama mmoja wenu amewekewa amana na mwenzake basi aliyeaminiwa airudishe amana ya mwenzake, na amche Mwenyezi Mungu Mola wake. Wala msifiche ushahidi (japo juu ya nafsi zenu) Na atakayeficha basi hakika moyo wake ni wenye kuingia dhambini. Na Mwenyezi Mungu huyajua mnayoyatenda.” (2:282).



(b) Ushirika katika biashara
Uislamu unaruhusu watu kufanya biashara kwa shirika maadamu wanachunga sheria zilizowekwa (za Uislamu). Ushirikiano katika biashara unaweza kuwa wa watu wawili au zaidi. Mara nyingi wanaoshirikiana huchangia katika mtaji wa biashara yao. Pindi watu wakikubaliana kufanya biashara kwa shirika Uislamu unawalazimisha kushirikiana vile vile katika gharama, faida au hasara itakayopatikana. Hii hutegemea kiasi gani kila mshirika amechangia katika biashara hiyo. Ushirikiano mwingine wowote usiokuwa katika mtaji utategemea makubaliano ya washirika. Hebu tutazame ni kwa jinsi gani ushirika katika mtaji wa biashara unavyoweza kutumika badala ya mikopo ya rahani yenye riba.



(i)Mikopo inayopatikana kwa rahani (Mortgages). Kupata mkopo kwa kitu rahani si haramu katika Uislamu kama ilivyokwishabainishwa katika Qur’an. Hata Mtume Muhammad (s.a.w.) aliwahi kufanya hivyo kama tunavyofahamishwa katika Hadithi ifu atayo:



Bi Aisha (r.a) amesimulia kuwa: Mtume (s.a.w.) alinunua vyakula kwa mkopo kwa muda maalum na aliweka rahani (arm our) zake kwa ajili hiyo (Bukhari).
Wanyama wafugwao vile vile wanaweza kuwekwa rahani kwa ajili ya mkopo. Wanyama hawa wanaweza wakatumika hata kama bado wapo rahani. Hadithi ifuatayo inatuthibitishia hayo:



Abu Hurairah (r.a) amesimulia: Mtume wa Allah amesema: “Mnyama aliyewekwa rahani anaweza kutumika kuendeshwa maadamu analishwa na maziwa ya mnyama atoaye maziwa yanaweza yakanyewa kulingana na kiasi mtu anagharimika juu yake. Yule anayemwendesha mnyama au kunywa maziwa yake hana budi kugharimia mahitaji ya mnyama huyo”. (Bukhari).



Kinyume na utaratibu huo hivi sasa rahani hutumika katika kupata mikopo ya muda mrefu. Mikopo hii huweza kutolewa na makampuni ya bima au makampuni ya akiba. Kitu kinachowekwa rahani huhesabiwa kama dhamana ya mkopo uliotolewa. Kwa kawaida kitu kinachowekwa rahani ni kile ambacho kinaeleweka kuwa kina uwezo wa kuzalisha mathalani nyumba au mashine. Mkopo hulipwa na riba. Kama aliyekopeshwa atashindwa kutoa riba au malipo ya fedha za mkopo basi mkopeshaji huhesabiwa kuwa ana haki ya kuchukuwa mali ya dhulma iliyo bayana kwa aliyekopeshwa.



c) Ushirika katika mtaji badala ya mikopo ya rahani yenye riba
Mtu anaweza kupata fedha kwa njia hii bila kutoa riba. Njia hii inawezekana tu kwa kuwafanya watu wengine wawe wanashirika katika mali/kitu ambacho kingewekwa rahani kwa kuchangia katika thamani ya kitu hicho kwa njia ya kununua hisa (shared equity). Watu hawa wataridhia iwapo watafahamu hisa walizonazo katika mali/kitu hicho. Iwapo kwa mfano kitu hicho ni nyumba kodi itakayopatikana ni lazima igawanywe kwa wenye hisa wote (baada ya kutoa gharama za uendeshaji). Mwenye nyumba au mwenye nyumba mtarajiwa (the owner to be) atakubaliana na washiriki hao kununua hisa zao hatua kwa hatua mpaka hisa zote zitakapokuwa zake (yani nyumba itakapokuwa mali yake). Njia hii hutekelezwa kwa kufuata hatua zifuatazo:

(i) Makisio ya thamani ya kitu na idadi ya hisa. Kitu ambacho kilifikiriwa kuwekwa rahani ili kupata mikopo hufanyiwa utafiti wa bei ambayo ingeweza kuuzwa.Hii huchukuliwa kama thamani ya kuridhisha ya kitu hicho. Ni thamani hii ndiyo itakayogawanywa kwa watakaokuwa na hisa (akiwemo atakayekuwa mwenye nyumba) Thamani ya kila hisa huamuliwa na huyo mwenye kutafuta fedha kwa wengine.



Thamani ya kitu na thamani ya kila hisa ndivyo vitakavyoonesha idadi ya hisa. Iwapo thamani ya nyumba, mathalani ni shilingi 2,000,000 na thamani ya hisa moja ni shilingi 100,000 idadi ya hisa itakuwa



(ii)Kutafuta mtaji wa mwanzo wa atakayekuwa mwenye mali. Atakayekuwa mwenye mali lazima afahamu kiasi cha mtaji au hisa atakazokuwa nazo mwanzoni kabla ya kutoza hisa nyingine kwa wengine.



(iii)Kufahamu idadi ya hisa za washirika wengine. Idadi ya hisa za washirika wengine katika mali inapatikana kwa kugawa thamani ya hisa zote kwa thamani ya hisa m oj a.


(iv)Kufahamu mapato (kabla ya kutoa gharama) na mapato halisi (baada ya kutoa gharama za uendeshaji). wa mali. Mapato ya mali ambayo ilikusudiwa kuwekwa rahani kwa ajili ya kupata mkopo lazima yafahamike. Mapato kwa ajili ya nyumba kwa kawaida huwa ni kodi ya nyumba (rental charge). Thamani ya mapato hayo (gross rental value) si yote yanayogawanywa kwa wenye hisa katika mali. Kuna umuhimu wa kutoa gharama zote za uendeshaji.



(v)Mapato yaliyobaki baada ya kutoa gharama za uendeshaji, hugawanywa kwa wenye hisa kulingana na idadi ya hisa mtu alizonazo katika mali ile.
Itaonekana wazi kuwa njia hii haihusu riba kwa namna yoyote ile. Tofauti zinazojitokeza kati ya njia hii na ile ya kukopa kwa kuweka vitu rahani ni:



1)Mali humilikiwa na wenye hisa wote mpaka hapo atakayekuwa mmilikaji atakapomaliza kununua hisa za wengine wote.
2)Wenye hisa wote wana haki ya kugawana (kulingana na hisa mtu alizo nazo) mapato yanayotokana na mali hiyo na pia wana wajibu wa kushiriki katika gharama zote za uendeshaji.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 742


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Msimamo wa uislamu juu ya utumwa
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Waislamu wanaolazimika kufunga
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Namna ya kuswali swala ya maiti: nguzo zake, sunnah zake na maandalizi juu ya maiti
3. Soma Zaidi...

Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawa mirathi
Haya ni mamno muhimu yanayozingatiwa kabla ya kuanza zoezi la kugawa mirathi ya marehemu. Soma Zaidi...

Mambo yanayoweza kutoa udhu wako
Post hii itakufundisha mambo ambayo yanabatilisha udhu. Soma Zaidi...

Sanda ya mwanamke na namna ya kumkafini
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Jinsi ya kutwaharisha aina mbalimbali za najisi
Kila najisi ina namna yake ya kutwaharisha, hata hivyo namna hizo hufanana. Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutwaharisha najisi mbalimbali. Soma Zaidi...

Jinsi ya kutekeleza funga za sunnah
Hapa utajifunza muda wa kutia jia katika funga za sunnah. Pia utajifunza kuhusu uhuru ulio nao Soma Zaidi...

Jinsi ya kuzika maiti wa kiislamu hatuwa kwa hatuwa
Post hii itakufundisha taratibu za kuzika maiti wa kiislamu hatuwa kwa hatuwa. Soma Zaidi...

haki na hadhi za mwanamke katika jamii inayoishi kiislamu
Soma Zaidi...

Maneno mazuri mbele ya mwenyezi Mungu
kuna adhkari nyingi sana ambazo Mtume wa Allah ametutaka tuwe tunadumu nazo. lajkini kuna adhkari ambayo imekusanya maneno matukufu na yanayopendwa sana na Allah. Soma Zaidi...

Ujuwe utaratibu mzima wa funga na kutekeleza ibada ya Swaumu
Soma Zaidi...