namna ya kuswali swala ya vitani

namna ya kuswali swala ya vitani

Kusimamisha Swala VitaniMuislamu haruhusiwi kuswali swala ya faradhi nje ya wakati wake hata akiwa katika vita vya kupigania Dini ya Allah(s.w). Bali Allah (s.w) ametuhafifishia swala, tukiwa vitani na kutuelekeza tuswali ifuatavyo:


'Na unapokuwa pamoja nao (Wa is lamu katika vita) ukawaswalisha, basi kundi moja miongoni mwao wasimame pamoja nawe (waswali) na washike silaha zao. Na watakapomaliza sijda zao basi na wende nyuma yenu (kulinda); na lile kundi jingine ambalo halijaswali lisw ali pamoja naw e, nao washike hadhari yao na silaha zao (humo ndani ya swala, maana) wale waliokufuru wanataka mghafilike na silaha zenu na vitu vyenu ili wakuvamieni mvamio wa mara moja. Wala si vibaya kwenu ikiwa mnaona udhia kwa sababu ya mvua au mnaona ugonjwa, kuondoa silaha zenu,.


Na mshike hadhari yenu. Hakika Mwenyezi Mungu amewaandalia makafiri adhabu itakayowadhalilisha'. (4:102)
Namna ya kusimamisha swala katika uwanja wa vita kutokana na maelekezo ya aya hii ni kwamba, askari wagawanyike katika makundi mawili ambayo yataswalishwa na Imamu mmoja na swala itafupishwa kama ilivyo katika swala ya safari. Kundi moja litaanza kuswali na Imamu wakiwa na silaha zao na kundi lingine litabaki katika ulinzi. Imamu ataswali rakaa moja na hili kundi la kwanza na watakaponyanyuka kuswali rakaa ya pili Imamu atabakia pale akiendelea kusoma Qur-an na kila mtu katika wale wanaomfuata, atamaliza upesi upesi rakaa ya pili na baada ya kutoa Salaam atarudi nyuma upesi kuchukua nafasi ya ulinzi. Baada ya kundi la pili kupokelewa nafasi zao, watakwenda kujiunga na Imamu ambaye bado anaendelea na rakaa yake ya pili. Wote watakapojiunga na swala, Imamu atamalizia swala yake ya rakaa mbili. Baada ya Imamu kutoa salaam kila mmoja katika wale wanaomfuata atasimama na kumalizia rakaa yake ya pili.Aya hii ya (4:102) inayotuelekeza namna ya kuswali tukiwa katika vita vya kupigania Dini ya Allah (s.w) inafuatiwa na aya inayotoa amri ya kusimamisha swala kwa nyakati zake kama tunavyosoma:


Mwishapo kuswali kuweni mnamkumbuka Mwenyezi Mungu - msimamapo na mkaapo na (mlalapo) ubavu. Na mtakapopata amani, basi simamisheni swala (kama kawaida). Kwa hakika swala kw a Waislamu ni faradhi iliyow ekewa nyakati maalumu. (4:1 03)Hebu fikiri: Kama askari wa Allah (s.w) aliyejitoa muhanga kwa mali yake, ahli zake na nafsi yake kwa ajili ya kupigania dini ya Allah (s.w) hakuruhusiwa kuiacha swala au kuiswali nje ya wakati wake, je wewe uliyezama kwenye shughuli nyingine ndio utegemee kusamehewa kwa kupitisha wakati wa swala ukaswali wakati unapojiona kuwa huna shughuli. Aya hii inatufahamisha kwa uwazi kuwa swala tano zimefaradhishwa kwetu pamoja na nyakati zake makhsusi.Tukiondoa ruhusa tulizopewa kuziswali swala kidharura tunapokuwa vitani, na tukiondoa udhuru wa kusahau na kupitiwa na usingizi hapana ruhusa yoyote iliyotolewa katika Qur-an au Hadithi inayokubalika kuswali kadha kama wengi wafanyavyo. Je, mtindo huu wa kuswali kadha tunauiga kwa nani? Je, huku sio kupuuza swala? Kama tunapuuza swala kwa nini tusitarajie kupata ghadhabu za Allah (s.w) badala ya kujidanganya na kujipa matumaini ya kupata malipo mema kutoka kwake kutokana na kadha zetu hizo. Ujira wa wapuuzaji wa swala unabainishwa katika Qur-an:


Basi, adhabu itawathibitikia wanao swali. Ambao wanapuuza zao. (10 7:4-5).
                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 184

Post zifazofanana:-

Faida za Kuwa mwenye Subira na Uvumilivu
29. Soma Zaidi...

Kufunga Mwezi wa ramadhani kisheria
Soma Zaidi...

Kitabu Cha Dua 120
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

mgawanyiko wa elimu
Soma Zaidi...

Madai ya Makafiri Dhidi ya Qur'an na Udhaifu Wake
i. Soma Zaidi...

MAANA NA FADHILA ZA DUA
DUA Kwa ufupi dua ni kumuomba Allah akuondoshee lililobaya, ama linalo kuudhi ama akupe jambo fulani. Soma Zaidi...

Eda ya kufiwa na hukumu zake
Soma Zaidi...

Himizo la kuwasamehe waliotukosea
'Na wasiape wale wakarimu na wenye wasaa miongoni mwenu, kujizuia kuwasaidia jamaa zao, maskini na wale waliohama kwa ajili ya Dini ya Allah; na wasamehe na waachilie mbali (wapuuze yaliyopita). Soma Zaidi...

Kutowatii Wazazi katika kumuasi Allah (s.w)
"Na (wazazi wako) wakikushurutisha kunishirikisha na (yale) ambayo huna ilimu nayo, usiwatii; lakini kaa nao kwa wema hapa duniani (Maadamu ni wazee wako, ila usiwafuate tu mwenendo wao mbaya); Shika mwenendo wa wale wanaoelekea kwangu, kisha marejeo yenu Soma Zaidi...

nyakati za swala
3. Soma Zaidi...

Kuandaliwa Mtume (s.a.w) Kulingania Uislamu katika mji wa Makkah
7. Soma Zaidi...

NAMNA YA KUOMBA DUA, SUNNAH ZA DUA NA FADHILA ZA DUA
Soma Zaidi...