Sanda ya mwanaume na namna ya kumkafini

Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

-    Sanda ya mwanamume ina vipande (majavi) vitatu.

 

  1. Weka kipande cha kwanza juu ya mkeka kisha cha pili na cha tatu na vyote kushikizwa kwa uzi katikati, na kila kipande kipakwe marashi na ubani. 

 

  1. Pasua kamba katika pembe mbili za jamvi la kwanza, moja kwa ajili ya kufungia kichwani na nyingine kwa ajili ya kufungia miguuni.

Kamba moja itachanwa kutoka jamvi la pili, ili kumfunika (kufungia) maiti katikati. Na kamba tatu zitachanwa jamvi la tatu na la pili kwa ajili ya kufungia juu ya mkeka.

 

  1. Maiti italazwa juu ya majavi yote matatu. Ichukuliwe pamba iwekwe manukato kisha iwekwe juu ya viungo vyote vya sijda; paji la uso, viganja vya mikono, magotini na vidole vya miguu. Pamba itumike pia kuziba tundu zote mwilini; mdomo, masikio, pua na makalio.

 

  1. Maiti itatizwe (ifunikwe) mwili wote, kwa kuanza kipande cha kwanza, kisha cha pili na cha tatu ukitanguliza kunjo la kushoto kisha la kulia linafuata. Zile kamba zilizochanwa zitatumika kufungia vitanzi maiti kichwani, tumboni na miguuni. Baada ya hapo maiti inaweza kuwekwa kwenye jeneza baada ya kuzungushiwa kwa mkeka tayari kwa kuswaliwa.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 2781

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 web hosting    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina   

Post zinazofanana: