Ni mambo gani yanaharibu na kutengua udhu?
Yanayotengua Udhu
Mtu aliyetawadha hutokwa na udhu wake kwa kupatwa au kutokewa na mojawapo kati ya haya yafuatayo:
1.Kutokwa na kitu chochote kwenye sehemu za siri. Ni pamoja na kwenda haja ndogo au kubwa. Kutokwa na upepo, maji maji yatokayo katika utupu wa mbele kutokana na matamanio au sababu nyinginezo.
2.Kutokwa na fahamu kwa kulala usingizi kwa kuegemea mahali bila ya kumakinisha makalio yake ardhini. Tunajifunza katika hadithi ifu atayo:
Amesimulia Basrah (r.a) kuwa Mtume (s.a.w) kasema:Kutawadha kuna kuwa lazima kwa mwenye kulala usingizi kitandani, kwa sababu anapolala kitandani maungo yake hulegea ”.(Tirmidh, Abuu Daud).
3.Kushika sehemu za siri kwa viganja vya mikono kama tunavyojifunza katika hadithi ifuatayo:
Amesimulia Basrah (r.a) kuwa Mtume (s.a.w) kasema: “Mmoja wenu atakapogusa tupu yake, na aende kutaw adha tena ”.(Malik, Ahm ad, Abuu Daud, Tirmidh, Nasai, Ibn Majah)
Haya matatu ndio yanayotengua udhu bila ya khitilafu yoyote kati ya Waislamu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 web hosting 👉3 ai web app 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Historia ya adhana na Iqama na jinsi ya kuadhini.
Hadithi hii inakwenda kukufundisha historia fupi ya adhana pia utakwenda kujifunza jinsi ya kuadhini na kuqimu.
Soma Zaidi...Nini maana ya kusimamisha swala
Post hii inakwenda kukufundisha maana ya kusimamisha swala kama inavyotumika kisheria.
Soma Zaidi...