picha

Kwanini lengo la zakat na sadaqat halifikiwi katika jamii yetu

Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)

Kwa nini lengo la Zakat na Sadaka halifikiwi katika jamii yetu?


Pamoja na zakat na sadaka kutolewa na baadhi ya waislamu lakini malengo yake hayafikiwi, zifuatazo ni baadhi ya sababu;

1. Wengi watoao zakat na sadakat hawajui lengo lake halisi.
2. Waislamu wengi wanatoa zaka na sadaka kwa lengo la kupata thawabu na kufutiwa madhambi tu na sio utakaso.
3. Waislamu wengi hawatoi zakat kabisa.
4. Waislamu wengi licha ya kuwa na mali na uwezo wa kutoa zakat na sadaka lakini hawatekelezi au kuhimiza wengine katika kutoa mali zao pia. Rejea Quran (2:2-3).
5. Wengi watoao zakat na sadakat hawatekelezi masharti ya utoaji.
6. Pamoja na matajiri wachache kutoa zakat na sadaka, lakini bado hutoa kwa ria, masimbulizi, adha na kuleta uadui na fitna katika jamii. Rejea Quran (2:264).
7. Zakat na sadaka haikusanywi na kugawanywa kijamii.
8. Utoaji na ugawaji wa zakat na sadaka umekuwa unafanywa kila mtu kivyake, bila mpango maalumu wa kukusanya na kugawa kwa wanaostahiki.
9. Wengi watoao zakat na sadakat chumo lao ni la haramu.
10. Ingawa waislamu wengi hutoa zakat na sadaka, lakini lengo na matunda yake hayafikiwi kutokana na chumo lao kuwa haramu.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2022/01/18/Tuesday - 04:42:41 pm Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 3230

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 Dua za Mitume na Manabii    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina   

Post zinazofanana: