image

Njia haramu za uchumi.

Njia hizi ni haramu katika kukuza uchumi wako.

Njia za uchumi zilizoharamishwa

Vipengele vya biashara haramu vilivyoorodheshwa nyuma ni miongoni mwa hizo. Njia nyingine za uchumi zilizoharamishwa ni hizi zifuatazo:

 

(i)Wizi
Wizi wa aina yoyote ni kitendo cha dhulma ni haramu katika Uislamu.

 


(ii)Ulevi
Ulevi wa aina yoyote kwa kiwango chochote ni haramu. Uharamu wa ulevi hauishii kwa mnywaji tu; bali pia ni haramu kushiriki katika hatua yoyote ile ya utengenezaji, uuzaji na uandazi.

 


Anas ameeleza kuwa Mtume (s.a.w.) amewalaani (watu) kumi kuhusiana na pombe-yule anayeikamua, yule aliyehusishwa katika kuikamua, yule anayeinywa, yule anayeibeba, yule anayepelekewa, yule anayeiandaa, yule anayeiuza, yule anayepanga bei yake, yule anayeinunua na yule anayemnunulia. (Tirmidh, Ibn Majah).
Kutokana na Hadithi hii, inatuwia wazi kuwa aina yoyote ile ya utengenezaji, uuzaji na unywaji imeharamishwa. Pato lolote mtu atakalolipata kama malipo ya kushiriki katika hatua yoyote ya matayarisho na unywaji wa ulevi, litakuwa ni pato la haramu. Hebu tuangalie hali halisi. Je, hatuwaoni Waislamu wakishiriki kwa ukamilifu katika viwanda vya pombe kama mameneja, makarani, wakemia, madereva, n.k.? Je, hawa wataridhika kuendelea kujiita Waislamu na ili hali kila saa wako katika laana ya Allah na Mtume wake na ibada zao zote hazikubaliwi maadam miili yao imerutubishwa na kipato cha haramu; kivazi chao ni haramu na kila walicho nacho katika mazingira yao kimepatikana kwa pato la haramu?

 


(iii) Kamari
Kamari imeharamishwa pamoja na pombe kama ilivyo katika aya ya (5:90) na (2:2 19). Pia Hadithi ifuatayo inatubainishia kuharamishwa kwa kamari:
Abdullah bin Amr ameeleza kuwa Mtume wa Allah ameharamisha ulevi, michezo ya bahati nasibu, kamari ya karata, na gobairah (aina ya pombe) na anasema: “Kila ulevi ni haram”. (Abu Daud).

 


Hadithi hii inatubainishia kuwa aina zote za kamari-gudugudu, pata-potea, karata, bahati nasibu, nakadhalika, ni haramu na kwa hiyo pato lolote litakalo tokana na kamari ni pato haramu. Ni muhimu kufahamu kuwa uharamu wa kamari hauishii kwa watu wawili au kikundi cha watu wachache bali hata kama kamari hiyo itachezwa kitaifa, itabakia kuwa haramu tu.

 


Kwa hiyo bahati nasibu ya taifa, Bima ya Kimataifa, na michezo yote ya kamari iliyotolewa kibali na taifa, yote ni haramu mbele ya Allah na yeyote atakayeshiriki kwa namna yoyote katika michezo hiyo ya kamari atakuwa ameshiriki katika haramu na kipato chochote atakachokipata kutokana na ushiriki wake huo kitakuwa ni kipato cha haramu. Katika aya tulizozirejea hapo juu (5:90 -91) kamari imeharamishwa kwa sababu kuu tatu:

 

Kwanza, ni uchafu, kamari imeitwa “rijsi”. Kamari imeitwa uchafu kwa sababu pesa anazozipata mtu kwa kamari ni za dhulma na haramu. Kufumba na kufumbua mtu amepata maelfu ya pesa bila jasho lolote. Hivyo ni dhulma na ni haramu.

 


Pili, kamari inajenga chuki na uadui. Hii ni kwa sababu yule aliyeliwa pesa zake kwa maelfu kwa njia hii ya dhulma huwa ana mfundo mkubwa moyoni na anamchukia sana yule aliyechukua pesa zake hata kama ajidai kuwa hajali, ukweli ni kuwa pesa zake zitamuuma sana. Na mara kadhaa wacheza kamari wameishia kupigana na hata kuuana.

 


(iv)Kipato chochote kinachotokana na utengenezaji wa sanamu na picha za watu na wanyama ni kipato haramu.Rejea katika Hadithi zilizotolewa chini ya “Biashara haramu”.

 


(v)Kipato chochote kutokana na umalaya, ngoma na muziki wa aina yoyote ni kipato haramu. Kama inavyobainika katika Hadithi ifu atayo:
Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Allah ameharam isha kipato kutokana na mauzo ya mbwa, na kipato kutokana na kuimba kwa wasichana (sing-ing girls) (Sharhi Sunnat).

 


(vi)Kipato chochote kutokana na utabiri, ramli, na upigaji bao ni kipato haramu, na yote hayo ni kazi ya shetani katika Qur’an Allah (s.w.) ametuasa:

 

Enyi mlioamini! Bila shaka ulevi na kamari na kuabudiwa (kuombwa) asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli (na kwa vinginevyo); (yote haya) ni uchafu (na ni) katika kazi ya shetani. Basi jiepusheni navyo ili mpate kufaulu” (5:90)

 


Kutokana na aya hii upigaji ramli na utazamiaji wa aina yoyote ni haramu na kipato chake kitakachopatikana na kazi hiyo ni haramu pia. Utabiri wa aina yoyote ni haramu, hali kadhalika kipato kinachotokana na kazi hiyo ya utabiri ni haramu. Abu Bakar aliwahi kujitapisha baada ya kugundua kuwa amelishwa kutokana na malipo ya utabiri. Pia kipato kutokana na uchawi ni kipato haramu.

 


(vii) Hongo (Rushwa)
Utoaji na upokeaji wa rushwa ni haramu na pato lolote lililotokana na rushwa ni pato haramu. Mtoaji na mpokeaji wa rushwa wote wamelaaniwa na Allah na Mtume wake kama tunavyofahamishwa katika Hadithi ifu atayo:

 


Abdullah bin Amr ameeleza kuwa Mtume wa Allah amemlaani mpokeaji rushw a na mtoaji rushw a katika kutoa hukumu. (Abu Daud, Ibn Majah).
Hongo au rushwa ni kiasi chochote anachopokea muhudumu (mfanyakazi) zaidi kuliko malipo yake ya haki katika kutoa huduma alizoajiriwa kwazo. Kwa maana nyingine, mtu akipokea malipo yoyote, hata yawe madogo kiasi gani ambayo ni ziada ya mshahara wake katika kufanya kazi ile ile na katika kiwango kile kile cha kazi aliyoajiriwa kwayo, atakuwa amepokea rushwa. Turejee kwa makini Hadithi ifuatayo:

 


Abu Humaid as-Sayyid ameeleza Mtume (s.a.w.) alimteua mtu katika kabila la Azd aliyekuwa akiitwa Ibnul Luthiyyah kama, mkusanyaji wa zakat, Aliporudi Madina, alisema: “Hii ni kw a ajili yenu na hivi ni vyangu (nilivyopokea) kama zawadi Kisha Mtume (s.a.w.) alitoa hutuba baada ya kumhimidi na kumtukuza Allah akasema: Jambo lingine ni kwamba nimewateua baadhi ya watu miongoni mwenu kufanya (kuongoza) shughuli ambazo Allah amenipa mamlaka kwazo. Mmoja wao anakuja na kusema: ‘Hii ni kwa ajili yenu na hii ni zawadi niliyopewa. Kwa nini basi asibakie katika nyumba ya baba yake au katika nyumba ya mama yake na kuona kuwa angalipewa zawadi au hangelipewa? Kwa yule ambaye mikononi mwake uko uhai wangu hapana yoyote atakayechukua kitu chochote kutokana na zakati awe siku ya Kiyama hakutokea huku amebeba kitu hicho mabegani mwake. Kama alichukua punda atakuw a analia humo begani; kama alichukua mbuzi atakuwa analia (mee mee) humo begani. Kisha Mtume (s.a.w.) aliinua mikono yake mpaka tukaona weupe wa makwapani na akasema: “Ee Allah! Nimefikisha ujumbe)? Ee Allah! Nimefikisha ujumbe)?” (Bukhari na Muslim).

 


Hadithi hii inatuonesha kuwa mkusanyaji hakuwa na haki ya kuchukua zawadi katika kukusanya mali ambayo ndiyo kazi aliyoteuliwa kwayo. Swali aliloulizwa ni: Je, angalikuwa nyumbani au asingalitoka kukusanya zakat, angaliletewa zawadi hizo? Jibu ni kwamba asingeletewa zawadi hizo nyumbani kwake. Kwa hiyo zawadi zinazopatikana kwa namna hiyo si zawadi bali ni rushwa au hongo. Hadithi hii inatupa fundisho kubwa juu ya upokeaji zawadi makazini. Mara nyingi watu hupokea rushwa kwa jina la “zawadi”. Hadithi hii imetuwekea mpaka unaotenganisha rushwa na zawadi. Kitu cha ziada ya malipo ya kazi au ziada ya mshahara kitabainika kuwa zawadi au hongo (rushwa) kutokana na jibu la swali lifuatalo: Je, kama afisa (mfanyakazi) asingelikuwa katika nafasi ya kazi aliyonayo au katika cheo alicho nacho,

 

angalipata zawadi hiyo au asingelipata? Kama jibu ni “asingalipata” basi afisa huyo au mfanyakazi huyo akipokea zawadi ajuwe amepokea hongo. Kama afisa au mfanyakazi huyo amepewa zawadi isiyohusiana na nafasi yake ya kazi; na angaliweza kupata zawadi hiyo hata kama angalikuwa hana kazi au angalikuwa mahali pengine, basi zawadi hiyo itakuwa ni zawadi kweli na itakuwa halali kwake.

 


Madhara ya rushwa yako wazi. Kwanza, mwenye kupokea rushwa (hongo) anapokea chumo la haramu ambalo litamfanya asikubaliwe ibada zake zote. Pili, Mla rushwa hawezi kumsaidia mtu asiyejiweza. Kila mara watawahudumia wale wenye kitu cha kutoa hongo kwa namna nyingine mnyonge asiye na uwezo wa kutoa chochote hatapata huduma muhimu za maisha anazostahiki kupata. Tatu, mla rushwa hawezi kuheshimiwa au kuaminiwa katika jamii kwa shughuli yoyote ile.

            

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/08/26/Friday - 08:30:39 pm Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1200


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Mifano na namna ya kurithisha
Ugawaji wa mirathi-Mume ana nusu (1/2) = 1/2 -Mama ana sudusi. Soma Zaidi...

Haki za binadamu kwa ujumla (basic human rights)
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Nguzo za uislamu:Shahada
Nguzo za uislamu: Shahada (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Sifa za imamu wa swala ya jamaa
Post hii inakwenda kukupa sifa za imamu wa msikitini anayepasa kuswalisha swala ya jamii. Soma Zaidi...

Lengo la kufunga ramadhani, na faida zake, nguzo za kufunga na sharti zake
Saumu (Funga). Soma Zaidi...

Siku ambazo haziruhusiwi kufunga
Ni haramu kufunga katika masiku haya. Na endapo utafunga basi funga haitakuwa na malipo. Soma Zaidi...

Taratibu za kutaliki katika uislamu.
Hapa utajifunza taratibu zinazofuatwa wakati wa kukusudia kumuacha mke. Pia utajifunza sababu za kiwepo kwa eda baada ya kuachwa mwanamke. Soma Zaidi...

Aina za swala..
Nguzo za uislamu,aina za swala (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Sifa za Kuwa Mpole na Mnyenyekevu
22. Soma Zaidi...

DARSA ZA SWALA NA NMNA YA KUSWALI SWALA ZA SUNA NA FARAHDI, SHARTI NA NGUZO NA SUNA ZA SWALA
Soma Zaidi...

Historia na asili ya kuzibiti uzazi na uzazi wa mpango
Soma Zaidi...

Historia ya adhana na nama ya kuadhini
Soma Zaidi...