Siku ya idi al-fitir na namna ya kusherekea idi

Siku ya idi al-fitir na namna ya kusherekea idi

Yaliyo Sunnah kuyafanya Siku ya Idd



Ni sunnah siku ya Idd kukoga, kuvalia nguo nzuri kuliko zote ulizo nazo na kupaka uturi (manukato) kwa wanaume. Pia ni sunnah siku ya Idd kupika vyakula na kuandaa vinywaji vizuri zaidi kuliko siku za kawaida. kwa wafugaji na wale wenye wasaa, ni sunah kumchinja mnyama aliye bora zaidi kuliko wengine katika mifugo yake kama tunavyojifunza katika hadith ifuatayo:



Amehadithia Hasan Asibbit (r.a) kuwa Mtume (s.a.w) ametuamrisha katika Idd m bili kuvaa vizuri zaidi kadri tuw ezavyo, tupake uturi bora zaidi kuliko wote tulionao, na tuchinje wanyama wenye thamani zaidi kuliko wote tu lion a o. (A l-Ha kim).



Ni sunnah vile vile kuwakaribisha ndugu, marafiki, majirani, maskini, yatima na wengine wasiojiweza. Ni sunnah kuwatembelea ndugu, marafiki, majirani na wagonjwa. Ni sunnah vile vile kupeana zawadi.



Tahadhari Katika Siku ya Idd
Waislamu hawana budi kukumbuka kuwa sherehe za Kiislamu, makusudio yake na muundo wake, ni tofauti kabisa na sherehe zisizokuwa za Kiislamu. Sherehe za Kiislamu ni kilele cha kuonyesha shukrani zetu kwa Allah (s.w) kwa kutujaalia na kutuwezesha kutimiza wajibu wetu kwake katika kutekeleza ibada kubwa na nzito kama vile kufunga Ramadhani na kukamilisha Ibada ya Hija. Hivyo, sherehe hizi ni lazima ziambatane na kumshukuru, kumtukuza, kumtaja na kumkumbuka sana Allah (s.w).



Tunafahamu kuwa katika sherehe zisizokuwa za Kiislamu au zisizosherehekewa kwa mtazamo wa Kiislamu, ndio wakati ambao Allah (s.w) husahauliwa kuliko nyakati zote na ndio wakati ambao shetani hukumbukwa na kuadhimishwa kuliko nyakati zote. Kwa maana nyingine katika sherehe hizi watu hujiingiza kwa furaha na kicheko katika kumuasi Allah (s.w). Kutokana na uzoefu wetu sherehe hizi zimeambatana na ulevi, ngoma na mziki, mchanganyiko wa wanaume na wanawake, uzinifu na mengineyo kama haya.



Waislamu wanatahadharishwa sana wajiepushe na sherehe za namna hii, kwani zitawafanya wawe ni wenye kukufuru badala ya kuwa wenye kumshukuru Allah (s.w), kwa mafanikio hayo wanayo yasherehekea. Katika sherehe hizi za Idd Muislamu anatakiwa achukue hadhari kubwa katika kuchunga mipaka ya sherehe, kwani kumuasi Allah (s.w) katika siku ya Idd ni kosa kubwa sana mbele ya Allah kuliko kumuasi Allah (s.w) wakati mwingine, Mtume (s.a.w) amesema:
“Kumuasi Mwenyezi Mungu siku ya Idd ni sawa na kumuasi Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama ”.




                   


Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1234

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

NI ZIPI NGUZO NA SHARTI KUU ZA SWALA ILI IKUBALIWE

Sharti za SwalaSharti za Swala Sharti za swala ni yale mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu ayachunge na kuyatekeleza kabla hajaanza kuswali.

Soma Zaidi...
Warithi wasio na mafungu maalumu katika uislamu

Hapa utajifunza watu wanaorithi bila ya kuwekewa mafungu maalumu au viwango maalumi vya kurithi.

Soma Zaidi...
Milki ya raslimali katika uislamu

Milki ya RasilimaliIli kujipatia maendeleo ya kiuchumi katika zama zote mwanaadamu anahitaji rasilimali za kumwezesha kufikia azma hiyo.

Soma Zaidi...
Jinsi ya kujitwaharisha kutokana na najisi

Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kujitwaharisha kutokana na najisi.

Soma Zaidi...
Funga ya ramadhan na nyinginezo

Nguzo za uislamu (EDK form 2; dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...