Hapa utajifunza maana ya ndoa kulingana na uislamu na umuhimu wake katika jamiii
Maana ya Ndoa
Ndoa, kwa ujumla, ni mkataba wa kuishi pamoja kati ya mume na mke kwa kufuata utaratibu uliowekwa na jamii. Kwa mfano, hapa Tanzania mume na mke watatambulika kuwa wameoana kisheria, pale watakapokuwa wamefunga mkataba wa kuishi pamoja mbele ya Mkuu wa wilaya au mbele ya walii na mashahidi wawili (ndoa ya kiislamu)au mbele ya Padri (Kanisani).
Ndoa ya Kiislamu ni mkataba wa hiari kati ya mume na mke wa kuishi pamoja kwa kuzingatia masharti na taratibu zilizowekwa na sheria ya Kiislamu. Ndoa yoyote iliyofungwa kinyume na masharti na taratibu za Kiislamu, haikubaliki kwa Waislamu.
Umuhimu wa Ndoa kwa Mtazamo wa Uislamu
Katika Uislamu ndoa ni jambo lililokokotezwa sana kama tunavyojifunza katika Hadithi zifuatazo:
Katika Hadithi iliyopokelewa na Imamu Bukhari Mtume (s.a.w) amesisitiza kuwa ndoa ni katika sunnah yake na akaongeza kusema: "Yeyote anayekataa sunna yangu sipamoja nami ".
Anas (r.a) amesema kuwa Mtume wa Allah amesema, 'Mtu anapooa huwa amekamilisha nusu ya dini, kisha amche Allah ili akamilishe nusu iliyobakia." (Bukhari).
Ndoa inasisitizwa kutokana na umuhimu wake katika kuijenga na kuiendeleza jamii kwa:
(i)Kuihifadhi jamii na zinaa.
(ii)Kuendeleza kizazi kwa utaratibu mzuri.
(iii)Kujenga mapenzi na huruma katika familia.
(iv)Kukuza uhusiano na Udugu katika jamii.
(v)Kukilea kizazi katika maadili mema.
(vi)Kuwafanya watu wawajibike ipasavyo.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Suala la omba-ombaTukiliangalia suala la omba-omba kwa upana kidogo, ambalo hivi sasa linaongelewa katika vikao mbalimbali vya kitaifa na kimataifa, tutaona kuwa ni Uislamu pekee unaotoa namna bora ya kulishughulikia suala hili.
Soma Zaidi...Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3:Dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Sharti za SwalaSharti za Swala Sharti za swala ni yale mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu ayachunge na kuyatekeleza kabla hajaanza kuswali.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza utaratibu wa kusherekea ifil fitir. Pia utajifunza sunnah zinazoambatsns na idil fitir
Soma Zaidi...Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...