Swala ya Idi al-fitir na namna ya kuiendea

Swala ya Idi al-fitir na namna ya kuiendea

Iddil -FitriIddil-Fitri ni siku kuu ya Kiislamu ya kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Ramadhani. Mwezi wa Ramadhani ambao ndani yake imefaradhishwa funga ambayo imeambatanishwa na matendo mbali mbali ya sunnah, umekusudiwa uwe mwezi wa mafunzo na mazoezi ya kumfanya mja awe mchaji Mungu katika kiwango kinachostahiki kwa kipindi chote cha mwaka mzima.


Iddil-Fitri ndicho kilele cha mafunzo haya ambapo Waislamu wanafurahia na kumshukuru Allah (s.w) kwa kumaliza salama mafunzo haya muhimu na wakati huo huo humuomba Allah (s.w) ayafanye mafunzo hayo yawe yenye kuwafikisha kwenye lengo lililokusudiwa. Hivyo, moja kwa moja inadhihiri kuwa Iddil-Fitri haisherehekewi kwa mavazi mazuri na kwa vyakula na vinywaji vizuri tu, bali kilele cha sherehe hii kinafikiwa kwa kuswali swala ya Iddil-Fitri na kumtukuza na kumuhimidi Allah (s.w) sana kwa Takbira.Swala ya Iddil-FitriSwala ya Idd mbili - Iddil-Fitri na Iddil-Hajj (kilele cha ibada ya Hija) ni sunnah zilizokokotezwa. Swala ya Idd inaswaliwa kwa rakaa mbili na kufuatiwa na Khutuba mbili kama zile zinazosomwa kabla ya swala ya Ijumaa. Swala ya idd ina Takbira 12,takbira 7 hutolewa katika rakaa ya kwanza kabla ya kusoma suratul-Faatiha na takbira 5 huletwa katika rakaa ya pili. vile vile kabla ya kusoma suratul-Faatiha.Mahali pa kuswalia Idd ni bora pawe uwanjani ili Waislamu wakusanyike pamoja kutoka sehemu mbali mbali za mji. Mtume (s.a.w) alikuwa akifanya hivyo. Ni sunnah kula chochote kabla ya kuswali Iddil-Fitri kama tunavyofahamishwa katika Hadith zifu atazo:Anas (r.a) ameeleza kuw a Mtume w a Allah hakw enda kusw ali Iddil- Fitri mpaka alipokula Tende katika idadi ya witri. (Bukhari).
Buraydah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah alikuwa hatoki kwa swala ya Iddil-Fitri mpaka awe amekula (Kitu) na hakuwa anakula katika s iku ya kuchinja (Iddil-Haj) mpaka asw ali (Dirim i).Ni sunnah kuleta takbira mara kwa mara kuanzia pale mwezi wa Shawwal unapoandama mpaka baada ya swala ya Iddil-fitri. Takbira


Tafsiri ya Takbira:
Allah Mkubwa, Allah Mkubwa, Allah Mkubwa hapana mola ila Allah Allah Mkubwa, Allah Mkubwa na shukurani zote ni za Allah. Allah Mkubwa aliyetukuka, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi, na namtakasa asubuhi na jioni. Hapana Mola ila Allah. Wala hatumuabudu yeyote ila Yeye peke yake, tunamtakasa yeye na dini yake hata kama w atachukia makafiri.Hapana mola ila Allah peke yake. Ameisadikisha (ameitimiza) ahadi yake na akamnusuru mja (Mtume s.a.w) wake, na akalitukuza jeshi lake, akalipa ushindi kundi lake. Hapana mola ila Allah. Allah Mkubwa. Ewe Allah, teremsha rehma zako juu ya Muhammad, na Maswahaba wake Muhammad, na waliomnusuru Muhammad, na Wakeze Muhammad, na kizazi chake Muhammad, na uwape salama na amani kwa wingi.
                   
Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 883


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Kazi na wajibu wa khalifa katika dola ya kiislamu
Kazi na Wajibu wa KhalifaKhalifa katika Serikali ya Kiislamu ndiye mtendaji mkuu wa Serikali kama alivyokuwa Mtume(s. Soma Zaidi...

SHARTI ZA KUWAJIBIKA KWA ZAKA
Soma Zaidi...

Hadhi na Haki za Mwanamke Ulaya chini ya kanisa hapo zamani
Soma Zaidi...

.Mazingatio muhimu katika uchumi wa Kiislamu
3. Soma Zaidi...

Uchaguzi wa Abubakari kuwa Khalifa wa kwanza baada ya kufariki Mtume Muhammad (s.a.w)
Soma Zaidi...

Nini maana ya asaba katika mirathi ya kiislamu
Soma Zaidi...

Kuanzishwa kwa vitenge vya ulinza na Usalama, na usalama wa taifa
Soma Zaidi...

NI ZIPI NGUZO NA SHARTI KUU ZA SWALA ILI IKUBALIWE
Sharti za SwalaSharti za Swala Sharti za swala ni yale mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu ayachunge na kuyatekeleza kabla hajaanza kuswali. Soma Zaidi...

DUA 21 - 31
21. Soma Zaidi...

Yusufu(a.s) Atupwa afungwa Gerezani
Mkewe Al-Aziz hakumkatia tamaa Yusufu(a. Soma Zaidi...

Hadithi Ya 41: Hatoamini Mmoja Wenu Mpaka Mapenzi Yake Yatakapomili (yatakapoendana) Na Yale Niliyokuja Nayo
Soma Zaidi...

Dalili za uti kwa wanaume na wanawake
tambuwa chanzo na dalili za UTI na tiba yake, pamoja na njia za kupambana na UTI Soma Zaidi...