image

Funga za kafara, aina zake na sababu za funga hizi za kafara na hukumu zake

Funga za kafara, aina zake na sababu za funga hizi za kafara na hukumu zake

Funga za Kafara



Funga za kafara ni funga anazolazimika Muislamu kuzileta ili ziwe kitubio baada ya kutenda kosa fulani. Yaani funga hizi zimewekwa na sheria ya Kiislamu kama fidia au faini baada ya kutenda kosa na kutaka kutubia kwa Allah (s.w). Zifuatazo ni funga za kafara kama zilivyobanishwa katika Qur-an na Hadith:



(i) Kufunga miezi miwili mfululizo kwa Muislamu aliyemuua mtu kwa bahati mbaya na akakosa mali ya kulipia fidiya kama inavyobainishwa katika Qur-an:


Na haiwi kwa Mu is lamu kumuua Muislamu (mwenziwe kusudi) ila kwa kukosea.Na mwenye kumuua Muislamu kwa kukosea basi ampe uungwana mtumwa aliye Muislamu, na pia atoe fidiya (Malipo) kuwapa warithi wake. Isipokuwa waache weny ewe kwa kufanya kuwa ni sadaqat (yao). Na aliyeuawa akiwa ni jamaa wa maadui zenu, hali yeye ni Mu is lam, basi ampe uungwana mtumwa aliye Muislamu (basi, hapana wa kupewa fidiya). Na kama (aliyeuawa) ni moja wa watu ambao kuna ahadi baina yenu na baina yao; basi warithi wake wapewe malipo na pia apewe uungwana mtumwa aliye Muislamu. Na asiyepata basi afunge miezi miwili mfululizo. Ndio kitubio kitokacho kwa Mwenyezi Mungu.Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mw eny e Hekim a. (4:92).



(ii) Kufunga miezi miwili mfululizo kwa mtu atakayemsusa mkewe kwa kumfananisha na mama yake kwa kutamka: “Wewe kwangu mimi nakuona kama mgongo wa mama yangu.” Maneno haya yalitamkwa na Sahaba wa Mtume (s.a.w) - Aus Ibn Samit (r.a), walipogombana na mkewe. Maneno haya kwa jamii ya Waarabu wakati ule wa Mtume (s.a.w) yalikuwa mabaya sana na yalikuwa ni ya kumdhalilisha mwanamke. Hivyo baada ya kufanyika kitendo hiki, mkewe huyu Sahaba alikwenda kwa Mtume (s.a.w) kushitakia; lakini Mtume (s.a.w) hakuweza kumpatia ufumbuzi wa tatizo lake. Mama huyu alizidi kusononeka sana huku akitarajia nusra ya Allah (s.w).Ni katika hali hii ya kusononeka huyu mama Allah (s.w) alishusha kwa Mtume wake aya zifuatazo:



Mwenyezi Mungu amekwisha sikia usemi wa mwanamke yule anayejadiliana nawe sababu ya mumewe, na anashtaki mbele ya



Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu; anayasikia majibizano yenu; hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia mwenye kuona. Wale miongoni mwenu wawaitao wake zao mama zao, (kwa hivyo wakajiepusha nao wasiwaingilie wala wasiw ape ruhusa kuolewa na mwanaume wengine), hao si mama zao. Hawakuwa mama zao ila wale waliowazaa.Wanasema neno baya na la uwongo.Na Mwenyezi Mungu ni mwenye msamaha, mwenye maghfira.(58:1-2).



Baada ya kosa la huyu Sahaba kubainishwa katika aya hizi, aya zifuatazo zinatoa kitubio au adhabu ya kosa hili:


Na wale wawaitao wake zao mama zao kisha wakarudia katika yale w aliyoyasema (wakataka kuw arejea wake zao w aendelee kuishi kama kawaida), basi wampe mtumwa huru kabla ya kugusana.Mnapewa maonyo kwa haya. Na Mwenyezi Mungu anajua (yote) mnayoyatenda. Na asiye pata (mtumwa) basi afunge saumu ya miezi miwili mfululizo kabla ya kugusana; na asiyeweza basi awalishe maskini sitini.


(Mmeambiw a haya ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu,na kwa makafiri iko adhabu iumizayo. (58:3-4).



(iii) Kufunga siku tatu mfululizo kama kafara ya kuvunja kiapo kama tunavyoamrishwa katika aya ifuatayo:


“Mwenyezi Mungu hatakuteseni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini atakukamateni kwa viapo mlivyo viapa kwa nia mlioifunga bara bara. Basi kafara yake ni kuw alisha maskini kumi kwa chakula cha katikati mnacho walisha watu wa majumbani mwenu, au kuwavisha, au kumpa uungwana mtumwa. Lakini asiyeweza kupata hayo, basi afunge siku tatu. Hii ndiyo kafara ya viapo vyenu mnapoapa. Na vilindeni viapo vyenu (msiape kisha msitimize). Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainisheni aya zake ili mpate kushukuru ” (5:89).



(iv) Kufunga miezi miwili mfululizo kama kitubio cha kufanya tendo la ndoa kati ya mume na mkewe makusudi katika mchana wa mwezi wa Ramadhani.



(v)Mtu aliyehirimia Hijja au Umra haruhusiwi kuwinda na endapo atavunja amri hii ya kutowinda kitubio au kafara yake ni kufunga kama inavyobainishwa katika aya ifuatayo



“Enyi mliomini! Msiue mawindo na hali (ya kuwa) mumo katika Hija au Umra. Na miongoni mwenu atakayemuua kwa kusudi, basi malipo yake yatakuwa kwa (kuchinja) kilicho sawa na alichokiua,katika wanyama wanaofugwa,kama watakavyohukumu waadilifu wawili miongoni mwenu mnyama huyo apelekwe iliko Ka’aba, au badala ya hayo ni kufunga, ili aonje ubaya wa jambo lake hili ... (5:95). Muda wa kufunga utategemeana na thamani ya mnyama ambaye angalimchinja katika hesabu ya vibaba vya chakula.



(vi) Kama mwenye kuhiji au kufanya Umra atavunja miiko ya Ihram au iwapo atashindwa kutekeleza baadhi ya matendo ya Hijja, atalazimika kufunga kama inavyobainishwa katika aya ifuatayo:


Na timizeni Hija na Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na kama mkizuiwa, basi (chinjeni) wanyama walio wepesi kupatikana (nao ni mbuzi). Wala msinyoe vichwa vyenu mpaka wanyama hao wafike machinjioni mwao. Na atakayekuwa mgonjwa katika nyinyi au ana vya kumuudhi kichwani mwake (akafanya yaliyokatazwa kama vile kunyoa), basi atoe fidia kwa kufunga au kutoa sadaqat au kuchinja wanyama (2:196).




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1265


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Jinsi ya kutwaharisha aina mbalimbali za najisi
Kila najisi ina namna yake ya kutwaharisha, hata hivyo namna hizo hufanana. Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutwaharisha najisi mbalimbali. Soma Zaidi...

Aina za Najisi na twahara katika uislamu
Post hii inakwenda kukufundisha aina za najis. Pia utajifunza aina za twahara katika uislamu Soma Zaidi...

Kumuandaa maiti punde baada ya kufariki dunia
Soma Zaidi...

Mambo yaliyo haramu kwa mwenye hedhi na nifasi
Katika post hii utakwenda kujifunza mambo ambayo ni haramu kwa mwanamke aliye na hedhi na nifasi Soma Zaidi...

SWALA
1. Soma Zaidi...

Hoja juu ya hitajio la kuzibiti uzazi na uzazi wa mpango
Soma Zaidi...

Maneno mazuri mbele ya mwenyezi Mungu
kuna adhkari nyingi sana ambazo Mtume wa Allah ametutaka tuwe tunadumu nazo. lajkini kuna adhkari ambayo imekusanya maneno matukufu na yanayopendwa sana na Allah. Soma Zaidi...

Swala ya maiti, namna ya kuiswali, nguzo zake, sharti zake na suna zake, hatua kwa hatua
Soma Zaidi...

Yaliyo haramu kwa mtu asiyekuwa na udhu
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu mambo ambauo ni haramu kwa mtu asiye na udhu. Soma Zaidi...

NAMNA YA KUSWALI SWALA YA IJUMAA, JENEZA, SWALA YA JAMAA NA SWALA YA SUNNHA (tarawehe, tahajudi na qiyamu layl)
1. Soma Zaidi...

Jinsi ya kutekeleza funga za sunnah
Hapa utajifunza muda wa kutia jia katika funga za sunnah. Pia utajifunza kuhusu uhuru ulio nao Soma Zaidi...

Misingi na Maadili Katika Uislamu
5. Soma Zaidi...