Chakujitwah aris hia
Nafsi ya mtu hutwaharika kwa mtu huyo kumuamini Allah (s.w) ipasavyo na kufuata mwongozo wake katika kukiendea kila kipengele cha maisha yake ya kibinafsi na kijamii.
Muislamu atatwaharika kutokana na Najisi na Hadath kwa kutumia maji safi au udongo safi kwa kufuata masharti na maelekezo ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
Sifa za Maji Safi
Maji safi kwa mtazamo wa twahara ni yale yanayofaa kujitwaharishia yaliyogawanyika katika makundi yafuatayo:
(a)Maji Mutlak (maji asili)
Maji yoyote katika hali yake ya asili ni maji safi yanayofaa kujitwaharishia. Maji asili (natural water) ni maji ya mvua, chem chem, visima, mito, maziwa na maji ya bahari.
(b)Maji mengi:
Maji mengi ni maji yaliyokusanywa au yaliyokusanyika pamoja na kuwa na ujazo wa mabirika (qullatain) au ujazo usiopungua madebe 12. Mfano wa maji mengi yaliyokusanywa ni maji ya mapipa yenye ujazo wa lita 240, maji ya mabirika (matangi) maalum yaliyojengwa kuhifadhia maji msikitini na nyumbani. Mfano wa maji mengi yaliyojikusanya ni yale ya madimbwi makubwa yanayojikusanya wakati wa mvua.
Maji mengi hayahabiriki upesi. Hayaharibiki kwa kujitwaharishia ndani ya chombo kilichoyakusanya au ndani ya mkusanyiko huo wa maji. Pia maji mengi hayaharibiki kwa kuingiwa na najisi. Bali maji mengi yatakuwa hayafai kujitwaharishia iwapo yatabadilika asili yake katika rangi au utamu (ladha) au harufu.
(c)Maji machache:
Maji machache ni yale yaliyokusanywa katika chombo au yaliyojikusanya katika ardhi yakiwa na ujazo chini ya Qullatain* au chini ya ujazo wa pipa lenye ujazo wa madebe 12 au chini ya ujazo wa lita 224. Mfano wa maji machache ni ya ndoo, maji ya mtungi na maji yaliyojikusanya kwenye vidimbwi vidogo vidogo wakati wa mvua.
Maji machache hayatafaa kujitwaharishia iwapo
(i)yataingiwa na najisi japo kidogo sana.
(ii)Iwapo yatakuwa yametumika katika kujitwaharishia humo humo kwa kuondoa najisi au Hadath.
(iii)Iwapo yatakuwa yametumika kwa kufulia au kuoshea vyombo au kuogea humo humo.
(iv)Iwapo yataingiwa na kitu kikayabadilisha asili yake katika rangi, harufu au tamu(ladha).
Kutokana na haya tunajifunza kuwa, tunapokuwa na maji machache hatuna budi kuwa waangalifu wakati wa kuyatumia ili tusiyaharibu. Tusijitwaharishe ndani ya vyombo vilivyohifadhia maji hayo, bali tuyateke na kujitwaharisha mbali nayo. Kwa mfano tunakoga kwa kutumia kata na tunatawadha kwa kutumia kopo au birika.
(d)Maji makombo
Maji makombo ni maji yaliyonywewa na binaadamu au mnyama yakabakishwa.Maji makombo yanafaa kujitwaharishia ila yale yaliyonywewa na kubakishwa na mbwa au nguruwe.
Udongo safi
Udongo safi ni ule ulioepukana na najisi na ukabakia katika asili yake na kutochanganyika na kitu kama vile unga, majivu au vumbi la mkaa, vumbi la mbao (saw dust) n.k. kwa kawaida udongo wote katika ardhi ni safi.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1244
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉2 Madrasa kiganjani
👉3 Kitau cha Fiqh
👉4 Kitabu cha Afya
👉5 Simulizi za Hadithi Audio
👉6 kitabu cha Simulizi
Namna ya kulipa swaumu ya ramadhani na ni nani anatakiwa alipe
Soma Zaidi...
Jinsi ya kujitwaharisha kutokana na najisi
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kujitwaharisha kutokana na najisi. Soma Zaidi...
Aina za talaka zinazo rejewa
Soma Zaidi...
Mambo yasiyoharibu Swaumu na Kufunguza mwenye kufunga
Soma Zaidi...
NINI MAANA YA KUSIMAMISHA SWALA, KATIKA UISLAMU (NI YUPI TARQU SWALA) yaani mwenye kuacha swala)
Kusimamisha Swala. Soma Zaidi...
Riba na Madhara Yake Katika Jamii
- Riba ni kipato chochote kile cha ziada kutokana na mkopo au mtaji bila kushiriki katika faida au hasara. Soma Zaidi...
Yaliyo haramu kwa mwenye hadathi kubwa.
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu mambo ya haramu kwa mwenye hadathi kubwa Soma Zaidi...
kanunu na sheria za biashara katika islamu
Soma Zaidi...
Haki, wajibu na majukumu katika familia ya kiislamu na majirani zake
Soma Zaidi...
Aina ya talaka zisizo rejewa
2. Soma Zaidi...
haki na hadhi za mwanamke katika jamii inayoishi kiislamu
Soma Zaidi...