image

Hadhi na Haki za mwanamke katika jamii za Kirumi hapo zamani

(b) WarumiJamii ya Warumi nayo ni miongoni mwa jamii zinazohesabika kuwa zilianza kustaarabika mapema katika historia ya ulimwengu.

Hadhi na Haki za mwanamke katika jamii za Kirumi hapo zamani

(b) Warumi
Jamii ya Warumi nayo ni miongoni mwa jamii zinazohesabika kuwa zilianza kustaarabika mapema katika historia ya ulimwengu. Je jamii hii ilimpa mwanamke heshima na hadhi anayostahiki? Katika historia ya Urumi tunajifunza kuwa Warumi walimwona mwanamke kama mtoto anayetakiwa kuangaliwa na kukemewa. Akiolewa yeye na mali yake ni mali ya mume. Akikosea, mume alikuwa na mamlaka ya kupitisha hukumu yoyote.aliyoweza hata ya kutoa adhabu ya kifo.



Mwanamke alikatazwa kushiriki katika jambo lolote. Hakuruhusiwa kutoa ushahidi wala kumuwekea mtu dhamana. Mumewe akifariki, Shemeji zake walikuwa na haki ya kumrithi.



Hapo awali katika historia ya Urumi, wanawake walibakia nyumbani na ukahaba (umalaya) haukujulikana. Mtu kufanya kitendo cha mapenzi na mkewe kama vile kumbusu mkewe hadharani ilionekana ni kitendo kiovu na utovu wa adabu na heshima. Kiongozi mmoja wa Kirumi alishutumiwa vibaya na raia wake kwa kitendo cha kumbusu mkewe mbele ya binti yake.



Warumi waliposongambele katika maendeleo ya kijamii, waliona wamkomboe mwanamke kwa kulegeza sharia ya ndoa kiasi cha kuifanya kama mkataba wa wawili wanaopendana. Wanawake walipewa haki ya kurithi na walikuwa huru na mamlaka ya baba au mume. Katika wakati huu sio tu kuwa wanawake wa Kirumi walijitegemea kiuchumi bali walikuwa wakiwakopesha waume zao kwa nba kubwa kwa kiasi kwamba Wanaume ambao wake zao walikuwa matajiri walijikuta wamekuwa watumwa wao.
Kutaliki kulikuwa jambo jepesi na ndoa zilikatika bila ya sababu za msingi.


Kwa mfano Seneca (4B.C - 65 A.D), Mwanfalsafa Mashuhuri wa Kirumi alitoa shutuma kwa watu wake kutokana na kiwango cha talaka kilicho kithini katika jamii yake kwa kusema: "Now divorce is not regarded as something shameful in Rome. Woman calculate their age by the number of husbands they have taken."



Tafsiri:
"Talaka sasa hainonekani kuwa nijambo la aibu hapa Urumi. Wanawake wanahesabu umri wao kwa idadi ya Wanaume waliofunga nao ndoa."



Yaani, wanawake wa Kirumi katika wakati huo wa historia, kwa uhuru waliopewa na jamii waliweza kuolewa na wanaume wengi kwa muda mfupi. Kwa mfano Martial (43 A.D - 104 A.D) ameeleza juu ya mwanamke aliyeolewa na wanaume kumi. Juvenal (60 A.D - 130 A.D) ameandika juu ya mwanamke aliyeolewa na wanaume wanane, mmoja baada ya mwingine, katika kipindi cha miaka 8. St. Jerome (340 A.D - 420 A.D) ameeleza juu ya mwanamke wa ajabu ambaye mume wake wa mwisho alikuwa wa 23, mmoja baada ya mwingine. Yeye mwenyewe kwa mumewe huyo wa mwisho alikuwa ni mke wake wa 21. ni katika wakati huu uzinifu ulianza kustawi na wazinifu hawakuhesabiwa kuwa ni wakosaji wanaostahiki kuadhibiwa.



Katika historia hii fupi, tunajifunza jisni mwanamke alivyokandamizwa na jamii hapo awali na tumeona hali ya mwanamke ilivyokuwa baada ya kukombolewa. Je, ukombozi huu ulimpa mwanamke hadhi yake anayostahiki?




                   







           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 612


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

Zaka ni nini? Nini maana ya zaka katika uislamu
Zaka, kilugha ni kukua; kubariki na kuzidi kheri. Soma Zaidi...

msimamo wa uislamu juu ya kupanga uzazi na uzazi wa mpango
Msimamo wa Uislamu juu ya kudhibiti uzaziKama tulivyoona, msukumo wa kampeni ya kudhibiti kizazi, umetokana na mfumo mbaya wa kijamii na kiuchumi ulioundwa na wanadamu kutokana na matashi yao ya ubinafsi. Soma Zaidi...

Sifa za imamu wa swala ya jamaa
Post hii inakwenda kukupa sifa za imamu wa msikitini anayepasa kuswalisha swala ya jamii. Soma Zaidi...

Fiqh.
Kipengele hichi tutajifunza chimbuko la fiqh na maana ya figh. Soma Zaidi...

Zijuwe funga za kafara na jinsi ya kuzigunga
Post hii itakufundisha kuhusu funga za kafara, zinavyotokea na na jinsi ya kuzifunga. Soma Zaidi...

Jinsi Uislamu Ulivyokomesha Biashara ya Utumwa wakati na baada ya Mtume Muhammad (s.a.w)
- Uislamu ulieneza nadharia kuwa wanaadamu wote ni sawa na wote ni watumwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s. Soma Zaidi...

Ni zipi nguzo za swaumu na masharti ya Swaumu
Soma Zaidi...

ijuwe maawe maan ya kusimamisha swala
Soma Zaidi...

Maana ya uadilifu na usawa na tofauti zao
Posti hii itakwenda kukufunza utofauti kati ya uadilifu na usawa Soma Zaidi...

Kwa nini waislamu wanaoa mke zaidi ya mmoja
Post hiibitakugundisha hekima ya kuruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja katika sheria za kiislamu. Soma Zaidi...

Kusimamisha swala za Sunnah
Nguzo za uislamu, kusimamisha swala za Sunnah (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

hizi ndizo sharti za swala
Soma Zaidi...