Kwa nini waislamu wanaoa mke zaidi ya mmoja

Post hiibitakugundisha hekima ya kuruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja katika sheria za kiislamu.

Hekima ya Ukewenza

Kuna sababu nyingi za kibinafsi, kimaadili, kiuchumi na kijamii zinazoonesha kuwa wakati mwingine, kuoa mke zaidi ya mmoja ni jambo lisilobudi. Hebu turejee mifano ya hali kadhaa zifuatazo:

 


(a)Kama Mke ni Tasa
Mfikirie mwanamume ambaye amehakikisha kuwa mkewe ni tasa na bado anahamu ya kupata mtoto atakayekuwa mrithi wake. Katika hali hii mwanamume huyu atafanya mojawapo katika haya yafuatayo:
(i)Atakaa na kusononeka kwa kukosa mtoto katika maisha yake yote au
(ii)Atamuacha huyu mke asiye zaa iii aoe mwingine anayezaa au
(iii)Atatembea na wanawake wengine nje ya ndoa iii
wampatie watoto, japo kisheria si watoto wake au
(iv)Ataendelea kukaa na mkewe kwa mapenzi na furaha, kisha aoe mke mwingine atakayemzalia watoto ambao watakuwa wake kisheria.
Utakuta, uchaguzi wa kuoa mke wa pili, ndio ulio bora kabisa. Wengi katika jamii ya Kiislamu, wameoa mke wa pili kwa sababu hii:

 


(b)Kama Mke ana maradhi ya kudumu
Mfikirie tena mwanamume ambaye mkewe ana ugonjwa wa kudumu kwa kiasi kwamba hana uwezo wa kutekeleza majukumu yake kama mke. Bila shaka mwanamume huyu atafanya mojawapo katika haya yafuatayo:
(i)Atajizuia na matamanio yake ya kimwili kwa muda wote wa maisha yake uliobakia.
(ii)Anaweza kumtaliki mkewe mgonjwa wakati ambapo anahitajia uangalizi, huruma na mapenzi ya hali ya juu kutoka kwake, iii aoe mke mwingine atakaye tosheleza mahitaji yake, au.
(iii)Anaweza kubakia na mkewe mgonjwa na kufanya uzinifu kwa sin na wanawake wengi nje ya ndoa, au.
(iv)Ataoa mke wa pili atakayemsaidia kumuhudumia mkewe mgonjwa.

 


Hebu tuzijadili hizi hatua tatu za mwanzo kwa mtazamo wa mafundisho ya Uislamu.
Hatua ya kwanza inakwenda kinyume na umbile Ia mwanaadamu. Mwenyezi Mungu (s.w) analifahamu fika umbile Ia mwanaadamu na haja yake ya kutosheleza matamanio ya jimai na ameweka utaratibu mzuri wa sheria ya ndoa wa kutosheleza mahitajio haya ya kimaumbile.

 


Hatua ya pili ni kinyume kabisa ha ubinaadamu. Kumwacha mke kwa sababu amekuwa mgonjwa, badala ya kumuhudumia kwa upendo na huruma, ni kinyume kabisa na utu.
Hatua ya tatu ni haramu na ni uchafu katika Uislamu.

 


Utaona kuwa hatua ambayo itamuwezesha mume huyu aendelee kumtunza mkewe kwa huruma na wakati huo huo aweze kutosheleza mahitajio yake ya kimaumbile kwa utaratibu mzuri wa heshima na ucha-Mungu ni kuoa mke wa pili.

 


(c)Wanawake Wajane:
Wajane ni wanawake waliofiwa na waume zao au waliotalakiwa. Hakuna jamii isiyo na wajane, na idadi yao huongezeka zaidi nyakati za vita ambapo wanaume wengi huuliwa vitani. Je, wanawake hawa warudishwe kwa wazazi au walezi wao na kukaa hivyo hivyo bila ya kukidhi matashi yao ya kimaumbile mpaka wazeeke? Au waachwe wawe Malaya na kuitokomeza jamii kutokana na matatizo mbali mbali yanayosababishwa na zinaa? Kwa vyovyote vile utaona kuwa njia pekee ya kuwahifadhi wanawake wajane na watoto wao ni hii ruhusa ya kuoa mke zaidi ya mmoja hadi wane - kwa kufuata masharti yaliyowekwa.

 


(d)Wanawake wakiwa wengi katika Jamii:
Inatokea katika jamii nyingi wanawake kuwa wengi zaidi kuliko wanaume. Katika jamii hizi, kama tutaweka sheria ya mume mmoja - mke mmoja, kama wanavyodai watetezi wa usawa wa mwanamke, wanawake watakao kosa wanaume wa kuwaoa watakwenda wapi? Watafanyaje ili kukidhi matashi yao ya kimaumbile? Je, kama watajizuilia mpaka wazeeke huoni hii itawaathiri kimwili, na kisaikologia na kuwafanya wasiwe watu wenye manufaa katika jamii? Nani atakayetoa hifadhi kwa wanawake hawa kiuchumi na kimaadili? llivyo katika maumbile ya mwanaadamu, kila mwanamke wa kawaida anahitajia kuwa na mwanamume anayempenda na kumhurumia. Hivyo, wanawake hawa watakapowakosa wanaume wa ndoa, watafanya kila hila ya kuwashawishi wanaume kwa kuwawekea mitego mbali mbali kama vile kujipitisha mbele yao wakiwa wamejipodoa na kujiremba, kutembea mbele yao uchi, kuzurura kwenye majumba ya sinema, n.k., ambayo itawanasa na kuwatumbukiza katika zinaa.

 


Mfikirie mwanamke anayeishi kwa kuvizia wanaume. Je, atakuwa na utulivu na usalama katika maisha yake? Je, jamii yenye wanawake wa namna hii wa kuwavizia na kuwateka kwa tashiwishi waume za watu, inaweza kuwa jamii yenye amani na furaha? Wanawake wa namna hii mara nyingi wamekuwa ndio chanzo cha vurugu katika unyumba wa watu, kuwafitinisha watu na kusababisha vifo. Ikitokea mwanamke wa namna hii kupata mimba, jukumu Ia kumlea mtoto ni lake mwenyewe. Hivyo, watoto wanaozaliwa nje ya ndoa mara nyingi hukosa malezi mazuri na wengi wao huishia kuwa wezi wavuta bangi, na wahuni wa kupindukia katika jamii.

 


Kwa vyovyote vile iko haja kwa kila mwanamke kupata mume wa kukidhi haja zake na kuhifadhi maisha yake na utu wake. Uislamu umetoa ruhusa ya kuoa wake zaidi ya mmoja hadi wanne ili kumfanya kila mwanamke anayetaka kuolewa, aolewe na kupata hifadhi na haki zake zote zinazomstahiki.
Kwa nini mwanamke asiruhusiwe kuolewa na Mume zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja?

 


Wapinzani wa ukewenza, wanadai kuwa ili pawe na usawa, wanawake waruhusiwe kuolewa na mume zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja endapo wanaume wataruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.

 


Kimaumbile na kisaikolojia, mwanamke ni wa mwanamume mmoja. llivyo, takriban katika jamii zote za ulimwenguni, mwanamume ndiye kiongozi wa familia. Fikiria ingalikuwaje kama familia moja ingalikuwa na viongozi wawili au zaidi!

 

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1526

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Hili ndio lengo la kufunga.

Ni kwa nini Allah ametutaka tugunge. Je kuna lengo gani hasa katika kufunga.

Soma Zaidi...
Hadhi na Haki za Mwanamke katika jamii mbalimbali hapo zamani

Utangulizi:Uislamu unamuelekeza mwanaadamu namna nzuri ya kuendesha maisha yake katika kila kipengele cha maisha akiwa binafsi, katika familia na katika jamii.

Soma Zaidi...
Mambo muhimu ya kuzingatia katika kujenga uchumi wa kiislamu

Nazingatio muhimu katika uchumi unaofuata sheria za kiislamu.

Soma Zaidi...
Nini kifanyike baada ya mazishi ya kiislamu

Huu ni utaratibu unaotakiwa kufanyika baada ya kuzika.

Soma Zaidi...
Ijuwe swala ya Tawbah na jinsi ya kuiswali

Post hii itakufundisha kuhusu swala ya sinnah ya tawba.

Soma Zaidi...
Mafungu ya urithi katika uislamu

Hspa utajifunza viwango maalumu vya kutithi mirathi ys kiislamu.

Soma Zaidi...
Sanda ya mwanamke na namna ya kumkafini

Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Namna lengo la zakat linavyofikiwa

Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...