image

Hili ndilo hasa lengo la kuamrishwa kufunga

Hili ndilo hasa lengo la kuamrishwa kufunga

Lengo la Funga



Lengo la funga limebainishwa katika Qur-an pale ilipotolewa amri ya kufunga:


“Enyi mlioamini! Mmeamrishwa kufunga kama walivyoamrishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu ”. (2:183)


Hapa tunabainishwiwa kuwa lengo la kufunga ni kuwafanya Waumini kuwa wacha-Mungu. Neno “Taqwa ” ambalo linatafsiriwa kuwa ni “Uchamungu” lina maana pana zaidi. “Taqwa” ni hali ya kuhofu ghadhabu za Mwenyezi Mungu (s.w) ambayo humfanya mja ajiepushe mbali na yale yote yanayomghadhibisha Mwenyezi Mungu (s.w) na ayaendee mbio kwa unyenyekevu na kwa jitihada kubwa yale yote aliyoamrisha Mwenyezi Mungu (s.w) na yale yote anayoyaridhia. Maana ya ‘Taqwa’ inabainishwa vyema na Hadith ifuatayo:



Siku moja Umar (r.a) alimuuliza Ubbay bin Ka ’b (r.a) amueleweshe maana hasa ya Taqwa. Ubbay (r.a) alijibu: “Amir Muuminin, umewahi kupita njia ya kichaka chenye miba?” Umar (r.a) akajibu: “Naam, nimepita mara nyingi” Kisha Ubbay (r.a) akamuuliza ni hadhari gani uliyoichukua wakati ukipita huko? “Nilishikilia na kukusanya pamoja nguo zangu na kutembea kwa uangalifu katika kupita njia hiyo”, alisema Umar (r.a) ili sehemu yoyote ya nguo zangu isije shikwa na miba hiyo”. Kutokana na jibu hili, Ubbay (r.a) alisema: “Hii hasa ndio maana ya “Taqwa”.



Kutokana na mfano huu mtu mwenye “Taqwa” au Muttaq ni yule mwenye shauku na jitihada kubwa kuepukana na kila aina ya mwiba (uovu) katika kila hatua na kila kipengele cha maisha yake yote na wakati huo huo huwa na shauku na jitihada kubwa ya kuyakimbilia mema katika kila hatua ya maisha yake ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu (s.w). Muttaq ni mtu mwenye cheo na hadhi kubwa sana mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w) kama tunavyofahamishwa katika Qur-an:


“... Hakika aheshimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule aliye Muttaq (am chaye Mw enyezi Mungu zaidi) katika nyinyi. Kw a yakini Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mw enye khabari ya mambo yote. (49:13).



Hiki ni cheo kikubwa sana ambacho hakina mfano wake katika vyeo vya hapa ulimwenguni. Cheo hiki hakipatikani kwa kuomba kura au kwa hongo, bali kinapatikana kwa kujizatiti kujiepusha na makatazo yote ya Mwenyezi Mungu (s.w) na kujitahidi kutenda mema na kutekeleza maamrisho yote ya Mwenyezi Mungu (s.w) kwa matarajio ya kupata Radhi ya Mwenyezi Mungu (s.w).




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 485


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

Ni zipi funga za suna, na faida na fadhila zake pamoja na wakati wake wa kufunga
Soma Zaidi...

Yajuwe mandalizi ya Ibada ya hija
Soma Zaidi...

Kufunga Mwezi wa ramadhani kisheria
Soma Zaidi...

Kuandama kwa Mwezi na Kufunga ama kufungua ramadhani, sheria na hukumu za kuangalia mwezi
Soma Zaidi...

Taratibu za ndoa ya kiislamu, hatua kwa hatua
Soma Zaidi...

hukumu na taratibu za biashara ya ushirika na hisa katika uislamu
Soma Zaidi...

Kwa nini lengo la Hija halifikiwi?
Soma Zaidi...

Zijuwe funga za sunnah na jinsi ya kuzifunga
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu funga za sunnah na jinsi ya kuzigunga. Soma Zaidi...

Ni zipi sifa za imamu wa swala?
Soma Zaidi...

Usitamani kifo hata ukiwa mchamungu mno ama muovu mno
Katika uislamu imekatazwa kutamani kufa hata kama utakuwa ni mtu muovu sana ama mchamungu sana. Soma Zaidi...

Faida na umuhimu wa ndoa katika jamii
Hapa utajifunza faida za ndoa katika Jamii na kwa wanadamu kiafya, kiroho, kiuchumi Soma Zaidi...

Je mahari inashusha hadhi ya mwanamke katika jamii
Unadhani mwanamke kupewa mahari kitendo hiki kinaweza kushusha hadhi yake? Soma Zaidi...