Navigation Menu



image

Watu wanaowajibikiwa kuhiji

Watu wanaowajibikiwa kuhiji

Wanaowajibika kuhiji


“...Na Mwenyezi Mungu anawaamrisha watu kufanya Hija katika nyumba hiyo (Al-Ka ’aba) yule awezaye kufunga safari kwenda huko ...” (3:97).



(a) Waliobaleghe



Watoto wa kiume na wa kike ambao hawajabaleghe au hawajafikia umri wa kubaleghe (miaka 15), hawawajibiki kwa Hija hata kama wana uwezo wa kwenda huko. Hata hivyo watoto wanaruhusiwa kuhiji kama tunavyofahamishwa katika Hadith zifu atazo:



Ibn Abbas(r.a) ameeleza kuwa katika safari ya Hija ya kuaga, mwanamke mmoja alimleta mtoto wake mbele ya Mtume na akauliza kama naye anaruhusiw a kuhiji. Mtume (s.a.w) alijibu: “Ndio na pia utapata malipo yake.” (Bukhari).



Jabir (r.a) amehadithia:” Tuliongozana na Mtume (s.a.w) katika msafara wa Hija na tulikuwa pamoja na wanawake na watoto. Tuliitikia - “Labbayka ” kwa niaba ya watoto na tulitupa mawe kwenye minara( kwa niaba yao)”. (Ahmad, Ibn Majah).



Kutokana na Hadith hizi watoto pia wanaruhusiwa kuhiji, na vile vitendo wasivyoweza kuvitekeleza vifanywe kwa niaba yao na wazazi au walezi wao. Kama mzazi au mlezi itabidi ambebe mtoto kwa ajili ya kutekeleza ibada ya tawafu na sa’i, ni lazima anuie kuwa anamfanyia mtoto na haitachanganywa na tawafu na sa’i yake. Hivyo itabidi atufu na kusai tena kwa niaba yake mwenyewe. Ieleweke kuwa Hija ya mtoto haimvui mtu kwenye wajibu wa kuhiji atakapofikia baleghe. Hivyo mtu atakapofikia baleghe atalazimika kuhiji tena iwapo atakuwa na uwezo wa kufanya hivyo.



(b)Wenye Akili Timamu



Mtu aliyepungukiwa au aliyevurugikiwa na akili kama vile kichaa, punguani, taahira, n.k. hawajibiki kwa amrisho lolote lile la Uislamu na hesabu yake ni kama ile ya mtoto ambaye hajafikia baleghe, kwani Mtume (s.a.w) amesema:“Kalamu (ya kuandika amali njema au mbaya ya mja) inasimamishwa kwa watu watatu - mtu aliye lala mpaka aamke, mtoto mpaka afikie baleghe, na kichaa (mgonjwa wa akili) mpaka apone.”



(c)Waungwana



Wafungwa au watumwa hawawajibiki kwa Hija mpaka watakapokuwa huru.



(d)Wenye Uwezo



Wanaowajibika kuhiji ni wale wenye uwezo wa afya, na nauli ya kuwawezesha kufunga safari ya Makka ya kwenda na kurudi, pamoja na matumizi (masurufu) ya safari nzima na matumizi ya kuwaachia familia yake nyumbani. Si vyema mtu kuzunguka huku na huko kuomba omba kwa ajili ya Hija. Halikadhalika si vyema mtu kufunga safari ya Hija na huku hana masurufu ya kumtosha kiasi cha kumpelekea kuwa aanze kuombaomba ili aweze kumaliza safari. Pia si vema mtu kuwaacha ahali zake pasina matumizi ya kawaida katika kipindi chote atakapokuwa safarini na kuwaacha katika hali itakayowapelekea kuwa ombaomba. Kwa ujumla kuombaomba katika Uislam ni haramu. Kwa nini kujikalifisha nafsi na hali faradhi ya Hija ni kwa wale tu wenye uwezo kama isemavyo Qur’an


“.. .Na Mwenyezi Mungu amewajibisha wafanye Hija katika Nyumba hiyo (al-Ka ’aba) kwa yule awezaye kufunga safari kwenda huko. (3:97).
Aidha Allah (s.w) anatuhimiza kuchukua masurufu ya kutosha



“...Na chukueni masurufu (ya kutumia njiani, msiombe) Na hakika masurufu bora ni yale yanayomfanya mtu asiombe. Na nicheni Mimi enye wenyi akili” (2:197).



Ni dhahiri kuwa endapo mtu hana masurufu ya kumtosha yeye mwenyewe kutumia njiani,na ya kumtosha kuwabakishia kitu cha kuwatosha ahali zake, hawajibiki kwa Hija hata kama ana nauli ya kwenda na kurudi. Kama mtu ana uwezo wa mali lakini hana uwezo wa afya kwa sababu ya ugonjwa au uzee, hatawajibika kwa Hija. Mgonjwa atawajibika tena atakapopona endapo atakuwa bado ana uwezo wa kimali. Wazee na wenye magonjwa ya kudumu, kama wana mali ya kutosha kuhiji watawapa ndugu zao Waislamu wakahiji kwa niaba yao, kama tunavyojifunza katika Hadith ifu atayo:



Imesimuliwa na Fazal bin Abbas (r.a) kuwa mwanamke mmoja kutoka katika kabila la Banu Khasham alimuuliza Mtume (s.a.w): “Allah (s.w) amefaradhisha Hija kwa watu wote, lakini baba yangu ni mzee sana kwa kiasi kwamba hawezi kufunga safari hii ya Hija Je, ninaweza kuhiji kwa niaba yake?” Mtume (s.w) alimpa ruhusa ya kufanya hivyo. Hii ilitokea katika Hija ya kuaga. (Bukhari na Muslim).



Ni muhimu kwa wenye kuhiji kwa niaba ya wengine, wawe wenyewe wameshahiji kwa mnasaba wa Hadith ifuatayo:
Abdullah bin Abbas(r.a) ameeleza kuwa katika Hija ya kuaga, Mtume (s.a.w) alimsikia mtu mmoja akiitikia “Labbayka” kwa niaba ya Shubruma. Alimuuliza yule mtu kuwa yeye mwenyewe keshahiji. Alipopata jibu kuwa haja hiji, Mtume (s.a.w) alimuamuru kufanya Hija yake kwanza na ndio baadaye afanye Hija kwa niaba ya Shubruma. (Abu Daud).



Mwenye kuhiji kwa niaba ya mwingine atapata malipo ya Hija sawa na yule aliyefanya Hija kwa niaba yake ambaye ndiye aliyetoa gharama zote za Hija. Pia inajuzu kufanya Hija kwa niaba ya ndugu Muislamu aliyefariki huku akiwa na uwezo na nia ya kuhiji kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:



Amehadithia Abdullah bin Abbas (r.a) kuwa mwanamke mmoja aliuliza: “Mama yangu alinuia kuhiji lakini alifariki kabla ya Kuhiji. Je, naw eza kuhiji kwa niaba yake? Alijibu Mtume (s.a.w)” unaweza, hasa. Jaalia kuwa mama yako alikuwa na deni, je isingelikuwa umeshamlipia deni hilo? Hali kadhalika hili ni deni la Allah (s.w) juu yako na Allah (s.w) ana haki zaidi na deni lake kuliko mw ingine yeyote ”(Bukhari).



Kutokana na Hadith hii Muislamu yeyote aliyekufa na deni la Hija, yaani aliyekuwa na mali na uwezo wa kumuwezesha kuhiji lakini akafa bila ya kuhiji, itabidi warithi wake, kabla ya kugawanya urithi watenge fungu la kutosha kuhiji kwani hili ni deni kwa Allah (s.w). Kisha warithi watamteau miongoni mwao au Muislamu yeyote kwenda kufanya Hija kwa niaba ya marehemu kwa kutumia fungu hilo.



(e)Wasiowekewa kizuizi njiani



Iwapo njia wanayosafiria kwenda Hija itakuwa imewekewa kizuizi au imefungwa kwa karantini (Quarantine), kwa usalama au kwa sababu nyingine yoyote, basi Waislamu wa sehemu hiyo hawatalazimika kwa Hija mwaka huo.



(f)Wanawake waongozane na Maharim



Hija imeamrishwa kwa Waislamu wanaume na wanawake wenye sifa zote hizo zilizotajwa hapo juu (a)-(e), lakini pia mwanamke hatawajibika kwa Hija mpaka apate wa kuongozana naye, awe mume wake au maharimu wake kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:



Abu Sayyid Khudhr (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema:
“Ni haramu kwa mwanamke mwenye kumuamini Allah na siku ya Mwisho kuchukua safari ya siku moja au zaidi bila ya kuandamana na baba yake au kaka yake au mume wake au mtoto wake wa kiume au maharimu wake wengine” (Bukhari).



Imesimuliwa kuwa Sahaba mmoja alieleza kuwa mke wake ameenda kuhiji, na yeye mwenyewe alijiandikisha kwa vita fulani vya Jihadi. Mtume (s.a.w) alimuamuru asiende kwenye vita na badala yake aende kuhiji. (Bukh ari).



Mwanamke ambaye Hija imemuwajibikia na ambaye anaongozana na maharimu wake, hana budi kumtaka ruhusa mumewe. Kama mumewe atamnyima ruhusa, itabidi aende tu kwani mume hana haki ya kumkataza mkewe kutekeleza maamrisho ya Allah (s.w) bali anaweza kumkatalia kufanya kitendo cha Naafilah(Sunnah).



Ames imulia Abdullah bin Umar(r.a) kuwa w akati mmoja mw anamke tajiri alikataliwa kwenda safari ya Hija ya nyongeza. Shauri hili lilipofikishwa kwa Mtume (s.a.w) Mtume (s.a.w) alikubaliana na uamuzi wa yule mumewe. (Dar Qutni).


Kwa ujumla matendo yote ya Naafilah (Sunnah) wanawake watafanya kwa kutaka ruhusa kwa waume zao. Muislamu atakapokamilika kwa sifa zote hizi, (a)-(f) hana budi kuharakisha kukamilisha ibada hii ya Hija, ili baada ya muda asije akapungukiwa na baadhi ya sifa hizi na kushindwa kutekeleza ibada hii. Tukumbuke kuwa tukijichelewesha kufanya Hija kwa uzembe tu baada ya kuwa na uwezo tutakuwa mas-uul (wenye kuulizwa) mbele ya Allah (s.w), endapo tutaondokewa na uwezo wa kuhiji baada ya muda kupita. Daima mwanadamu hajui yanayokuja mbele yake. Mtu anaweza kufilisika au kupatwa na ugonjwa wa kudumu au kufa wakati wowote.Hivyo, daima Muislamu anatakiwa aharakie kutekeleza maamrisho ya Allah (s.w). Ni katika msingi huu Mtume (s.a.w) anatuusia:



“Yeyote anayekusudia kuhiji na aharakishe”. (Abu Daud, Darimi).




                   







           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 939


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

Dua ya kuzuru makaburi, na utaratibu wa kuzuru makaburi
Kuzuru makaburi ni katika matendo ya sunah yaani unapata thawabu kwa kwenda klizuru kaburi. Soma Zaidi...

Mambo anayofanyiwa mtu anayekaribia kufa
Haya ni maandalizi anayofanyiwa mtu aliye katika kilevi cha kifo yaani sakaratul maut Soma Zaidi...

Sanda ya mwanamke na namna ya kumkafini
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Ni nini maana ya swala
Post hii inakwenda kukugundisha kuhusu maana halisi ya ibada ya swala. Soma Zaidi...

darasa la funga
Soma Zaidi...

Je inafaha kuingizwa eda na kutolewa?
Kuingizwa au Kutolewa EdaKatika sheria ya Kiislamu hapana suala Ia kuingizwa au kutolewa eda na Sheikh. Soma Zaidi...

Namna ya kutawadha hatuwa kwa hatuwa.
Post hii inakwenda kukugundisha jinsi ya kutawadha hatuwa kwa hatuwa. Soma Zaidi...

Nguzo za udhu ni sita
Post hii itakufundisha kuhusu nguzo kuu sita za udhu. Soma Zaidi...

Nini kifanyike baada ya mazishi ya kiislamu
Huu ni utaratibu unaotakiwa kufanyika baada ya kuzika. Soma Zaidi...

NAMNA YA KUCHINJA KATIKA UISLAMU
عَنْ أَبِي يَعْلَى شَدَّادِ بْنِ أَوْسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم قَالَ: "إنَّ اللَّهَ كَتَبَ الْإِح... Soma Zaidi...

Jinsi ya kukaa itiqaf na taratibu zake
Hapa utajifunza kuhusu taratibu za ibada ya itiqaf yaani kukaa msikitini kwa ajili ya ibada. Soma Zaidi...

Usawa katika uchumi wa kiislamu
5. Soma Zaidi...