Zijuwe Faida za Kuwa na Istiqama (Msimamo Thabiti)

38.

Zijuwe Faida za Kuwa na Istiqama (Msimamo Thabiti)

38. Kuwa na Istiqama (Msimamo Thabiti)



Muumini wa kweli anayemtegemea Mwenyezi Mungu (s.w) kwa kila hali hana budi kuwa na msimamo thabiti katika kuusimamisha na kuufuata Uislamu. Si muumini wa kweli yule anayeyumba yumba (mudhabidhabina) kwa kuchanganya haki na batili au utii na uasi katika kuendesha maisha yake ya kila siku. Mwenyezi Mungu (s.w) ametuamrisha wale tutoao shahada ya kweli tuuingie Uislamu wote au tuwe Waislamu katika kila kipengele na kila hatua ya maisha yetu na wala tusiuingie nusu nusu. Anatuamrisha:


Enyi mlioamini! ingieni katika Uislamu wote, wala msifuate nyayo za shetani, kwa hakika yeye kwenu ni adui dhahiri. (2:208)
Hivyo, kutamka tu shahada au kusema: “Tunakiri kuwa hapana Mola ila Mwenyezi Mungu na Muhammad (s.a.w) ni Mtume wake” haitoshi kutufanya kuwa Waislamu wale walioahidiwa malipo makubwa huko akhera; bali tutakuwa wa kweli katika shahada zetu iwapo tutaendesha


maisha yetu yote kama alivyotutaka tuishi Mwenyezi Mungu (s.w) na kama alivyotuelekeza Mtume wake (s.a.w). Waislamu watakaokuwa imara katika kuutekeleza Uislamu katika maisha yao ya kila siku, ndio walioahidiwa malipo makubwa ya Peponi katika maisha ya Akhera. Hebu turejee aya chache zifuatazo:


“Wale waliosema: Mola wetu ni Mwenyezi Mungu kisha wakabakia imara (wakawa na msimamo), hao huwateremkia Malaika (wakawaambia), “Msiogope wala msihuzunike, na furahini kwa Pepo mliyokuwa mkiahidiwa. Sisi ni vipenzi vyenu katika maisha ya dunia na katika Akhera, na humo mtapata vitu vinavyopendwa na nafsi zenu, na humo mtapata mtakavyovitaka ”. (41:30-31).


Hakika wale waliosema: “Mola wetu ni Mwenyezi Mungu’, kisha wakatengenea (wakawa na msimamo) hawatakuwa na khofu (siku ya kufa kwao wala baadaye) wala hawatahuzunika. Hao ndio watu wa Peponi, watakaa humo (milele); ni malipo ya yale waliyokuwa wakiyatenda. (46:13-1 4).
Hebu pia tuone jinsi Mtume (s.a.w) alivyotuwaidhi juu ya kuwa na msimamo katika Uislamu wetu:
Sufyaan bin Abdullah (r.a) amesimulia kuwa alisema: Ee! Mtume wa Allah niambie neno juu ya Uislamu ambalo sitakuwa tena na haja ya


kumuuliza mtu mwingine baada ya hapa. Alisema Mtume(s.a.w); ‘Sema: Ninamuamini Mwenyezi Mungu kisha ubakie katika msimamo huo”. (Muslim)
Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: Fuata barabara njia sahihi ya imani na kuwa na msimamo huo, na ujue kwamba hapana yeyote atakayeokoka kutokana na amali yake (nzuri). Mmoja akauliza: Hata wewe Mtume wa Allah? Akajibu (Mtume) hata mimi, ila mpaka Allah anikunjulie Rehema zake na Fadhila zake. (Muslim)


Enyi mlioamini! Kwanini mnasema msiyoyatenda. Ni chukizo kubwa mbele ya Allah kusema msiyoyatenda.
(61:2-3)




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jifunze Main: Dini File: Download PDF Views 1332

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

Zoezi

Maswali mbalimbali yanayohusu elimu ya dini ya kiislamu na mwongozo wa elimu na elimu mazingira.

Soma Zaidi...
(x)Wenye kuepuka lagh-wi

Waumini wa kweli waliofuzu hujiepusha na Lagh-wi.

Soma Zaidi...
jamii somo la 35

Hutekeleza ahadi zao wanapoahidiana na wanaadamu wenziwao maadamu ni katika mipaka ya Allah (s.

Soma Zaidi...
Fadhila za kujenga msikiti

Kuna malipo makubwa kwa ambaye amejenga msikiti kwa ajili ya kuoatavradhi za Allah.

Soma Zaidi...
HADITHI YA MZEE WA KWANZA NA MBUZI

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MZEE WA KWANZA NA MBUZI WAKE.

Soma Zaidi...
Uandishi wa hadithi wakati wa mtume (s.a.w)

Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...