17.
17. Kuepuka kujisifu na kujitukuza
Waislamu tumekatazwa kujisifu sisi wenyewe na pia tumekatazwa kuwasifu wengine kupita kiasi.Mtume (saw) amekataza jambo hili katika Hadith zifuatazo:
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume (saw) amependekeza kwetu kuwa tumtupie mchanga (vumbi) usoni yule anayejihusisha na kuw asifus ifu w atu kupita kiw ango kinachos tahili. (Tirim idh).
Abu Bakar (ra) amesimulia kuwa mtu mmoja alimsifu mtu mwingine mbele ya Mtume (saw). Mtume (saw) alisema mara tatu. “Ole wako umekata kichwa cha ndugu yako!” (Kisha anasema Mtume); Yeyote miongoni mwenu ambaye ataona hapana budi kumsifu mwingine na aseme; Nafikiri fulani yuko hivi na hivi ( ana sifa hizi na hizi) na Allah (sw) atamuhesabu hivyo kama kweli mbele yake anastahiki sifa hizo. Lakini asithubutu mtu kumpachika yeyote sifa ya Ucha-Mungu(wema) juu ya Allah.” (Bukhari na Muslim)
Aidha Allah (sw) ametukataza kujisifu sifu katika aya ifuatayo:
“…Yeye (Allah) ndiye anayekujueni sana tangu alipokuumbeni katika ardhi na mlipokuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msizitakase nafsi zenu; Yeye (Allah) anamjua sana aliyetakasika ”. (53:32)
Kuwasifu sana watu kupita kiasi huwapelekea wale wenye kusifiwa kuvimba vichwa na kujihisi kuwa wao ni watukufu na bora zaidi kuliko wengine katika jamii. Tunayaona madhara makubwa yaliyojitokeza katika jamii ya waislamu kutokana na sifa za kupita kiasi tulizowapachika masheikhe zetu na watu wengine tuliowapachika usharifu, uwalii, ucha-mungu,n.k. Mgawanyiko wa waislamu tunaoushuhudia hivi leo kwenye madh-habu, twarika na matapo mengine mbali mbali, unatokana na dhambi hii ya kuwasifu viongozi wa hayo makundi kupita kiasi.
Pia tunajifunza katika historia kuwa chanzo cha Mitume wa Allah (sw) na watu wema kushirikishwa na Allah (s.w) ni kuwasifu kupita
kiasi. Katika Qur’an (9:30) tunafahamishwa kuwa kuwaiga washirikina waliowatangulia katika kuwasifu kupita kiasi viongozi wao, Mayahudi walimfaya Uzair (Mtu mwema) mwana wa Mungu na wakristo wakamfanya Isa Bin Maryam mwana wa Mungu. Kwa kuchelea watu wa Ummah nao wasijetumbukia kwenye shirki hii ya sifa, Mtume (saw) anatuasa katika Hadith ifuatayo:
“ Imepokelewa kutoka kwa Umar(r.a) kuwa amesema Mtume wa Allah (saw) Msizidishe kwenye kunisifu kama walivyozidisha wakristo ( manasara) katika kums ifu mwana wa Maryam. Mimi ni mja wa Allah tu; kwa hiyo niiteni ;”Mja wa Allah na Mtume wake ”. (Bukhari)
Hivyo muumini wa mkweli hanabudi kujiepusha na kujisifu sifu au kuwasifusifu watu. Na ikiwa hapana budi kumsifu mtu tuzingatie mipaka na tuseme kama alivyotuelekeza Mtume (saw) katika Hadith tuliyoirejea hapa juu. Tabia ya kujisifusifu au kuwasifusifu watu ni tabia ya uwongo, unafiki na ushirikina.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1288
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio
👉2 kitabu cha Simulizi
👉3 Kitabu cha Afya
👉4 Madrasa kiganjani
👉5 Kitau cha Fiqh
👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Tanzu (makundi) za hadithi
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Majina ya vijana wa pangoni
Makala hii inakwenda kukutajia majina ya vijana saba wa pangoni Soma Zaidi...
ZOEZI
Zoezi la 1 (a) Ainisha maana ya sunnah kilugha na kisheria. Soma Zaidi...
UANDISHI WA HADITHI WAKATI WA TABI'INA
Wakati wa Wafuasi wa masahaba (Tabi'ina)101-200 A. Soma Zaidi...
KULA HALALI NA ZILICHO KIZURI NI AMRI KATIKA UISLAMU
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم "إنَّ اللَّهَ طَيِّبٌ لَا يَقْبَلُ إلَّا طَي... Soma Zaidi...
swali langu nikwamba Mimi nimeolewa make wa pili nimeishi ndaniya ndoa miaka 22 mume akafikwa na mauti je ninahaki ya kupata mirathi?
Ni ipi haki ya mwanamke kwenye mirathi endapo atafiwa na mume wake, ilihali yeye ni mke wa pili? Soma Zaidi...
DARSA LA KUJIFUNZA KUHUSU QURAN NA SUNNAH
Soma Zaidi...
quran na sayansi
Soma Zaidi...
(x)Wenye kuepuka lagh-wi
Waumini wa kweli waliofuzu hujiepusha na Lagh-wi. Soma Zaidi...
Faida za kuwa na Huruma Kwenye Uislamu
23. Soma Zaidi...
quran na sayansi
2:UUMBWAJI KWA MAJI YA UZAZIUumbwaji wa mwanadamu umepitia hatua mbalimbali na haya yote yamefanywa kwa sababumaalumu ili tipate mazingatio. Soma Zaidi...