image

Faida za Kuwa mwenye Subira na Uvumilivu

29.

Faida za Kuwa mwenye Subira na Uvumilivu

29. Kuwa mwenye Subira na Uvumilivu



Subira ni kitendo cha kuwa na uvumilivu na utulivu baada ya kupatwa na matatizo au misuko suko mbali mbali katika maisha ya kila siku. Muislamu anatakiwa awe ni mwenye kusubiri baada ya kupata shida au matatizo kama tunavyoamrishwa katika Qur-an:



“Enyi mlioamini! Jisaidieni (katika mambo yenu) kwa kusubiri na kusw ali. Bila shaka Allah yupo pamoja na wanaosubiri” (2:153)


“Enyi mlioamini! Subirini na washindeni wengine wote kwa kusubiri na kuweni imara na mcheni Allah mpate kufaulu ”. (3:200)
Suala la kupatwa na matatizo, misiba na misukosuko mbali mbali ni jambo la kawaida katika maisha ya hapa duniani. Hatuna budi kufahamu kuwa ulimwengu huu haukukusudiwa na Mola Muumba uwe Pepo. Bali umekusudiwa uwe uwanja wa kumtahini mwanaadamu. Hivyo viumbe vyote vilivyomzingira pamoja na matukio na miondoko yote ya maisha viko pale kama vifaa vya kumtahini mwanaadamu. Suala la kutahiniwa mwanaadamu limewekwa bayana katika Qur-an:


Kwa hakika tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyochanganyika, ili tumfanyie m tihani ( kw a amri zetu na m akatazo yetu) kwa hivyo tukamfanya ni Mwenye kusikia (na) mwenye kuona. Hakika Sisi tumembainishia njia . Basi (mwenyewe tena) atakuwa mwenye shukurani au awe mwenye kukufuru (76:2-3)


Ametukuka yule ambaye mkononi mwake umo Ufalme (wote); naye ni mwenye uwezo juu ya kila kitu. Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni (kukufanyieni mtihani); ni nani miongoni mwenu mw enye vitendo vizuri zaidi. Naye ni Mwenye Nguvu na Mw enye Msamaha.
(67:1-2)



“Na tutakufanyieni mitihani mpaka tuwadhihirishe (wajulikane) wale wanaopigania dini miongoni mwenu na wanaosubiri; nasi tutadhihirisha habari zenu. (47:31)


“Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, na hali hamjajiwa na mfano wa (yale yaliyowajia) wale waliopita kabla yenu? Yaliwapata mashaka na madhara na wakatetemeshwa sana hata Mitume na walioamini pamoja nao w akasema: :Nusura ya Mw enyezi Mungu itafika lini?” Jueni kuw a nusura ya Mwenyezi Mungu iko karibu. (2:214).


Je, watu wanadhani wataachwa (wasitiwe katika misukosuko) kwa kuwa w anasema, “Tumeamini? ” Basi ndio w asijaribiwe (wasipate mitihani)? Hapana; bila shaka tuliwatia katika taabu wale waliokuwa kabla yao, na kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha wale walio wa kw eli na kuwatambulisha (wale w alio) waongo. (29:2-3).


“Je! Mnadhani mtaingia Peponi, hali Mwenyezi Mungu hajawapambanua wale waliopigania dini ya Mwenyezi Mungu miongoni mwenu, na kuw apambanua w aliofanya sub ira ?”(3:142)


Ili kukamilisha kusudio hili la kumjaribu (kumtahini) Mwanaadamu Mwenyezi Mungu (s.w) ameupamba huu ulimwengu kwa machungu na matamu yaliyochanganyika. Uzuri au mazuri hayapatikani kwa urahisi ila mpaka kuvuka vikwazo vingi vya matatizo na misukosuko ya namna kadha wa kadhaa. Na uzuri au mazuri yanapopatikana hayabakii milele bali huwa ni ya muda mfupi kwani nayo yamezingirwa na matatizo na mikasa elfu moja na moja. Hii ndio sura halisi ya maisha ya huu ulimwengu. Kwa hiyo wale wanaodhania ulimwengu huu ni mahali pa starehe - kufurahia maisha tu bila ya kuonja machungu yake watakuwa wamejidanganya mno na badala yake wataishi maisha ya huzuni, wasiwasi na kukata tamaa. Kinyume chake, Waislamu wanatakiwa wawe na uhakika juu ya maisha ya huu ulimwengu kuwa ni ya majaribio na mafanikio yatapatikana kwa kutenda wema kwa ajili ya Allah (s.w) na kusubiri au kustahamili mazito, matatizo na misukosuko yote ya maisha itakayowakabili.
Kufanya subira si jambo jepesi bali ni jambo linalohitaji jitihada na azma kubwa. Hebu turejee usia wa Mzee Luqman kwa Mwanae:


“Ewe Mwanangu! Simamisha swala, na uamrishe mema, na ukataze mabaya, na usubiri juu ya yale yatakayokusibu (kwani mwenye kuamrisha mema na kukataza mabaya lazima zitamfika tu taabu); Hakika hayo ni katika mambo yanayostahiki kuazimiwa (na kila mtu). (31:17)


Na anayesubiri na kusamehe (atalipwa wema wake). Bila shaka hilo ni katika mambo makubwa ya kuazimiwa kufanywa (na kila Mu is lamu). (42:43).
Kufanya subira ni kitendo cha hali ya juu cha Ucha Mungu na Mwenyezi Mungu (s.w) Ameahidi malipo makubwa kwa yule atakayejitahidi kusubiri kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:



Sema: “Enyi waja wangu mlioamini! Mcheni Mola wenu. Wale w afanyao wema katika dunia hii watapata wema; na ardhi ya Allah ina wasaa. Na bila shaka wafanyao subira watapewa ujira wao pasipo hisabu”. (39:10)


“Na tutakutieni katika msukosuko wa (baadhi ya mambo haya); hofu na njaa na upungufu wa mali na wa watu na wa matunda. Na wapashe habari njema wanaosubiri. Ambao uwapatapo msiba husema: “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye tutarejea (atatupa jaza yake)” Hao juu yao zitakuw a baraka zitokazo kwa Mola w ao na rehema; na ndio wenye kuongoka. (2:155-157)



Pia Mtume (s.a.w) anatufahamisha kuwa malipo ya subira ni Pepo na kusamehewa madhambi kama tunavyojifunza katika Hadithi zifu atazo:
Abu Hurairah (r.a) amehadithia kuwa Mtume wa Allah amesema, Mwenyezi Mungu (s.w) amesema, “Sina malipo mengine ila Pepo kwa mja wangu aliyeamini ambaye anasubiri wakati ninapomchukulia kipenzi chake kutoka miongoni mwa wakazi wa ulimwengu”. (Bukhari).



Anas (r.a) amesimulia kuwa amemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema kuwa Allah (s.w) amesema, “Ninapomtia msuko suko mja wangu katika vitu vyake viwili vipenzi (macho yake) na akatulia kwa subira, nitamlipa macho yake kw a Pepo ” (Bukhari).



Abu Said na Abu Hurairah(r.a) wameeleza kuwa wamemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema: Aslani Muumini hafikwi na makero (matatizo), magumu au ugonjwa, huzuni au hata wasi wasi moyoni, iwe hakusamehew a dhambi zake. (Bukhari na Muslim).


Imesimuliwa katika mamlaka ya Abu Hurairah kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema Muislamu mwanamume au Muislamu mwanamke ataendelea kuwa katika majaribu juu ya maisha yake, mali yake na watoto wake mpaka amkabili Mw enyezi Mungu (s.w) katika hali am bayo dham bi zake zote zimesamehewa. (Tirmidh).
Hivyo kila Muislamu wa kweli hana budi kujitahidi kusubiri kwa lolote zito litakalomfika na ajiliwaze kwa maliwazo aliyotufunza Mwenyezi Mungu (s.w) kwa kusema:
“...Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake yeye tutarejea ”.(2:156)



Muislamu hatakiwi achoke kusubiri wala asitamani kufa au kuomba kifo kutokana na mazito yaliyomfika:
Anas (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: “Pasiwe na yoyote miongoni mwenu anayetamani kufa (au anayeomba kifo) kwa sababu ya tatizo lolote lililomfika. Kama amefika mwisho wa kuvumilia naaseme: “Ee Allah nibakishe hai iwapo kuishi ni bora zaidi kwangu na nifishe kama kufa ndio bora kwangu”. (Bukhari na Muslim).



Maeneo ya subira



Katika Uislamu subira inatakiwa ihudhurishwe katika maeneo makuu yafuatayo:
Kwanza: kusubiri unapofikwa na misukosuko au matatizo mbali mbali ya kimaisha miongoni mwa khofu, kufiwa, kuugua, kuuguliwa, kukosa maslahi ya kimaisha na matatizo mengine mbali mbali yanayowafika wanaadamu katika maisha ya kila siku.



Pili: kusubiri au kuwa wastahimilivu katika kutekeleza maamrisho ya Allah (s.w) katika maisha yetu yote. Maamrisho kama kusimamisha swala, kufunga Ramadhan, kuwatendea wema wazazi, mayatima, maskini, majirani na wanaadam wengine, kuchunga haki za wengine, (n.k) ni matendo mja anayotakiwa aendelee kuyafanya mpaka mwisho wa maisha yake. Juu ya kusimamisha swala, tunaamrishwa katika Qur-an:
“Na waamrishe watu wako kuswali, na
uendelee mw enyew e kufanya hivyo...” (20:132).


Tatu: kusubiri au kuwa wavumilivu katika kumtii Allah (s.w) kwa kuacha yale aliyotuharamishia. Maovu mengi yaliyoharamishwa na Allah (s.w), machoni mwa mwanaadamu yanaonekana kuwa mazuri na starehe yenye mvuto mkubwa. Kwa mfano nani asiyeona jinsi ulevi, uzinifu, muziki, kamari, riba, hongo, nyama ya nguruwe, n.k. vinavyowavutia walimwengu na kuwazamisha humo mamilioni.
Mtume (s.a.w) amesema:



Pepo imezungukwa na yasiyopendeka (vikwazo) na Moto umezungukwa na vitu vya anasa (carnal desires). (Muslim)
Nne: ni kusubiri au kustahimili maudhi kutoka kwa wanadamu wenzetu. Misukosuko na matatizo mengi yanayomkabili mwanaadamu ni yale yanayosababishwa na wanaadamu wenzake. Muislamu wa kweli hatalipiza kisasi kwa maovu aliyofanyiwa na mwingine, wala hatamuapiza na kumlaani aliyemfanyia maovu hayo bali atastahimili kwa matarajio ya kupata malipo makubwa kutoka kwa Allah (s.w).
Waislamu tunatakiwa mara kwa mara tumuombe Allah (s.w) atumiminie subira kama Yeye mwenyewe anavyotuelekeza kuomba:


~ ~ ~
“... Mola wetu! Tumiminie subira na tufishe hali ya kuwa Waislamu”. (7:126)



“Mola wetu! Tumiminie subira na uithibitishe miguu yetu, na utusaidie juu ya watu hawa makafiri”. (2:250).




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1177


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

HADITHI YA MZEE WA KWANZA NA MBUZI
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MZEE WA KWANZA NA MBUZI WAKE. Soma Zaidi...

Umbwaji wa mwanadamu kutoka Nutfa (tone la mbegu za uzazi), alaqah (tone la damu, mudgha (pande la nyama) na kuwa mtu kamili
عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم ... Soma Zaidi...

Faida za kuwa na Huruma Kwenye Uislamu
23. Soma Zaidi...

Husaidia wenye matatizo katika jam ii
Huwa wepesi wa kutoa msaada kwa hali na mali kwa wanaadamu wenziwe wanaohitajia msaada. Soma Zaidi...

ndoto za kweli
Soma Zaidi...

Zoezi la 3
Kipengele hichi kina maswali mbalimbali kuhusiana na dini na mitazamo mbalimbali. Soma Zaidi...

Mtazamo wa Uislamu juu ya usawa kati ya mwanaume na mwanamke
Soma Zaidi...

Husimamisha swala
Husimamisha swala katika maisha yao yote. Soma Zaidi...

(x)Wenye kuepuka lagh-wi
Waumini wa kweli waliofuzu hujiepusha na Lagh-wi. Soma Zaidi...

Tanzu (makundi) za hadithi
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Elimu
Uwanja wa elimu na maarifa Soma Zaidi...

Epuka kuwa muoga na yajue madhara ya uwoga
36. Soma Zaidi...