2. Kuwa na Hekima

Elimu, pamoja na ubora wake, hainufaishi bila ya kutumiwa kwa hekima. Kufanya jambo kwa hekima ni kufanya jambo kwa kutumia ujuzi unaostahiki na kwa kufuata utaratibu unaostahiki kulingana na mahali na wakati kwa kuzingatia mwongozo na mipaka ya Allah (s.w) na Sunnah ya Mtume wake.Kila Muumini anawajibika kufanya mambo yake yote kwa ujuzi wa kutosha. Kabla Muislamu hajafanya jambo lolote anatakiwa afahamu len

go la hilo analolifanya na je, hilo lengo linampelekea kumuabudu Mola wake na kuwa Khalifa wake au la. Baada ya kulifahamu lengo hanabudi kuwa na ujuzi na mbinu zinazostahiki kumfikisha kwenye lengo kwa wepesi na kwa ufanisi. Asichague njia ndefu na ngumu akaacha njia fupi na nyepesi inayowafikiana na mwongozo wa Allah (s.w) na Sunnah za Mitume wake.Hekima ni katika vipengele vya tabia njema vilivyo azizi anavyotakiwa avipiganie Muumini ili awe na hadhi inayostahiki, hadhi ya Ukhalifa wa Allah (s.w) hapa ulimwenguni. Waumini hatuna budi kufanya mambo yetu kwa hekima na daima tumuombe Allah atuzidishie Hekima.“(Allah) Humpa hikma amtakaye, na aliyepewa hikma bila shaka amepewa heri nyingi. Na hawakumbuki ila wenye akili.” (2:269).