Menu



HISTORIA YA UANDISHI WA HADITHI

Historia fupi ya uandishi wa Hadith za Mtume (s.

HISTORIA YA UANDISHI WA HADITHI

Historia fupi ya uandishi wa Hadith za Mtume (s.a.w)
Tofauti na Qur-an, ambayo iliandikwa mara tu baada ya kushushwa chini ya malekezo na usimamizi wa Mtume (s.a.w) mwenyewe, Hadith za Mtume (s.a.w) ambamo ndani yake ndio tunapata sunnah yake, zimeandikwa na watu kulingana na walivyomuona, au walivyomsikia. Historia ya uandishi wa Hadith za Mtume (s.a.w) katika vitabu vya Hadith , imechukua takriban muda wa karne tatu. Kwa kurahisisha tutaigawa historia ya kuhifadhiwa Hadith katika maandishi katika hatua nne zifuatazo:Β  - Wakati wa Mtume (s.a.w).
- Wakati wa Maswahaba wa Mtume (s.a.w).
- Wakati wa Tabi'iina.
- Wakati wa Tabii Tabi'iina.

Wakati wa Mtume (s.a.w)
Wakati wa Mtume (s.a.w), hapakuwa na uandishi mkubwa wa Hadith kwa sababu:

Kwanza, Mtume mwenyewe alikuwepo, hivyo kilichokuwa muhimu kwa Masahaba ni kufuata mafundisho ya Mtume(s.a.w) na kuigiza mwenendo wake,kila walipokwama katika utendaji au kila walipotatizwa na tatizo lolote, walimwendea Mtume(s.a.w) na aliwakwamua au kuwatatulia tatizo lolote walilokuwa nalo.

Pili, Masahaba katika kipindi hiki walijishughulisha sana na kuandika, kusoma na kuhifadhi Qur-an moyoni na kuitekeleza katika maisha yao ya kila siku.

Tatu, kwa kuwa mwanzoni Mtume (s.a.w) aliwakataza Masahaba wake kuandika Hadith, walizoea kutoandika Hadith hata wakati waliporuhusiwa kuandika na walipendelea kutoandika kuliko kuandika Hadith.

Nne, katika wakati huu wa Mtume (s.a.w) Masahaba walishughulika sana katika harakati za kuuhami Uislamu ambao ulikuwa umesongwa sana na maadui wake ambao walipania sana kumuua Mtume, Uislamu na Waislamu.

Kutokana na sababu hizi nne na nyinginezo, uandishi wa Hadith haukupewa nafasi nzito katika kipindi hiki cha Mtume (s.a.w). Hivyo, Hadith nyingi zilibakia katika matendo na vifua vya Masahaba. Masahaba waliokuwa karibu sana na Mtume (s.a.w) kwa muda mrefu wa maisha yao, walihifadhi Hadith nyingi zaidi kuliko wale waliokaa mbali na Mtume (s.a.w).Β 

Miongoni mwa Masahaba waliofahamika kuwa mashuhuri kwa kuhifadhi Hadith nyingi ni Abu Hurairah, bibi Aysha (mkewe Mtume (s.a.w)) 'Abdullah bin 'Umar, 'Abdullah bin 'Abbas, na Abdullah bin 'Amr na Abdallah bin Masu'ud (r.a)


                   

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Main: Dini File: Download PDF Views 458

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰2 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰3 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰4 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰5 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana: