37. Kuepukana na Kukata TamaaPia Muislamu hatakiwi kukata tamaa na Rehema za Mwenyezi Mungu (s.w). Hakuna kinachoshindikana kwa Mwenyezi Mungu. Muislamu hana budi kufanya jitihada katika kufanikisha jambo muhimu la maisha kwa kufuata njia za halali anazoziridhia Mwenyezi Mungu (s.w). Kama jambo hilo lina kheri na yeye, basi Mwenyezi Mungu (s.w) atalifanikisha. Mzee Yaquub (a.s) akiwausia wanawe wasichoke kumtafuta Yusuf na ndugu yake aliwaambia:“Enyi wanangu! Nendeni mkamtafute Yusuf na nduguye, w ala msikate tamaa na Rehema ya Mwenyezi Mungu. Hawakati tamaa na Rehema ya Mw enyezi Mungu isipokuw a w atu makafiri”. (12:87).Pia iwapo baada ya Muislamu kufanya juhudi na kutumia uwezo wake wote, hakupata mafanikio aliyotarajia, asikate tamaa bali aridhike kuwa matokeo hayo ndiyo yenye kheri kwake kwa kuzingatia Qur-an:


“... Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mugu ndiye anayejua, (lakini) nyinyi hamjui”. (2:216).