Uandishi wa hadithi wakati wa tabiina (wafuasi wa maswahaba)
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Uandishi wa Hadith Wakati wa Tabi’ina (wafuasi wa maswahaba),
(101 A.H – 200 A.H).
- Ni karne ya pili ambapo wanazuoni wengi walijitokeza waliojizatiti katika kazi ya ukusanyaji wa Hadith kutoka vituo mbali mbali vya elimu.
- Vituo mashuhuri vya elimu kipindi hicho vilikuwa; Madinah, Makkah, Baghdad, Basra, Khurasan na Kufa.
- Pia ni kipindi hiki ambapo walitokea maimamu wanne mashuhuri wa Fiqh ambao ni;
- Imamu Abu Hanifa Al-Nu’man bin Thabit (80 – 150A.H).
- Mwanachuoni wa Qur’an na Hadith katika mji wa Kufa, Iraq.
- Alitoa Fat’wa za kifiq kwa kutumia Qur’an, Hadith na Ijmaa.
- Hakuandika kitabu chochote.
- Imam Malik bin Anas (95 – 179 A.H).
- Mwanachuoni mcha-Mungu wa mji wa Madinah.
- Aliandika kitabu mashuhuri cha Hadith kiitwacho, “Al-Muwatta” kilichotegemewa na umma wa waislamu katika ibada maalum tu.
- Alifutu mas’ala ya Uislamu kwa mujibu wa Qur’an na Sunnah tu.
- Imam Muhammad bin Idris Al-Shafii (150 – 204 A.H).
- Mwanachuoni mkubwa wa sheria za Kiislamu aliyezaliwa Gaza, Palestina.
- Imam Malik bin Anas ni miongoni mwa walimu wake.
- Alitoa fat’wa kwa mujibu wa Qur’an, Hadith na Ijmaa (na Qiyaas pia).
- Hakuandika kitabu chochote cha Hadith.
- Imam Ahmad bin Muhammad bin Hambal (164 – 241 A.H).
- Mwanachuoni mkubwa wa Fiqh na elimu ya Hadith aliyezaliwa mji wa
Baghdad, Iraq.
- Imam Shafii alikuwa mwalimu wake.
- Imam Ahmad alitoa fat’wa tofauti na mwalimu wake, Imam Shafii lakini
waliheshimiana sana.
- Aliandika kitabu cha Hadith kiitwacho, “Isnad ya Ibn Hambal”
kilichokusanya zaidi ya Hadith 30,000.
- Pamoja na jitihada kubwa za ukusanyaji wa Hadith, wanazuoni hawa waliandika vitabu mashuhuri viwili tu;
- Al-Muwatta cha Imam Malik bin Anas.
- Isnad ya Ibn Hambal (Musnad Ahmad) cha Imam Ahmad bin Hambal.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 Simulizi za Hadithi Audio 👉4 Kitabu cha Afya 👉5 ai web app 👉6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
nini maana ya Unafiki na sifa za unafiki katika quran na sunnah
Mnafiki ni yule anayeukubali Uislamu mdomoni (kwa kauli tu) lakini moyoni mwake na katika matendo yake anaukanusha.
Soma Zaidi...Kitabu Cha Dua 120
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.
Soma Zaidi...Uandishi wa hadithi wakati wa mtume (s.a.w)
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Uandishi wa hadithi wakati wa tabii tabiina
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...