26. Kujiepusha na Chuki na UaduiMuislamu anatakiwa kwa kadiri ya uwezo wake ajitahidi kujiepusha na matendo yote yale yatakayosababisha kutoelewana baina yake na watu wengine. Ajiepushe na kujenga chuki na uadui moyoni mwake dhidi ya mtu yeyote na ajitahidi kujiepusha na kuwafanyia wengine yale yote yatakayowafanya wajenge chuki na uadui dhidi yake au dhidi ya watu wengine. Mtume (s.a.w) anatuusia:“Msikate uhusiano, msijiingize katika uadui, msikaribishe chuki na husuda dhidi ya wengine na msiwadharau w engine. Kuw eni ndugu kati yenu na kuweni watumwa wa Allah. Hapana ruhusa kwa mtu kukata uhusiano na ndugu yake zaidi ya siku tatu ”. (Bukhari).Katika Hadithi nyingine imeelezwa kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Hairuhusiwi kwa Mu is lamu kuvunja uhusiano na Mu is lamu mwenzake zaidi ya siku tatu. Baada ya siku tatu kupita na ikatokea akakutana na ndugu yake, ni lazima amsalimu. Kama ataitikia salamu basi wote watapata thawabu (ujira) na kama hataitikia salaam, dhambi zitakuwa juu yake (yule asiyeitikia) na yule aliyeanza kutoa salaam atakuw a hana hatia na dhambi ya kukata uhusiano. (Abu Daud).Kama Waislamu, kwa bahati mbaya, imetokea wamegombana, waislamu wengine wanawajibika kuwasuluhisha. Kuwapatanisha waliogombana ni amri ya Allah (s.w) kama ilivyo katika aya ifuatayo:


“Kwa hakika Waislamu wote ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu na mcheni Allah ili mrehemewe”. (49:10)
Katika kusuluhishwa, yule aliyemkosea mwenzake hana budi kukiri makosa yake na kisha kumtaka samahani yule aliyemkosea. Mtume (s.a.w) ametuusia:


Yule ambaye amehujumu haki au heshima ya ndugu yake hana budi kumtaka samahani leo kabla ya siku hiyo kuja ambayo hatakuwa na dirham wala dinar (za kulipa); kama atakuwa na amali njema, basi zitachukuliwa kiasi kile kinacholingana na hujuma aliyomfanyia ndugu yake. Kama hatakuwa na amali yoyote njema, basi madhambi ya yule aliyedhulumiwa yatachukuliwa na kuwekwa katika hesabu yake.” (Bukh ari).Chuki na uadui ni kazi ya shetani. Penye chuki na uadui hapana jema lolote linalofanyika na ni furaha kwa shetani. Chuki inayoruhusiwa kwa waislamu ni ile ya kuchukia uovu na maadui wa Allah (s.w) - maadui wa Uislamu na Waislamu. Waislamu wanakatazwa kuwa na urafiki na maadui wa Allah (s.w):


“Enyi mlioamini! Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki, mnawapelekea (habari zenu) kwa ajili ya urafiki hali ya kuwa w ameshaikanusha haki iliyokujieni...” (60:1)


“Enyi mlioamini! Msifanye urafiki na watu ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia; na wamekata tamaa ya kupata malipo ya Akhera kama w alivyokata tamaa makafiri w alio makaburini” (60:13)


“Enyi mlioamini! Msiwafanye marafiki wale walioifanyia mzaha na mchezo dini yenu miongoni mwa wale waliopewa kitabu kabla yenu na miongoni mwa makafiri.Na mcheni Mwenyezi Mungu kama nyinyi ni wenye


kuamini. (5:57)
Pamoja na hivyo haina maana Waislamu wasiwafanyie uadilifu hawa maadui wa Allah na maadui wa Uislamu, bali Waislamu wataendelea kuwatendea wema na kuishi nao kwa wema iwapo watataka amani.