picha

Hadhi na haki za mwanamke katika uislamu

4.

Hadhi na haki za mwanamke katika uislamu

4. HADHI NA HAKI ZA MWANAMKE KA11KAJAMII YA KIISLAMU.
Maadui wa Uislamu na watu wasio ufahamu Uislamu vizuri, wameuangalia Uislamu kama wanavyoziangalia jamii nyinginezo na kushutumu Sheria za Kiislamu kuwa nazo zinamkandamiza mwanamke. Kutokana na shutuma hizi imekuwa ni wajibu kwetu katika sehemu hii kuonesha kwa uwazi jinsi Uislamu unavyompa mwanamke hadhi na haki zake. Tumeshaona kuwa wale wote waliojipiga kifua kuwa wanamtetea mwanamke na kumpa hadhi yake anayostahiki, harakati zao ziliishia ukutani. Walivunja familia ambayo ndio msingi wa jamii na walizidi kumdhalilisha mwanamke mpaka kufikia uduni kuliko ule wa hayawani.


Bila shaka watetezi hawa wa haki na hadhi ya mwanamke hawakuwa na nia mbaya ya kuzidi kumdunisha na kumkandamiza bali kosa lao kubwa ni kule kujiingiza kwao kwenye kazi wasio na ujuzi nayo. Allah (s.w) ndiye aliyemuumba mwanaadamu na vyote vilivyomzunguka. Hivyo ni Allah (s.w) pekee mwenye haki na uwezo wa kumuwekea mwanaadamu muongozo wa maisha mwenye kumuelekeza namna ya kukiendea kila kipengele cha maisha yake ya binafsi, familia, uchumu, siasa, utamaduni na maisha yote ya kijamii kwa ujumla ili aweze kuishi kwa furaha na amani na hapo hapo afikie lengo Ia kuumbwa kwake.


Ni dhahiri kwamba watu wanaokana au wasiotambua kuwepo kwa Allah (s.w) na mwongozo wake, ambao hujiundia sheria za kuiongoza na kuilinda jamii kutokana na msukumo wa matashi yao, kamwe hawawezi kuweka utaratibu utakao mhakikishia kila mtu katika jamii kupata haki zake zote na kuishi kwa furaha na amani. Hivyo wale wote wasiofuata mwongozo wa Allah (s.w), wasitegemee kamwe kupata haki zao na kuishi kwa furaha na amani katika jamii zao.



Tofauti na sheria za jamii zinazotungwa na binaadamu baada ya haja kutokea, sheria za Kiislamu kwak uwa zimewekwa na Allah (s.w), Mjuzi Mwenye Hekima, haziko pale kutosheleza haja ya dharura, bali zimekuwa pale hata kabla ya Adam (a.s) kuja hapa ulimwenguni. Hivyo ni vyema ifahamike tangu mwanzo kuwa katika mjadala wetu huu utaratibu au sheria ya Kiislamu ambayo inamhakikishia mwanake kupata haki na hadhi yake, haikutungwa baada ya kuona kuwa mwanamke anakandamizwa na kupuuzwa, bali ilikuwepo sheria hiyo hata kabla ya kuumbwa Adam na Hawa. Allah (s.w) anamfahamu vyema mwanaadamu kuwa endapo hatapewa mwongozo kutoka kwake na kuufuata ni muhali kuepukana na maisha hayo ya kudhulumiana na hasa wenye nguvu kuwadhulumu wanyonge.



Ili kutofautisha hatua za kumkomboa mwanamke zilizochukuliwa na jamii zilizojitahidi kufanya hivyo na hatua zinazochukuliwa na sheria ya Kiislamu, hapa tutajihusisha na vipengele vitatu vifuatavyo:-
1.Mtizamo wa Uislamu juu ya Usawa kati ya mwanamume na mwanamke.
2.Haki za mwanamke katika Uislamu.
3.Hifadhi ya mwanamke na maadili ya Jamii.


                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF Views 1705

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 web hosting     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 ai web app     👉5 Dua za Mitume na Manabii     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zinazofanana:

quran na sayansi

2:UUMBWAJI KWA MAJI YA UZAZIUumbwaji wa mwanadamu umepitia hatua mbalimbali na haya yote yamefanywa kwa sababumaalumu ili tipate mazingatio.

Soma Zaidi...
Assalam Baada yakufariki wazazi wake mtume alilelewa nanani???

Mtume Muhammad s.a.w amezaliwa yatima asiyena baba. Lakini hii haikumfanya asipate maelezo bora yaliyo mazuri. Je unajuwa aliyemlea baada ya kufariki kwa mama yake?.

Soma Zaidi...
(xi)Hutoa Zakat na Sadakat

Waumini wa kweli waliofuzu hutoa Zakat wakiwa na mali na hutoa misaada na huduma waziwezazo kwa wanaadamu wenziwe kwa kadiri ya haja ilivyojitokeza.

Soma Zaidi...
Mawaidha Kutokwa kwa Shekhe

Karibu kwenye Darsa za mawaidha na Mafundisho ya dini.

Soma Zaidi...
Uchambuzi wa hadithi za mtume

Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...