image

kuwa mwenye huruma na faida zake

25.

kuwa mwenye huruma na faida zake

25. Kuwa na UpendoUpendo ni matunda ya vipengele vingi vya tabia njema vikiunganishwa pamoja. Kwa mfano kuongea na watu vizuri, kuwahurumia wakati wanamatatizo au kuwafanyia wema wa aina yoyote kama kuwasaidia kazi, kuwakirimu kitu n.k. ni miongoni mwa maadili mema yanayoleta upendo na mahusiano mema kati ya wanaadamu. Kinyume chake, kauli mbaya, ukatili, usengenyi, fitina, uchochezi, husuda, na matendo mengine mabaya kama haya yakitendwa kwa wan adam hujenga chuki na uadui.Uislamu unatutaka tudumishe upendo kati yetu kwa kuwafanyia wenzetu mema tunayoyapenda na ambayo tungeliwataka wengine watufanyie. Pamoja na kusisitizwa na Uislamu kuwafanyia wengine mema na kujiepusha na kuwaudhi, tunashauriwa pia tuwe na tabia ya kupeana zawadi ili kukaza imara zaidi kifungo cha uhusianao mwema na upendo. Muislamu anashuriwa ajitahidi kutoa zawadi kuwapa wengine kila anapopata fursa ya kufanya hivyo na pia anashauriwa kupokea zawadi kwa moyo mkunjufu kila anapo pewa hata kama yeye ni tajiri na huyo anayempa ni maskini. Hebu turejee Hadith zifuatazo tuone jinsi Mtume (saw) anavyotuelekeza katika kupeana na kupokea zawadi:Aysha(ra) amesimulai kuwa Mtume w a Allah amesema: Peaneni zawadi, kwani zawadi inaondoa chuki. (Tirmidh)
Aysha (ra) ameeleza kuwa Mtume wa Allah alikuwa akipokea zawadi akirudisha kitu kin gine badala yake kama badilisho kumpa yule aliyetoa. (Bukh ari).


Jab ir ames imulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Yeyote yule aliyepewa zawadi na akawa na uwezo, na airudishie kwa zawadi nyingine , na yule ambaye hana kitu cha ku rejesha , na atoe shukurani na yule asiyetoa ahsante, ni mkosefu wa shukurani, na yule anayejifanya amepewa kitu na huku hakupewa, anakuwa kama yule aliyevaa magwanda(nguo) maw ili ya uw ongo ( ni mw ongo mkubw a-mnafiki). (Tirmidh, Abu-Daud).Hadith hizi mbili zinatufahamisha kuwa zawadi isielekee upande mmoja tu bali kila anayepokea zawadi naye ajitahidi, kutoa zawadi ya namna nyingine kwa yule aliyempa kama ana uwezo na kama hana cha kutoa atoe ahsante na kumuombea dua aliye mzawadia.
Si tabia ya kiislamu kukataa zawadi- ya aina yoyote iliyohalali. Tunajifunza hili kutokana na hadith zifuatazo:Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Ningalikaribishwa unyayo wa mguu wa mbuzi (uliopikwa) hakika ningalikaribia na ningalipewa zawadi ya mguu wa mbuzi, hakika ningali pokea. (Bukhari).
Anas amesimulia kuwa Mtume wa Allah alikuwa harudishi manukato yoyote (aliyopewa kama zawadi). (Bukhari)Ibn Sayid amesimulia: “Omar aliniteua kukusanya Zakat. Nilipo maliza na kuwasilisha zakat yote kwake, aliamuru nipwe ujira wangu. Nilisema: Nilifanya kwa ajili ya Allah na ujira wangu uko kwa Allah. Alisema: chukua kile ulichopewa kwa sababu niliteuliwa kufanya kazi kama hiyo wakati wa Mtume wa Allah. Aliniteua nikasema namna unavyosema. Mtume wa Allah akaniambia: unapopewa kitu ambacho hukukiomba, basi kula na toa sadaqa. (Abu Daud).Hadith zote hizi zinatufundisha kuwa Muislamu akipewa kitu chochote cha halali asikatae hata kikiwa kidogo namna gani. Na kama hakihitajii sana, basi akipokee kisha atoe sadaqa. Pia tunapata fundisho kuwa Muislamu akikaribishwa na mwenziwe kula kitu chochote kilicho halali asikatae. Alimradi madhumuni ya kutoa na kupokea zawadi siku zote yawe ni kuzidisha upendo, udugu na mahusiano mema kati ya Waislamu na wanaadamu wote kwa ujumla.
Pia kutoleana salamu ni miongoni mwa nyenzo za kujenga upendo baina ya watu kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:


Abu Hurairah (ra) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema; “Ham taingia Pep oni mpaka mw amini na hamtaamini mpaka mpendane. Je, nisikufahamisheni juu ya jambo ambalo mkilifanya mtapendana? Toleaneni salamu baina yenu” (Muslim)
                   
           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 253


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

quran na sayansi
QURANI KATIKA ZAMA ZA SAYANSI NA TEKNOLOJIAAsalaalaamu alykum warahmatullah wabarakaatuh. Soma Zaidi...

Fadhila za kujenga msikiti
Kuna malipo makubwa kwa ambaye amejenga msikiti kwa ajili ya kuoatavradhi za Allah. Soma Zaidi...

swali langu nikwamba Mimi nimeolewa make wa pili nimeishi ndaniya ndoa miaka 22 mume akafikwa na mauti je ninahaki ya kupata mirathi?
Ni ipi haki ya mwanamke kwenye mirathi endapo atafiwa na mume wake, ilihali yeye ni mke wa pili? Soma Zaidi...

DARSA ZA DINI YA KIISLAMU KAMA QURAN, FIQH, SIRA, AFYA, TAJWID NA TAFSIR ZA QURAN
Soma Zaidi...

(ix)Wenye kuhifadhi swala
Waumini wa kweli waliofuzu huhifadhi swala kwa kutekeleza kwa ukamilifu shuruti zote za swala nguzo zote za swala na huswali kama alivyoswali Mtume (s. Soma Zaidi...

ndoto za kweli
Soma Zaidi...

Uandishi wa hadithi wakati wa maswahaba wa mtume (s.a.w)
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kitabu Cha Darsa za dua
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Aina za hadithi
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

dharura
14. Soma Zaidi...

Uhakiki wa hadithi za mtume
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Nani Muadilifu na zipi sifa za mtu muadilifu kwenye uislamu
Uadilifu ni usimamizi wa ukweli na kutoa haki kwa kila anayestahiki kulingana na ukweli. Soma Zaidi...