Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Uandishi wa Hadith Wakati wa Tabi’i Tabi’ina (wafuasi wa wafuasi wa
maswahaba, 201 – 300 A.H).
- Ni kipindi hiki wanazuoni sita walijitokeza waliokusanya na kuchambua kwa umakini mkubwa Hadith sahihi na kuziandika katika vitabu sita mashuhuri kama, “Sahihu Sitta” ambavyo ni;
- Ni kitabu cha Muhammad bin Ismail Abu Abdallah Al-Ju’fi – mashuhuri
kama Imam Bukhari wa mji wa Bukhara, Urusi (194 A.H/810 A.D – 256
A.H/870 A.D).
- Alikusanya Hadith 600,000 na kuhifadhi 200,000 na alihakiki na kuandika
Hadith 7,275 tu katika kitabu chake.
- Kitabu chake ndio namba moja kwa usahihi wa Hadith, mashuhuri kwa jina
la “Al-Jami’u Al-Sahihi” au “Sahihi Bukhari”.
- Ni kitabu cha Abu Husain Muslim bin Al-Hajjaj mashuhuri – Imam Muslim
wa mji wa Misabur, (202 A.H/818A.D – 261 A.H/875 A.D).
- Alikusanya Hadith 300,000 na alizohakiki na kuziandika katika kitabu chake
ni 9,200 tu.
- Kitabu chake ni namba mbili kwa usahihi wa Hadith, mashuhuri kwa jina la
“Sahihi Muslim”
- Ni kitabu cha hadith cha Imam Abu Daud (203 – 275 A.H).
- Alikusanya Hadith 500,000 na alizohakiki na kuziandika ni 4,800 katika
kitabu chake kiitwacho, “Sunan Abi Daud”.
- Ni kitabu cha Hadith cha Abu Isa Muhammad bin Issa bin Sarwa bin
Shaddad, mashuhuri kama Imam At-Tirmidh (209 – 279 A.H).
- Aliandika kitabu cha Hadith mashuhuri kwa jina la, “Jami’u”.
- Ni kitabu cha Hadith cha Muhammad bin Yazid – mashuhuri kwa jina la
Imam Ibn Majah (209 A.H – 295 A.H).
- Aliandika cha Hadith mashuhuri kama, “Sunanu Ibn Majah” au “Sunnah
Ibn Majah”.
- Ni kitabu cha Hadith cha Abu Abdur-Rahman Ahmad bin An-Nasai –
mashuhuri kwa jina la, Imam An-Nasai (214 – 303 A.H).
- Aliandika kitabu cha Hadith mashuhuri kama, “Sunan An-Nasai” au
“Sunnah An-Nasai”.
- Hadith za Bukhari na Muslim ndio daraja la kwanza kwa usahihi na za
Maimam Abu Daud, Tirmidh, Ibn Majah na An-Nasai ni daraja la pili kwa
usahihi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Mnafiki ni yule anayeukubaliย Uislamu mdomoni (kwa kauli tu) lakini moyoni mwake na katika matendo yake anaukanusha.
Soma Zaidi...2:UUMBWAJI KWA MAJI YA UZAZIUumbwaji wa mwanadamu umepitia hatua mbalimbali na haya yote yamefanywa kwa sababumaalumu ili tipate mazingatio.
Soma Zaidi...Waumini wa kweli waliofuzu huwa na khushui (unyenyekevu) katika swala.
Soma Zaidi...Waumini wa kweli waliofuzu huhifadhi swala kwa kutekeleza kwa ukamilifu shuruti zote za swala nguzo zote za swala na huswali kama alivyoswali Mtume (s.
Soma Zaidi...