Navigation Menu



image

kuwa mwenye kusamehe, na faida zake

27.

kuwa mwenye kusamehe, na faida zake

27. Kuwa Mwenye Kusamehe



Muislamu anatakiwa ajenge tabia ya kuwavumilia wengine. Awe na tabia ya kujihesabu. Ajione kuwa naye kama binaadamu wenzake ni mkosaji na angependa asamehewe na wale aliowakosea kwa makusudi au kwa bahati mbaya. Kitendo cha kuwasamehe wale waliokukosea ni kitendo cha ucha Mungu chenye malipo makubwa mbele ya Allah (s.w) kama inavyobainishwa katika aya zifuatazo:


“Na yaendeeni upesi upesi maghufira ya Mola wenu na Pepo (yake) ambayo upana wake (tu) ni (sawa na) mbingu na ardhi. (Pepo) iliyowekewa wamchao Mungu. Ambao hutoa katika (hali ya) wasaa na katika (hali ya) dhiki, na wazuiyao ghadhabu na wanasamehe watu na Mw enyezi Mungu anawapenda wafanyao ihsani. ” (3:133-134)


“Basi vyote hivi mlivyopewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilichoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora na cha kudumu (milele). Watakistahiki wale walioamini na wakawa wanamtegemea Mola wao.(42:36)
“Na wale wanaojiepusha na madhambi makubwa na mambo


mabaya, na wale ambao wanapokasirika husamehe. (42:37)
Mwenye kuwasamehe wengine husamehewa makosa yake na Allah


“Na wasiape wale wenye mwendo mzuri (waumini) na wenye wasaa (katika maisha yao) miongoni mwenu (wasiape kujizuia) kuwapa walio jamaa na maskini na waliohama kwa njia ya Mwenyezi Mungu; na w aachilie mbali, (wapuuze yaliyopita). Je, nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu akusameheni? Na Mwenyezi Mungu ni Mw ingi w a msamaha (na) Mwingi wa Rehema. (24:22).



Naye Mtume (s.a.w) anatufahamisha ubora wa kusamehe katika Hadithi zifuatazo:
‘Uqbah bin Amir (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Ee ‘Uqbah! Je, nikufahamishe juu ya watu wema kuliko w ote katika dunia hii na akhera?” Alijibu Ndio, akasema (Mtume): “Utaendeleza uhusiano mwema na mtu aliyevunja uhusiano kati yako na yeye; utampa yule aliyekunyima; na utamsamehe yule aliyekudhulumu”. (Baihaqi).



Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema kuwa Mussa (a.s), mwana wa Imran, aliuliza: Ee Mola wangu! Nani, katika waja wako anayeheshimika (mwenye hadhi) zaidi mbele yako? (Allah) alimjibu: Yule anayesamehe ambapo ana nguvu au uwezo (wa kutosamehe). (Ba ih aqi).
Hivyo Allah (s.w) anatuusia:


“Shikamana na kusamehe na amrisha mema na wapuuze majahili...” (7:199)


Kukataa kusamehe baada ya kuombwa msamaha na yule aliyekukosea ni jambo ovu. Allah (s.w) hamsamehi yule asiyesamehe wanaadamu wenzake. Ukweli ni kwamba wanayotukosea wanaadamu wenzetu hata tuyaone ni makubwa vipi, ni madogo sana ukilinganisha na makosa yetu kwa Allah (s.w). Inakuwaje sasa tushindwe kusamehe haya makosa madogo madogo na wakati huo tunatamani kusamehewa milima na milima ya makosa yetu?



Hivyo, yule anayetaka kusamehewa na Allah(s.w), basi awe mwepesi wa kuwasamehe wanaadamu wenzake. Kuhusu uovu wa kukataa kuwasamehe wale waliokiri makosa yao na kuomba msamaha, anasema Mtume (s.a.w):



Kama mtu, anakiri makosa yake kwa mwingine na kutaka msamaha, na yule akakataa kutoa msamaha, basi hatanyweshwa maji ya kawthar (huyo aliyekataa, kusamehe). (Tabrani).




                   







           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1513


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Kujiepusha na Chuki na Uadui
26. Soma Zaidi...

HISTORIA YA UANDISHI WA HADITHI
Historia fupi ya uandishi wa Hadith za Mtume (s. Soma Zaidi...

Kushika mwenendo wa kati "Na ushike mwenendo wa kati…." (31:19)
Mwenendo wa kati ni mwenendo ulioepukana na kibri na majivuno kwa upande mmoja na ulioepukkana na udhalili na unyonge kwa upande mwingine. Soma Zaidi...

(viii)Wenye khushui katika swala
Waumini wa kweli waliofuzu huwa na khushui (unyenyekevu) katika swala. Soma Zaidi...

jamii somo la 35
Hutekeleza ahadi zao wanapoahidiana na wanaadamu wenziwao maadamu ni katika mipaka ya Allah (s. Soma Zaidi...

MAADILI MEMA KATIKA UISLAMU
Yajuwe maadili mema yaliyotajwa katika quran Soma Zaidi...

Hadhi na haki za mwanamke katika uislamu
4. Soma Zaidi...

Uandishi wa hadithi wakati wa mtume (s.a.w)
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

jamii somo la 32
Soma Zaidi...

Iv shekh haifai kufunga kwa nia utimize jambo labda kuna kitu unakitaka kwhy unaamua kugunga ili kama kuzidisha maombi kwa mungu jambo lifanikiwe
Ibada yavfubga ni katika ibadavanbazo hufanya nakaribia dini zote kubwa. Ibada hii imekuwaikikabiliw na naswlo mengi. Soma Zaidi...

Kwanini Ni muhimu kusimamisha uislamu katika jamii
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Fadhila za kujenga msikiti
Kuna malipo makubwa kwa ambaye amejenga msikiti kwa ajili ya kuoatavradhi za Allah. Soma Zaidi...