kuwa mwenye kusamehe, na faida zake

27.

kuwa mwenye kusamehe, na faida zake

27. Kuwa Mwenye Kusamehe



Muislamu anatakiwa ajenge tabia ya kuwavumilia wengine. Awe na tabia ya kujihesabu. Ajione kuwa naye kama binaadamu wenzake ni mkosaji na angependa asamehewe na wale aliowakosea kwa makusudi au kwa bahati mbaya. Kitendo cha kuwasamehe wale waliokukosea ni kitendo cha ucha Mungu chenye malipo makubwa mbele ya Allah (s.w) kama inavyobainishwa katika aya zifuatazo:


“Na yaendeeni upesi upesi maghufira ya Mola wenu na Pepo (yake) ambayo upana wake (tu) ni (sawa na) mbingu na ardhi. (Pepo) iliyowekewa wamchao Mungu. Ambao hutoa katika (hali ya) wasaa na katika (hali ya) dhiki, na wazuiyao ghadhabu na wanasamehe watu na Mw enyezi Mungu anawapenda wafanyao ihsani. ” (3:133-134)


“Basi vyote hivi mlivyopewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilichoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora na cha kudumu (milele). Watakistahiki wale walioamini na wakawa wanamtegemea Mola wao.(42:36)
“Na wale wanaojiepusha na madhambi makubwa na mambo


mabaya, na wale ambao wanapokasirika husamehe. (42:37)
Mwenye kuwasamehe wengine husamehewa makosa yake na Allah


“Na wasiape wale wenye mwendo mzuri (waumini) na wenye wasaa (katika maisha yao) miongoni mwenu (wasiape kujizuia) kuwapa walio jamaa na maskini na waliohama kwa njia ya Mwenyezi Mungu; na w aachilie mbali, (wapuuze yaliyopita). Je, nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu akusameheni? Na Mwenyezi Mungu ni Mw ingi w a msamaha (na) Mwingi wa Rehema. (24:22).



Naye Mtume (s.a.w) anatufahamisha ubora wa kusamehe katika Hadithi zifuatazo:
‘Uqbah bin Amir (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Ee ‘Uqbah! Je, nikufahamishe juu ya watu wema kuliko w ote katika dunia hii na akhera?” Alijibu Ndio, akasema (Mtume): “Utaendeleza uhusiano mwema na mtu aliyevunja uhusiano kati yako na yeye; utampa yule aliyekunyima; na utamsamehe yule aliyekudhulumu”. (Baihaqi).



Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema kuwa Mussa (a.s), mwana wa Imran, aliuliza: Ee Mola wangu! Nani, katika waja wako anayeheshimika (mwenye hadhi) zaidi mbele yako? (Allah) alimjibu: Yule anayesamehe ambapo ana nguvu au uwezo (wa kutosamehe). (Ba ih aqi).
Hivyo Allah (s.w) anatuusia:


“Shikamana na kusamehe na amrisha mema na wapuuze majahili...” (7:199)


Kukataa kusamehe baada ya kuombwa msamaha na yule aliyekukosea ni jambo ovu. Allah (s.w) hamsamehi yule asiyesamehe wanaadamu wenzake. Ukweli ni kwamba wanayotukosea wanaadamu wenzetu hata tuyaone ni makubwa vipi, ni madogo sana ukilinganisha na makosa yetu kwa Allah (s.w). Inakuwaje sasa tushindwe kusamehe haya makosa madogo madogo na wakati huo tunatamani kusamehewa milima na milima ya makosa yetu?



Hivyo, yule anayetaka kusamehewa na Allah(s.w), basi awe mwepesi wa kuwasamehe wanaadamu wenzake. Kuhusu uovu wa kukataa kuwasamehe wale waliokiri makosa yao na kuomba msamaha, anasema Mtume (s.a.w):



Kama mtu, anakiri makosa yake kwa mwingine na kutaka msamaha, na yule akakataa kutoa msamaha, basi hatanyweshwa maji ya kawthar (huyo aliyekataa, kusamehe). (Tabrani).




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jifunze Main: Dini File: Download PDF Views 2457

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Bongolite - Game zone - Play free game    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Assalam Baada yakufariki wazazi wake mtume alilelewa nanani???

Mtume Muhammad s.a.w amezaliwa yatima asiyena baba. Lakini hii haikumfanya asipate maelezo bora yaliyo mazuri. Je unajuwa aliyemlea baada ya kufariki kwa mama yake?.

Soma Zaidi...
(xi)Hutoa Zakat na Sadakat

Waumini wa kweli waliofuzu hutoa Zakat wakiwa na mali na hutoa misaada na huduma waziwezazo kwa wanaadamu wenziwe kwa kadiri ya haja ilivyojitokeza.

Soma Zaidi...
Nani Muadilifu na zipi sifa za mtu muadilifu kwenye uislamu

Uadilifu ni usimamizi wa ukweli na kutoa haki kwa kila anayestahiki kulingana na ukweli.

Soma Zaidi...
(x)Wenye kuepuka lagh-wi

Waumini wa kweli waliofuzu hujiepusha na Lagh-wi.

Soma Zaidi...
Uandishi wa hadithi wakati wa mtume (s.a.w)

Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...